Hali Halisi-Nina VVU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali Halisi-Nina VVU

Discussion in 'JF Doctor' started by Utingo, Nov 15, 2010.

 1. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ninaogopa....
  Ninajiogopa mimi mwenyewe, ninauogopa ugonjwa nilionao.-
  Kwani itatokea lini, itatokea lini?
  Kifo cha taratibu, au labda cha haraka na bila maumivu?
  Watu...
  Wale wasionionyesha upendo
  Wale wasionipa ulinzi ninaohitaji.
  Tatizo la kifedha...
  Ambapo hakuna msaada unaoweza kuonekana
  Hufanya maumivu kuwa makali zaidi.
  Wote wananitazama na kutikisa vichwa vyao...
  "Hata hivyo unaenda kufa"
  "Hatujui mbele hali itakuwaje"
  "Una bima ya maisha?"
  "Sithubutu kukupenda, Je kama ukifa na kuniacha!"
  "Je ukiniambukiza?"
  Ninataka kujiua...
  Nitafunga kamba kuzunguka shingo yangu
  Nitajirusha
  Nitameza vidonge,
  lakini labda kesho,
  katika makutano ya barabara
  au ndege ya kijeshi kuangukia katika sebule yangu
  Hapana....
  Nimetahadharishwa.
  Tahadhari ambayo watu wachache tu hupata.
  Je inanifanya mimi kuwa wa pekee?
  Kitu cha pekee?
  Inanifanya niogope
  - lakini pia mwenye furaha.
  Imenifundisha kupenda maisha
  Na kuyathamini
  Badala ya kuishi tu.
  Sasa nahitaji kuishi
  Nahitaji kuujua upendo.
  Nahitaji kujua usalama.
  Niamini....
  Nifanye msikivu
  Sikiliza sauti yangu ya ndani.
  Sauti.
  Hufanya ninyenyue kichwa changu juu
  Na kutabasamu juu ya hatima yangu.
  Inanifanya niishi kwa matumaini
  Na kuniambia ni vyema,
  maisha yangu yatakuwa mafupi kuliko ya wengine
  Lakini labda mazuri zaidi?
  Ninatumaini....
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mmmh,ngoja nitafute miwani kwanza duh
   
 3. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,541
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  sijakusoma bado
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  najiandaa siku ya ukimwi duniani
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  . . .
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Pole sana
   
 7. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,541
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180

  unajiandaa kufanyaje
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Nov 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ndg Utingo eleweka basi!
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  kuwa na ukimwi
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Utingo Asante sana kwa shairi lako zuri ingwa ulinistusha kuniambia kama una VVU? unao kweli au ndio mashairi tu?
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  @Utingo

  Umeanza vizuri, katikati ukajichanganya, ila mwisho umeonyesha kejeli kwa ukimwi... OGOPA SANA TU!!!! and dont mess with the disease

  It could have been better, better to introduce the topic, let the poem flow and make and leading statement to discussion and say that najiandaa na ukimwi
  Mgonjwa wa ukimwi aliepewa counselling sahihi haogopi, haombi ndege imuangukie, hajiogopi, hawazi unayowaza, anaishi positively

  Thanks for starting this thread
   
Loading...