Hali inatisha bungeni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kama mdhaha vile. Moto unazidi kufukuta kati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wanaotoka vyama vya upinzani bungeni, anaandika Faki Sosi.

Mpasuko katika makundi hayo mawili (chama tawala na upinzani) unatishia usalama wa umoja unaohitajika katika kusimamia serikali kwa mujibu wa chombo hicho.

Taarifa zilizofikia mtandao huu zinaonesha kwamba, tayari uhasama kati ya CCM na upinzani umefika pabaya na hata kutengana katika baadhi ya mambo ambayo walikuwa wakifanya kwa pamoja nje ya Bunge.

Pia kauli za matusi, kejeli na dharau zinaendelea kushamiri jambo ambalo limezidisha mpasuko huo. Hatua hiyo imeongeza kuyumba kwa Bunge.

Msingi wa kukithiri myumbo huo ni kutokana na hatua ya upinzani kususa kushiriki vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge.

Hatua ya wabunge wa upinzani jana kutoka bungeni huku wakiwa wamefunga midomo yao kwa plasta imekwenda sambamba na kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii inayounganisha ikiwa ni pamoja na ule wa Whatsapp.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, hatua hiyo ya kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii inatokana na wabunge wa CCM kudaiwa kuwa wanachangia kumpa jeuri Dk. Tulia kuendesha Bunge kwa ubabe pia kuwaminya wapinzani.

Hatua hiyo ya wabunge hao kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii ilitanguliwa na ile ya wabunge wanawake kutoka upinzani kujiondoa kwenye umoja wa wanawake wa wabunge wote (wanawake) baada ya upinzani kutukanwa na mbunge wa CCM kwamba, ndani ya upinzani mwanamke hapewi nafasi mpaka aitwe baby’ kwa maana ya kutoa penzi.

Jana wakati wabunge wa upinzani wakitoka nje ya Bunge na kumsusia Dk. Tulia kuendesha kikao hicho, walikuwa wakizomewa na wabunge wa CCM.

Hatua ya upinzani kutoka nje ni mwendelezo wa kugomea vikao vinavyoongozwa na Dk. Tulia ambaye anatuhumiwa kuminya uhuru wa wabunge wa upinzania na kupendelea wabunge wa CCM.

Wabunge hao wa upinzani baada ya kutoka nje, walikwenda moja kwa moja kwenye Hoteli ya African Dream na kufanya kikao chao cha faragha.

Hata hivyo, hatua ya kuziba midomo kwa plasta imeelezwa kwamba, ni kuonesha wazi kuwa Bunge linawafunga midomo wapinzani na kuminya demokarasia.

Staili ya jana ni tofauti na ile ya awali ambapo wabunge walikuwa wakitoka bungeni kimya kimya, safari hii wametoa ujumbe mpya kwa Dk. Tulia.
 
Sasa kujiondoa kwenye watsup ndio mpasuko,kama ndio hivyo basi hii mipasuko huwa inatokea kila siku kwenye jamii,maana kila uchweo yanaanzishwa magroup kwenye watsup na watu wanajiondoa.
 
Mungu mjalie afya njema Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania arudi kuendesha chombo ambacho kinaonekana kumpwaya msaidizi wake. Amen.
 
All the best. japo jjitihada wanazofanya ni kama kupiga zomali mbele ya mbuzi ukitegemea atafurahiya toni ya zomali hiyo
 
CCM ni ukoma ulioitafuna nchi hii kwa muda mrefu hivyo ni busara tu kujitenga nao.
Zanzibar walitutangulia kuliona hili!
Kaa mbali na kijani na njano, ni rangi za kishetani!
 
Wewe naye, yaani kufunga midomoni plasta na kujitoa Whatsap ndiyo inatisha? Mimi nilidhani kifaru kilichoibiwa kinashambulia jengo la bunge.
 
Wabunge wa ccm kweli wanakosa maarifa. Sasa wao uogonvi wa Naibu spika na wapinzani wanajiingiza wa nini? Hapo hawajui ndio wanafanya hoja zao zionekane kweli ni za msingi
Ila wapo wabunge makini wa ccm hawataki kabisa kuunga mkono ujinga wa NS wala wabunge wenzao wasio jitambua
 
Tena jana walilewa ile mbaya baada ya kutoka hotelini wengine nilikutana nao City Style wakigida ugimbi.
Si unaona sasa mwananchi, anaamka asubuhi, anaenda kujipanga foleni anapiga kura..anaambulia nini?.usanii, makaratasi, wabunge wake kujifungia hotelini. Kugida ugimbi. nk. Jamani ukawa kuweni na huruma.
 
Kama mdhaha vile. Moto unazidi kufukuta kati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wanaotoka vyama vya upinzani bungeni, anaandika Faki Sosi.

Mpasuko katika makundi hayo mawili (chama tawala na upinzani) unatishia usalama wa umoja unaohitajika katika kusimamia serikali kwa mujibu wa chombo hicho.

Taarifa zilizofikia mtandao huu zinaonesha kwamba, tayari uhasama kati ya CCM na upinzani umefika pabaya na hata kutengana katika baadhi ya mambo ambayo walikuwa wakifanya kwa pamoja nje ya Bunge.

Pia kauli za matusi, kejeli na dharau zinaendelea kushamiri jambo ambalo limezidisha mpasuko huo. Hatua hiyo imeongeza kuyumba kwa Bunge.

Msingi wa kukithiri myumbo huo ni kutokana na hatua ya upinzani kususa kushiriki vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge.

Hatua ya wabunge wa upinzani jana kutoka bungeni huku wakiwa wamefunga midomo yao kwa plasta imekwenda sambamba na kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii inayounganisha ikiwa ni pamoja na ule wa Whatsapp.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, hatua hiyo ya kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii inatokana na wabunge wa CCM kudaiwa kuwa wanachangia kumpa jeuri Dk. Tulia kuendesha Bunge kwa ubabe pia kuwaminya wapinzani.

Hatua hiyo ya wabunge hao kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii ilitanguliwa na ile ya wabunge wanawake kutoka upinzani kujiondoa kwenye umoja wa wanawake wa wabunge wote (wanawake) baada ya upinzani kutukanwa na mbunge wa CCM kwamba, ndani ya upinzani mwanamke hapewi nafasi mpaka aitwe baby’ kwa maana ya kutoa penzi.

Jana wakati wabunge wa upinzani wakitoka nje ya Bunge na kumsusia Dk. Tulia kuendesha kikao hicho, walikuwa wakizomewa na wabunge wa CCM.

Hatua ya upinzani kutoka nje ni mwendelezo wa kugomea vikao vinavyoongozwa na Dk. Tulia ambaye anatuhumiwa kuminya uhuru wa wabunge wa upinzania na kupendelea wabunge wa CCM.

Wabunge hao wa upinzani baada ya kutoka nje, walikwenda moja kwa moja kwenye Hoteli ya African Dream na kufanya kikao chao cha faragha.

Hata hivyo, hatua ya kuziba midomo kwa plasta imeelezwa kwamba, ni kuonesha wazi kuwa Bunge linawafunga midomo wapinzani na kuminya demokarasia.

Staili ya jana ni tofauti na ile ya awali ambapo wabunge walikuwa wakitoka bungeni kimya kimya, safari hii wametoa ujumbe mpya kwa Dk. Tulia.

Huo mpasuko ndo mwanzo wa kuijenga nchi, tutafika mahala tutajua mchawi wetu hasa ni nani. Tuone kama kweli ccm wakiwa peke yao wanafanya ya maana au la. Simply time will tell
 
Wewe naye, yaani kufunga midomoni plasta na kujitoa Whatsap ndiyo inatisha? Mimi nilidhani kifaru kilichoibiwa kinashambulia jengo la bunge.

Mkuu..
Nadhani wewe ni mshabiki/mpiga vigelegele..

swali; hicho kifaru ulichokua unakiota wewe, unafahamu kua ni scraper/target kwenye shooting range exercise..???
 
Kuna wakati salamu ya wana ccm ilikuwa inasema "zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm"

Baadae wakabadili wakawa wanasema "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa ccm"

Siku hizi hawasemi kabisaaaaa

Bali wanadumisha fikra hatarishi za chama chao chahovyo!!
 
Hawa wanaojiitaa wanahabari huru kuna mda nao wachunguzwe akili huwezi sema bunge limefika pabayaa eti kisa mtu kajitoa kwenye group la whasapp...jitathimin mdau akili yako kama ya mbowe
 
Back
Top Bottom