Hali imekuwa ngumu sana Wakuu. Nidhamu ya kutunza hela inahitajika

Amani bm 150

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
315
487
Biashara zimekua ngumu sana wanajamvi, mahitaji ya maisha yamekua mengi, hali za biashara zinadorora kila leo.

Watu tuna mikopo ila hayo marejesho tunapata tabu sana kurejesha kuna wakati nafikria labda nihamie mjini Dar, lakni sasa huo mziki wa kuhamia Dar ni bora nikomae hapa hapa Mbeya

Maana kuna jamaa zangu waliwahi kuhamia Dar walirudi wako hoi balaaa bora ya mimi tena. Tuache masihara sasahivi hata nidhamu ya kutunza hela inahitajika sana.
 
Biashara zimekua ngumu sana wanajamvi mahitaji ya maisha yamekua mengi hali za biashara zinadolola kila leo watu tuna mikopo ila hayo marejesho tunapata tabu sana kurejesha kuna wakati nafikria labda nihamie mjini dar lakni sasa huo mziki wa kuhamia dar ni bora nikomae hapa hapa mbeya tena mana kuna jamaa zangu waliwahi kuhamia dar walirudi wako hoi balaaa bora ya mimi tena.ila tuache masihara sasahivi hata nidhamu ya kutunza hela inahitajika sana.
Hali ni tete. Labda tuanze kuuza manguo mazito na hili barid huenda zikatembea😁😁😁😁
 
Ukiingia maeneo yastarehe, huwezi kuamini unachosema kama ni sahihi

Hahaa mkuu hata sehemu za starehe sahizi hazina kasi sana ka ya mwezi december kuja mpaka mwezi wa tatu mi nipo mbeya kila siku napita sehemu moja hivi ina itwa mbeya pazur ni sehemu imechangamka sana tu kwa apa mbeya mjini ila saizi aisee hata hapana ile kasi iliokuepo labda sehemu zingine huko ila huku kwetu aisee we acha tu
 
Back
Top Bottom