kiraremapojoni
JF-Expert Member
- Nov 30, 2018
- 391
- 512
Jana nilibahati kakukaa wa wanazengo katika mitaa ya kati kujadili changamoto za kimaisha na hasa kwa wanaoishi mjini. Nimegundua kwamba maisha ni magumu kwa kila mtu sio mfanyakazi wala mfanyabiashara. Kila mtu analalamika upande wake
Mfanyakazi anakwambia hakuna nyongeza ya mshahara kwa mwaka wa tatu mfululizo na hata zile haki ambazo ni za kikatiba pia hawapati. Suala la masaa ya ziada ndo limekuwa kama anasa ingawa wanakaa kazini na wanatekeleza majukumu. Wanapojaribu kudai wanaambiwa wanatekeleza majukumu yao wakati mkabata wa ajira unawaamuru kufanya kazi mpaka saa tisa unusu au saa kumi
Mfanyabiashara analia kushuka kwa mauzo kiasi ambacho anakaa na bidhaa zake kwa muda mrefu na hii inamuongezea gharama za kuhifadhi mzigo (Storage costs) na anapopata mteja anauuza kwa bei ya hasara nagalau afidie gharama nyengine za kuendesha duka. Wale ambao wanamioyo dhaifu ndo wanaamua kufunga biashara mara baada ya kuona amepata hasara kwa miaka miwili mfu;lulizo na mtaji unakata bila ya sababu yamsingi.
sijazungumzia kundi athirika la vyeti feki na wale waliotumbuliwa ambao kesi zao hazijaanza wala hawajajua kama zitakwisha lini. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa