Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 787
Mimi nimetoka kupiga kura pale NIT MABIBO, hali hairidhishi, foleni inakwenda taratibu sana, watu ni wengi, hasa kundi la vijana ambao walikua ni wenye furaha sana. Mpaka saa mbili bado zoezi la kupiga kura lilikua halijaanza katika kituo cha kupigia kura "G"
Pia watu walikua wanahangaika kujua majina yao yalipo, utakuta mtu kapanga foleni akifika karibia na mlangoni anaambiwa jina lako halipo hapa kapange mstari ule pale, hiyo ilikua ni kero kubwa sana kwa watu, kwa maana ilibidi waanze tena upya foleni zao.
Acha upuuzi, vituo vyote vimepewa watu ambao sio zaidi ya 450!!! Wabongo mna matatizo sana... Mumeambiwa usome majina kwenye sehemy ujue umewekwa kwenye kituo kipi? Mimi nimeona kila kitu kilikuwa poa... watu kulalamika kawaida tu Tanzania.