Elections 2010 Hali halisi vituoni siku ya kupiga kura

Jamani mliokwisha piga kura hebu tuelezeni iwapo kuna ukweli wa habari kwamba tiki ya kwa Dr (phD) inaweza kuhamia kwa 'Dr' (wa kuchota). Hii hasa ni katika maeneo ambayo Dr(PhD) ana ufuasi mkubwa kama vile Mbeya, Mwanza, Bklb, Musoma, Arusha, kili, Manyara, Iringa, Rukwa.

Yes-- na hasa iwapo karatasi unaikunja mwenyewe au wasimamizi wanakukunjia? Na kwa utaratibu gani wa kukunja? Je kalamu yao au yako ya kuwekea tiki?
 
mmmmh! hilo sidhani kwani karatasi zote ni sawa tu za mwanza na za Dar... nimejaribu kuichunguza, naona ni jambo lisilowezekana. mi nadhani tuache woga, tupige kura ya mabadiliko!!
 
E BWANA ELI HUKU MAENEO YA MTONIMTONGANI TEMEKE HALI NI SHWARI KABISA HAKUNA FOLENI, NA NINAENDELEA KUHAMASISHA WATU WAKANYONGE NA HUKU KWETU KWENYE FOLENI HAMNA WAZEE KABISA YAAN VIJANA SA HIVI 2NANYONGA:israel:
 
Hata mimi nimejaribu sana kuchunguza hiyo kitu kwa jinsi karatasi ilivyokujwa haiwezekani kuhamia kwa FISADI JK
 
Mi nishamfukuzisha kazi mtu, alitishia ajira yangu nami nimesitisha ajira yake. Niliingia kupokea karatasi za kura huku nikifanya jogging mpaka msimamizi akasema kaka vipi nikamwambia naenda kumtoa mtu knockout pale kwenye Voting Box! Akacheka
 
Hata mimi nimejaribu sana kuchunguza hiyo kitu kwa jinsi karatasi ilivyokujwa haiwezekani kuhamia kwa FISADI JK

Hilo haliwezekani, vinginevyo Maria Roza atawashtaki; kwani kura yake ina ushahidi wa uhakika. Wote tumeona jinsi alivyowajibika.
 
Masha atakoma ubishi,amekuja na kusalimu kiungwana,amepanga foleni km raia wa kawaida mtiifu..ama kweli kiburi cha mende hua kinafika kikomo siku akianguka chali..
 
Am not sure lakini huu upuuzi maana sio lazima ukiikunja iingiliane na wa CCM, mkumbuke kuwa chama cha upinzani sio kimoja, ukipigia CHADEMA position yake itakuwa tofauti na aliyepigia CUF and the like.
 
si kweli...
Kitu cha kwanza kufanya baada ya kuingia kwenye ballot square ilikuwa ni kuchunguza hilo!
Nimeifanyia manjonjo yote karatasi ile, sikuona hali yoyote ya tofauti...nikajaribisha hadi kuinasisha kwa nguvu kwa mwenzie, wapi bana!
Ni uzushi na uvumi...amini kura yako imeenda kwa Slaa!
 
Kituo kina watu wasiozidi 500, hii ina maana ni maeneo ya karibu karibu. Yaani siku tatu watu wameshindwa kujua majina yao yako kituo gani? Huo kama sio uzembe sijui tuite nini?
 
Labda Tatizo la Kiufundi ambalo linaweza ama kula CHADEMA au CCM ni kuwa hawa wagombea wapo karibu karibu sana kwenye hiyo list sasa mtu anaweza kujikuta anaweza tiki kwenye kibox kisichokuwa cha mgombea anaemtaka. CCM iko juu CHADEMA chini yake.

ANGALIZO:Kuna kamtindo hawa wanaotoa hizo karatasi za kura wanapiga ule muhuri wa TUME juu ya Nembo ya CHADEMA sasa mtu anawaeza asiione na hivyo kujikuta anapigia CCM maana hizo Nembo ndo zipo karibu kabisa na kisanduku cha kuwekea alama, sasa Nembo ndio alama rahisi ya kumfanya mpiga kura asipotee mtari wa Mgombea anaemtaka.
 
Nasikiliza Redio One kila sehemu kuanzia lindi vijana wamejaa wakiwa na usongo wa kupiga kura
 
Jamani mbona hamtupi updates za toka huko?? sie wa DAR ndo tumejitahidi kuwahabarisha, jitahidini jamani, tunataka taarifa, kwa DAR naona ni kimya sana, nimepita sinza uzuri, tabata, na sasa nipo mlimani, kumetulia, sasa ndo naingia chumba namba 2 kituo cha UTAWALA- MLIMANI tayari kwa kumpa kura RAIS wa ukweli, nimefurahi pia kusikia wana JF wakikumbushana kuhakikisha wanaandika vyema, hii nimejua kua ni wao kutokana na thread moja waliyokua wanaijadili ambayo ilikua hapa kitaani! VIVA SLAA

Niko Kilimanjaro International Airport (KIA), mambo hapa ni shari kabisa. Kuna kituo kimoja karibu na uwanja ila watu sio wengi sana maana wengi walijiandikisha sehemu wanazoishi. Askari wa uwanja yaani KADCO Security Officers wengi wanalalamika kunyimwa nafasi ya kwenda kupiga kura kwa kisingizio kuwa inabidi wakae kazini japo kuwa wao walitaka kupeana zamu ili waende kupiga kura kwa awamu. Anyway hapa uwanjani leo ni kimya sana, madreva Taxi wako kimya maana wengi wamekwisha kupiga kura, walikuwa na mabishano kidogo yakisiasa ila hivi sasa linaloongelewa ni mpira. Wanakumbushana meche za jana na msimamo wa league za Ulaya. Ni hayo tu mkuu kwa upande huu.
 
mimi kwa huku dar es salaam nimechunguza kwa umakini mkubwa nikajaribu kukwaruza kwa Mheshimiwa D nikaona safi halafu nikaanza kura ya rais nikakunja nikaigongagonga ili ishikamane baadaye nikaikunjua tena na kukuta bado tiki yangu iko kwa mzee wa makazi bora anayechukia nyumba za tembe, kwa hiyo tutoke tupige kura na pia tuchunguze karatasi tunayopewa na tutashinda pamoja
 
Hivi matokeo ndio lini, maana zisinje zikaanza ngonjera hapa, mara oh sijui nini kimekuwa nini, toa matokeo kituoni, tujumlishe wote (si na sisi tunajua hesabu za kujumlisha?
 
Tunashukuru kwa kutupa update ya Iringa. Wanyalukolo pamoja na kubaniwa kumsikiriza Dr. Slaa tunaimani kuwa mtampa kura za Ndio
 
Back
Top Bottom