Thesis
JF-Expert Member
- Aug 30, 2017
- 1,805
- 3,085
Hoja yako ina mantiki sana bwana Ngabu, isipokuwa nadhani unapotofautiana na watu wengi nadhani ni swali je, hivyo vitu vinagusa watu wengi kiasi gani. Ukizungumzia ujenzi wa darasa na zahanati hivi ni vitu vinagusa maisha ya watu wote matajiri na masikini. Ukiongelea ujenzi wa barabara za lami na miundombinu ya umeme na njia ya treni unagusa maisha ya watu wote. Ila ukiongelea ndege, sioni kama unagusa maisha ya watu wengi zaidi ya wachache tu!Bila miundombinu kuna maendeleo?
Wananchi watawezaje kujikwamua kutoka kwenye hali zao kama miundombinu ni changamoto?
Zamani nakumbuka safari ya kwenda Shinyanga au Mwanza ilikuwa inachukua siku karibu tatu kwa treni ya TRC.
Kwa basi ndo usiseme kabisa. Hata kujua ilikuwa inachukua muda gani ilikuwa haijulikani maana changamoto zilikuwa tele.
Pale Sekenke kupita ilikuwa ni mbinde. Kama ni msimu wa mvua ndo sahau kabisa. Barabara zilikuwa za vumbi na tope tu.
Siku hizi mambo yamebadilika. Dar-Mwanza au Mwanza-Dar kwa basi ni safari za masaa tu!
Kujenga spitali si maendeleo? Spitali bila jengo inawezekana kweli?
Kujenga mashule si maendeleo? Madarasa si majengo?
Madarasa kuwa na umeme na madawati si maendeleo? Madawati siyo vitu?
Bi mdogo wangu [Kisura] shuleni kwao wanafundishwa hadi kutumia MS Applications. Mambo sijui ya PowerPoint, Excel spreadsheets, Word, nk., anayajua utadhani alizaliwa nayo. Wakati mwingine hata mimi ananionyesha vi tricks ambavyo sivijui. Jana nilikuwa nahangaika na ku-unfreeze pane, chap chap akanionyesha nilipokosea.
School district yao wanapewa iPads. Homeworks zao zinakuwa uploaded humo na siku mtoto asipoenda shule kwa ajili ya kuumwa au sababu yoyote ile, anafuatilia wenzake walichosoma siku hiyo na anakuwa hayuko nyuma akirudi shule.
Sasa iPad siyo kitu?
Sasa hivi kwenda Kigamboni ni rahisi. Unaenda kwa barabara, unavuka daraja, tayari ushafika. Zamani ilikuwa hadi upande pantoni!
Daraja siyo barabara? Barabara siyo muundombinu? Barabara bora si za muhimu katika ya usafirishaji na uchukuzi? Biashara zinaweza kwenda vizuri bila uchukuzi?
Bodaboda, bajaji, na simu janja ni vitu, siyo? Haya, siku hizi bongo kuna door to door delivery services. Na vitendea kazi ni hivyo vitu.
Maofisini watu wanapelekewa msosi. Unapiga simu kwa mchoma mishkaki, mchoma mishkaki anakufungia anampa kijana wa bodaboda anakuletea. Hapo mawasiliano yote yanafanyika kwa simu. Malipo nayo pia. Hatuna Grubhub, Doordash, wala UberEats lakini concept ni ile ile tu....quick food delivery.
Hayo siyo maendeleo?
Naelewa alichokuwa anasema Nyerere, ila, nadhani ama hakuelezea vizuri au labda nyakati sasa zimebadilika na alichokisema kipindi hicho hakipo applicable kwa hali ya sasa.
Hapa penyewe JF watu tupo kila kona ya dunia hii lakini kupitia vitu [simu janja, kompyuta, tablet] tunakutana na kujadiliana na kubadilishana mawazo na kuelimishana na kusaidiana.
Hayo siyo maendeleo? Yote hayo yangewezekana bila vitu?
Kwa maisha ya sasa, maendeleo ni watu pamoja na vitu.
Vitu ni vya watu. Vitu na watu vinafungamana.
Mimi naunga mkono miradi mingi sana ya Serikali ya awamu ya tano, kitu nisichounga mkono ni Mradi wa ndege tu! Mradi huu siuungi mkono kwasababu zifuatazo
1. Usafiri wa ndege kabla ya ATCL haukuwa na shida yoyote, hivyo hapakuwa na haja ya serikali kuwekeza kwenye huduma hiyo kwasababu huduma hiyo ilikuwepo;
2. Ushindani katika biashara ya anga ni mkubwa sana na serikali haijawahi kuwa efficient kwenye kusimamia biashara. Sitegemei kama shirika hili litazalisha faida na kurudisha gharama za uwekezaji;
3. Shirika limefufuliwa kwa nguvu na hoja za mhe. Rais, sidhani hata kama kuna sustainability plan after Magufuli;
4: Uwekezaji wa kununua ndege ni gharama sana na hauhudumii sehemu kubwa ya jamii. Fedha tulizowekeza kununua ndege kama tungeboresha hospitali zetu za kanda za rufaa, na hospitali za mikoa nadhani tungegusa maisha ya watu wengi zaidi. Aidha, suala la zahanati vijijini bado ni changamoto, bado kuna vijiji havina zahanati, kama tungewekeza huko tungegusa maisha ya watu wengi.
Hizo ndio sababu za msingi kabisa kuwa suala la uwekezaji kwenye ndege bado halijaniingia moyoni. Miradi mingine yote inaogusa maendeleo ya wananchi, Magufuli aendelee kuwekeza hata kama haionekani faida yake leo lkn kesho itaonekana.
Lkna yote kwa yote serikali inavowekeza lazima iwe makini hata kama miradi hiyo itakuwa na manufaa kwa wananchi wengi ipo haja ya kuangalia mradi huo utakuwa na manufaa gani kiuchumi kwa wananchi kwa wakati uliopo. Lazima mradi uangaliwe utaongeza kiasi gani cha fedha kwenye mzunguko. Mradi wa wa stigler, flyovers na standard gauge yote inafaida kwa wananchi wengi hapo baadae baada ya kukamilika lkn kwa sehemu kubwa kwasasa hivi inatoa fedha nje kuliko kuongeza mzunguko wa fedha kwenye uchumi wa nchi. Kwa mantiki hiyo, miradi hii kwa wakati uliopo itafifisha sana mzunguko wa fedha kwenye uchumi wa nchi, ilitakiwa kujengwa kwa awamu na sio kwa mkupuo kama tulivifanya.