Hali halisi ya mazao shambani

King66

Senior Member
Aug 12, 2017
103
106
Wakuu habari zenu,

Kutokana na hali ya mvua mwaka huu ilikuwa sio ya kuridhisha sana kwa baadhi ya maeneo, tulitegemea kwa sisi wakulima Bei za mazao zingepanda haraka haraka, lakini hali si hali hadi leo bei mbaya.

Mahindi kwa mfano bei 40000/= Angalau kidogo Alizeti bei inaleta matumaini. Sasa wakuu kuna matumaini kweli bei kuwa nzuri (Sana sana Mahindi).

Vipi wale mliopo mipakani huko Namanga, Holili, Mtukula, bei zina uelekeo mzuri? Ili tuendelee kujipa moyo. Kwa kweli kilimo pasua kichwa tunapambana, walanguaji nao wanatupiga haswaa!
------------------------------------------------
------------------------------------------------
Update;
Baada ya kufanya uchunguzi wangu, nimefahamu yafuatayo:
i) Wakulima wengi bado mahindi hatujavuna, na kama waliovuna ni wachache.
ii) Walanguzi wanatusumbua bure sababu wanajua hatuna pa kuyapeleka
iii) Bei halisi ya mahindi bado haijapanda ukifananisha na mazao mengine kama alizeti
Hivyo ni bora tukomae na shida zetu tukisubiri bei angalau ipande kidogo!
 
Back
Top Bottom