Hali halisi: CCM ni sawa na wakoloni ila wao ni weusi

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
1,626
2,000
Wasalaam, naongea ukweli umasikini wetu watanzania umetengenezwa na CCM kwa maslahi ya kakikundi ndani ya jamhuri ya muungano kamajiita CCM. Nasema haya maana tangu Uhuru tumetawaliwa na CCM kwa maslahi ya CCM.

Kwanini nasema tunatawaliwa na CCM? Ni kwa sababu mpaka Leo watanzania hatuna Uhuru kamili maana hata watawala wetu tunachaguli wa kwa nguvu na kundi moja wamajiita CCM.

CCM wamegeza jamhuri ya watanzania kuwa nchi ya kifalme maana anatawala babu hadi mjukuu kwa kauli mbiu za kukatisha tamaa na za ajabu mfano;

1. Mzee Mwinyi: Ruksa

2. Mzee Mkapa: Mtaji wa masikini ni nguvu zake

3. Mzee Kikwete: Maisha bora kwa kila mtanzania

4. Mzee Magufuli; hapa kazi tu.

Hatuna vipaumbele km taifa.

pamoja na kauli mbiu zote hizi bado watanzania tu masikini wa kutupa yaani malofa, maisha ni magumu yote sababu ya ccm, mikataba ya madini na gesi ni siri kubwa haijawahi kujadiliwa bungeni na kuijadili ni uhaini unawezapewa kesi ya utakatishaji pesa ukaozea jela.

Hitimisho; october 2020 ni mwaka wa uchaguzi rai yangu kwa watanzania bila kujali vyama vyetu wala dini zetu wala kabila zetu tukapige kura za hapana kuwapumzisha wakoloni weusi ccm ili tupate Uhuru wa kweli kujitawala na kuchagua watawala kwani Tanzania ni ya wote na itajengwa na sisi watanzania sio kikundi kinachoitwa ccm.
 

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,306
2,000
"Tunataka kuona katika taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini, sio vijana waoga, akina 'ndio bwana mkubwa'. Vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania" MWL. JULIUS K. NYERERE.


Safi kijana ubarikiwe.
 

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,165
2,000
Eed3_WRX0AAMutW.jpeg

Naona baada ya NEC Musiba naye ameshaanza. Ni bandika bandua na kuokoteza tu. Kikubwa tuweke kumbukumbu.
 

Mmeme

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
338
250
Watanzania hawachagui CCM, bali wanachagua sera za CCM. Na wewe uza sera zako, tukiridhika tutakuchagua. Acha kujitia unyonge, nchi hii ni yako pia.

Hatuwezi kuchagua sera ya kupinga kila jambo na kulalamika tu.
Mwaga sera zako tuamue wapiga kura.
 

kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,601
2,000
Nawewe jiunge na ccm ukale mema ya nchi, hutaki kuwa mkoloni?
 

kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,601
2,000
Maisha ni magumu alafu unapata mtu wa kukuseme unatoa maneno ya kereli.
Yaani niache kupambana kwenye mazingira yanayonizunguka mtaani eti nisubiri mtu anisemee mtandaoni. Kalabagao endelea kusubiri usemewe kama maisha yako yatarahisika.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,237
2,000
CCM a.k.a FISIEMU a.k.a Ukoo wa Panya. Siku wakiondojka madarakani hawa Wakoloni Weusi, hakika Nchi yetu itapiga hatua kubwa sana ya maendeleo ya Watu na Vitu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom