Hali mbaya: Nimemwona jamaa anatembeza chumvi kuuza

Kuna mwingne nilikutana nae anauza ndizi mbivu kumi kwa 500/= , mwengine Parachichi tatu 500/=,
Natafakar sana ,nawaonea huruma sana dada zangu na mama zangu wanao zungusha hivi vitu vidogo vidogo , sema tu sina cha kuwasaidia

Niliumia sana kukutana na mbaba katika mazungumzo aliniambia ana miaka 48 , ni mkubwa kwa Baba yangu mzazi afu anauza sumu ya panya ,mbuu ,na vitu vingine vidogo dogo. Kuna saa unaamua kunua bidhaa ya mtu kwa kumuonea tu huruma na sio kwamba una uhitaji nayo

Unakutana na kijana anauza spana namba zote ,plaizi. Tafakari anazunguka mchana kutwa na mzigo mzito hivo :

Haya haya maisha yaache tu ,unaweza jiona unateseka sana ila ukamuona mwenzako ukasema hapana hauteseki

Maisha ni fumbo ,Maisha yanategemeana .Tusaidiane sana

Kama una uwezo usisite kumsaidia mtu
Umenikumbusha kuna baba mmoja mtu mzima ukipanda basi toka mwanza kwenda shinyanga ukipapita misungwi kwa mbele anapanda yule baba ana ungo anauza pipi na jojo jamanii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sidhani kama unaumia kama mimi navowaonaga wamama barabarani wamepakata watoto wao na visinia wanauza karanga 100/= kwakwel wale sidhani hata pesa wanayopata inawalisha hata kwa siku nzima yani nikiwaona kama nina coins, zote nitanunua hizo karanga ingawa najua wala sikuwa na hamu nazo ila basi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu comment yako imenisisimua sana ndio tujiulize critically thinking kwamba service ya ndege bilioni 6 inamsaidia nini huyo mama ..Na mind you huyo ni mmoja Kati ya wengi.....au uki buy airplane kwa cash ..how does it touch a mother with kids selling cashewnuts for just 100 per pact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha kuna baba mmoja mtu mzima ukipanda basi toka mwanza kwenda shinyanga ukipapita misungwi kwa mbele anapanda yule baba ana ungo anauza pipi na jojo jamanii

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna mzee mmoja hivi naye anafanya biashara Kwa jeuri sana ,anapanda kwenye basi na bagia zake anasema anauzia watu wanne tu ,anasema nyoosha mkono kama unataka ,wakitimia wanne hauzi tena na ukihitaji anakujibu vibaya ,anashuka nazo

Duh wakti mwengine Biashara ni nyota tu ya mtu huyo mzee kazoeleka hivo, na kiburi chake kimemfanya watu wamkubali
 
Kuna mzee mmoja hivi naye anafanya biashara Kwa jeuri sana ,anapanda kwenye basi na bagia zake anasema anauzia watu wanne tu ,anasema nyoosha mkono kama unataka ,wakitimia wanne hauzi tena na ukihitaji anakujibu vibaya ,anashuka nazo

Duh wakti mwengine Biashara ni nyota tu ya mtu huyo mzee kazoeleka hivo, na kiburi chake kimemfanya watu wamkubali
Ahahhaahhahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu ni wanafiki na wapuuzi sana , unajua hizi identity fake zinadanganya sana , kama inalipa kwa nini yeye hajawa muuza karanga sasa ? , shenzi kabisa .Watu wanaleta masikhara kwenye mambo ya msingi , utasikia kima mmoja kaajiriwa serikalini anawaambia graduates eti wajiajiri , yeye kwa nini hataki kustaafu na kujiajiri ili kutoa fursa kwa wengine ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndivyo walivyo mkuu!Wanajificha nyuma ya hizi fake id, ndiyo mumiani wenyewe hao! Kuja miongoni mwa wananchi kuwadanganya, kumbe ni mbwa mwitu wenye ngozi ya kondoo!Nimeshawashtukia wengi sana.Part of propaganda and manipulation! Wenyewe wanaita "kula na kipofu"
 
Mbona hamuwashangai wauza pipi na Big G!?,
wamepanga chumba wanalipa bills zote.
Funny thing kuhusu biashara ndogo ndogo inaingiza mkwanja kuliko unavyodhani, ukiona wafanya biashara wa chumvi wamekua wengi jua kuna pesa hapo, ukiona wauza viberiti wengi jua kuna pesa hapo, jenga mazoea nao kisha waulize wanapata faida vipi ndio utashangaa.

Be crazy, Be Weird, Be whatever coz life is too short to be anything but HAPPY.
Upo sahihi kabisa kwenye katoni ya chumvi zipo pakti 40 gawa kwa 3 ni 13 mara 1000 ni sh 13000 na huku yeye kanunua sh 8000 hivyo ana faida sh 5000 kwa siku anauza katoni 4 mpaka 5 jumla sh 20,000 faida kwa siku.Kwa mwezi 600000 hajakuzidi wewe mwenye kuajiriwa?huyu hana makato
 
Nipo ighanuda huku nauza nyimbo ,movies,
Wimbo 1 Audio -200
Video-300
Movies:Series kipande100 kamani ya kihindi yenye dakika 18-21
Kikorea,kizungu zenye dakika 40 mpaka lisaa 200
Single movie-500

Na nina mpango wa kuwa bilionea 😂😂😂😂

Nawashukuru wana ighanuda wananiweka kijijini
 
Back
Top Bottom