Hali Ilivyo katika mipaka kati ya Tanzania na Burundi leo

Singidan

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
876
923
Kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, leo nimefika moja kati ya mipaka inayotenganisha Tanzania na Burundi;

Nimefika katika soko la Kimataifa la Mpuza. Hili ni soko ambalo Geography yake ni kati ya kijiji cha Mhange, Kakonko(Tanzania) na Kasenyi, Cankuzo(Burundi).

Hali ya Soko.
Kusema ukweli hali ni ngumu, soko limefungwa. Hakuna kuingia Burundi Wala Kuja Tanzania. Warundi walioko huko kwao nikiamua nawaona kwa macho tu,

Nilienda kununua kuku kutoka Burundi lakini imeshindikana. Watanzania waliokuwa na bidhaa kama nyanya na vingine wameduwaaa tu.

For surely, hili ni soko ambalo linawahudumia na kuwanufaisha watanzania kwa asilimia kubwa hasa wilaya ya Kakonko kwani hata kambi ya wakimbizi ya Mtendeli pia hutegemea kuku kutoka hapa kwa ajili ya kitoweo.

Lakini yote kwa yote, Uhai ni kitu muhimu kuliko vyote ndiyo maaana wenzetu Burundi wemechukuwa tahadhari.
 
Wabongo tunajuana tulivo.

HaDi umefika hapo (licha ya tahadhari zote zinazotolewa) najua lazima biashara ifanyike.

La msingi jalini afya zenu kwanza na za wale mlowaacha nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Upo sahihi, tuko na tahadhari.... Nimeishia ku zoom Polisi wakiwa wameshika Bunduki tu!! Burundi hawana mchezo. Nadhani bado hakuna Case ya Corona huko kwao.
 
Back
Top Bottom