Hali halisi ya maisha ya walimu wa Tanzania

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
2,087
2,193
Habari za asubuhi wadau wa elimu. Kama tujuavyo , walimu ni msingi mkuu wa maendeleo ya taifa lolote duniani. lakini katika taifa letu ualimu umekuwa ukionekana kama ni taaluma ya watu wanaotoka katika familia masikini na waliopata ufauru mdogo katika mitihani yao.

Serikali imekuwa ikifanya jitihada kuinua elimu lakini bado unakuta walimu wanalalamika na kukata tamaa, wengine mpaka kujuta kwanini walisomea ualimu. Tumeshuhudia katika awamu hii ya utawala wa magufuli hakuna ongezeko la mishahara na ajira zimesitishwa kwa kitambo sasa hari inayopelekea walimu kuwa na majukumu mazito zaidi kutokana na uchache wa walimu.

Lengo la kuanzisha thread hii ni kutaka wadau wa elimu tuweze kujadili changamoto/matatizo yanayowakumba walimu na nini kifanyike. endelea kuusikiliza wimbo huu ukiwa unachangia hoja yako hapaa. . nawasilisha
 
Tatizo elimu tumewaachia wanasiasa sampuli ya luside, maji mrefu, mlinga, msukuma eti hawa ndio wanafanya maamuzi ya uelekeo wa elimu ya nchi hii, this is ridiculous! Ndio maana wanakuja na division five

Eti Bashite mwenye division zero anamfuta cheo afisa elimu. Kwa mawazo yake ya kibashite bashite anafikiri ataweza kuinua kiwango cha elimu kwa kujenga ofisi huku akiwadhalilisha walimu. Tutasubiri sana
 
Wacha mnyanyasike mpaka mtie akili!

Mkipewa ile Miform six kwenye siku kuu ya wafanyakazi mnabaki mmekenua meno badala ya kuraise changamoto zenu!

Gomeni kuhudhuria Mei mosi!!
alaaaaah
 
hahahahaha nimecheka kama kichaa
 
Mwalimu kopo la chumvi ! Umuhimu wake ni pale tu inapohitajika hiyo chumvi! Ni shida na kero,haliangaliwi kama mke wa raisi ni mwalimu,waziri ni mwalimu nani hajui changamoto za ualimu? Nani anasilia kilio chao,kiki ndio zinawaendesha wanasiasa wanataka sifa za vitu wasivyovifanya kumbe ukifanya jambo zuri sifa inakufata! Chakuchekesha jana kanipigia simu rafikiangu mwalimu wameitwa kwenye semina tangu asubuhi chakula wamekula saa 11 jioni na posho 30000 bila kujali wapi mwalimu anatoka heeee! Halafu ni semina kubwa hiyo na inauzito wake!
 
Kwa kweli tumekata tamaa hata hamu ya kwenda kazini haipo ni kulala lala tu hakuna namna
 
Huko makazin sasa ndo usiseme walimu unaa unaa, usenge ndo usiseme moja likipata fursa hzo za kisenge ndo litawanafikia wenzake mpaka basi kujifanya lenyewe linyenyekevu kwa bosi.

In short walimu hatupendani wenyewe kwa wenyewe sasa nani atasimama kutupigania

Iendelee tu hivi hivi
 
Maisha ya Ualimu yanafanywa kuwa magumu na walimu wnyewe. Nina uzoefu mdogo wa miaka 7 ktk Ualimu ila nimejifunza yafuatayo.
1.kiongoz yyte ambae alipitia/alishawai kuwa mwalimu ni adui wa walimu kwa kuwa atatumia mda mwingi kuwakanyaga walim wenzake.
2.Siasa imeharibu na itaendelea kuharibu hadhi ya Walimu kwa kua kila mwanasiasa anaona sehemu ya kupatia nafuu ni sekta ya elimu. Mfano elimu bure imekuja kumkanda miza mwl. Wkt wazazi wanachangia elimu hasa sekondari walimu walipata nafuu zifuatazo i) Mkuu wa shule aliweza kudhibiti walimu kwa kuwafanya wawepo kituoni mda mwingi pale alipo weza kupata fungu japo la kutoa maji ya chai shuleni. Michango ya Ada ilisaidia hta vinapofanyika vikao Mkuu kuweza kutoa chakula cha mchana kwa walim wake ili kuzuia kuharibu ratiba ya masomo muda wa saa za kazi. ii) Michango ilisaidia walimu kupata viti vya kukalia akiwepo ofisin wkt wa kufanya maandaliz kwa kua mzazi alichangia dawati, tofauti na leo hii Serikali imejifanya imetaka kubeba hili jukum lakin imeshindwa. Shule za pembezoni mwa nchi bado zinaupunguf wa madawati. Mwl hakai chini mpk mwnafunzi atege akachukue kiti chake, wkt wa mitihani wnafunzi wanafunzi wanakaa wa wili kiti kimoja.
3. Kwnn michango haikufutwa kwenye sekta zengine kama Afya? Maji? Ambayo binadam akikosa athari yake itapatkana mara 1kuliko elimu?.
4. Naendelea kujifunza kuwa Hakuna dhamira ya kweli ya kuboresha hii sekta na hatimae kizazi kilichopo na kijacho cha maskin kitaumia zaid mana Serikali haiwez kuwa mdau pekee ambae ataweza kubeba mzigo wa gharama ya elim na taifa likabaki salama.
 
Ulichosema ni sahihi 100%. Kwa kweli hatakuja atokee kamwe wa kumsemea na kumwinua mwl.
 
Mkuu wa sasa ni Mwalimu, lakini jaribu kumwita mwalimu fulani uone! Aliyekuwa anafurahia kuitwa Mwalimu ni Nyerere tu! Alipenda aitwe "Mwalimu Nyerere" !
 
Ualimu ni fani pekee yenye watumishi wengi katika utumishi wa umma. Wateja wake pia ni wengi na wa full time. Ukitaka kuwalipa vizuri walimu utatumia sehemu ya bajet. Walimu ni sawa na watoto wengi waliozaliwa nyumba moja. Ni ndoto walimu kuja kulipwa vizuri hapa Afrika.
Suluhisho ni walimu kujiongeza kwa miradi binafsi
 
Majeshi ndy yanakula nchi.
 
Mwalimu kopo la chumvi ! Umuhimu wake ni pale tu inapohitajika hiyo chumvi! Ni shida na kero,haliangaliwi kama mke wa raisi ni mwalimu,waziri ni mwalimu nani hajui changamoto za ualimu? Nani anasilia kilio chao,kiki ndio zinawaendesha wanasiasa wanataka sifa za vitu wasivyovifanya kumbe ukifanya jambo zuri sifa inakufata! Chakuchekesha jana kanipigia simu rafikiangu mwalimu wameitwa kwenye semina tangu asubuhi chakula wamekula saa 11 jioni na posho 30000 bila kujali wapi mwalimu anatoka heeee! Halafu ni semina kubwa hiyo na inauzito wake!
Kibaya zaidi hata hiyo chansi ya semina kuipata itakuwa kmtoa kidogo mkuu wake wa kituo.
 
Kila mara nasema sekta ya elimu msingi yaani,shule za msingi na sekondari bila kupata chanzo cha uhakika cha mapato kuendesha hii sekta miaka nenda rudi hakutakuwepo maendeleo yoyote kwenye hii sekta.

Sekta kubwa kama hii haiwezi kuendeshwa kwa kutegemea ruzuku kutoka serikalini na misaada ambayo inatolewa kutokana na kampeni za kuomba omba.

Suluhisho: Hii sekta ili iweze kujimudu inabidi iwekewe misingi ya kujitegemea kwa maana kuwa na vyanzo vya mapato. Hapa ada haitaepukika. Serikali isaidie kulipia ada wale ambao ni yatima na familia duni kupitia miradi ya TASAF.

Ada hiyo itasaidia kuwepo na mafungu ya kuandaa semina na warsha mbalimbali za walimu(hapa ndipo wafanyakazi wa idara nyingine wanapotupigia gap) . Nyumba za walimu zitajengwa hivyo kuleta unafuu wa maisha(gharama za pango na nauli za kila siku hazitakuwepo). Mwisho miundombinu ya shule itaimarika hivyo kutengeneza mazingira bora ya ufanyiaji kazi.

Nafikiri hayo yakifanyika kelele za ugumu wa maisha za walimu zitapungua kama sio kuisha kabisa.
 
Back
Top Bottom