Elections 2010 Hali halisi vituoni siku ya kupiga kura

Oooooh.Nyamagana kuna wakala alianza kumpigia masha kampeni live kwa sauti kubwa wakati watu wamepanga msitari,watu wote wakataka kumrudi,bahati yake askari wamemuarest na kumpeleka kituoni.mpaka sasa ccm imebaki haina wakala
 
Toa taarifa zenye maana ili tuelewe unachotaka kutueleza. Tupe na picha au chaanzo cha habari
Mi nimehabarishwa na mdau anaecheki tv mpaka sasa kuwa huko Musoma Chadema wamewatia nguvuni polisi wawili baada ya kuonekana wanapewa rushwa na kiongozi wa ccm, cjajua ni jimbo gani, ila cha muhimu tazama itv au star tv.
 
Wakala wa CCM ataka kumpigia kampeni Masha kwa ujanja ujanja ktk kituo cha Rugumbizi hapa Nyamagana wakati watu wakiwa kwenye foleni.Wananchi wakahamaki,umati ukapiga kelele..askari wakamwarest,bila kujali alikua anampigia debe waziri wa mambo ya ndani(ambaye ndiye bosi wa polisi wote) wakamkamata na kumpeleka kituoni..
Hadi tunakwenda mitamboni kituo hiki kilikua bado hakijapata wakala mwingine wa ccm..OLE WAO!
 
Kuna ndugu yangu yuko sehemu flani siitaji kaniambia kuwa hadi waelekezaji ktk upigaji kura wana hamasa na changes kiasi kwamba akifika mbumbumbu wanamuelekeza kwa kutolea mfano alipo Dr Slaa ktkt picha. Kumbuka mbumbumbu ndio mtaji wa ccm. Kama hata wasimamizi wengi wanataka change basi mambo safi. Ila nikicheki ktk TV naboleka baadhi ya sehemu wapiga kura ni akina mama, na hawa ni ccm, sisi huku mkoa wa mara akina mama tunawafichia kadi zao hadi sa11 jioni
 
Naskia ubungo upigaji kura umesitishwa kutokana na msigano uliopo kati ya mawakala na msimamizi.
 
Ndo namaliza kumwadhibu kiongozi wa mafisadi na timu yake hapa shule ya msingi kizota Dom. Hali kwa ujumla ni shwali na wengi wamepiga kura asubuhi.
 
Mwananyamala kuna fujo, polisi na wanajeshi wanatumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi. Fuatilieni Channel 10.
 
Kuna mgambo ameingia kwenye kituo na sanduku lenye kura za ubunge nyamagana,mdogo wangu yuko hapo nae ni wakala,sasa timbili likaanzia hapo mana police walitaka kulazimisha zile kura ziingie bila kusema zimetoka wapi na nani anazileta? sasa masha anajua hakubaliki analazimisha lakini wananchi wamesimama kidete wakamkamata mgambo na kura zake, nasikia amepigwa sana.

Ndio hivo wakuu.
 
CCM BADO WANAPIGA KAMPENI TABORA!MWANZA VITUO HEWA VINGI WANANCHI WAWAFUKUZA WASIMAMIZI.MWANZA HAWAJAPIGA KURA.source ch10

Kweli halafu nasikia Lawrence Masha kawekwa kwenye kona, kutoka ni chupuchupu ndiyo maana hali iko hivyo
 
Back
Top Bottom