Hali halisi ya pato halisi (GDP) la Tanzania

mahunduhamza

Member
Aug 25, 2021
19
46
Katika kipindi cha mwaka 2001-2010 pato halisi la Tanzania(GDP) limeonyesha kiwango cha wastani wa kukua cha 7%. Ukuaji ulishuka mwaka 2009 na kuwa 6.0%, hasa kutokana na kudorora sana kwa ukuaji wa uchumi duniani.

Hata hivyo ulirudia kwenye 7% mwaka 2010. Sekta zilizoonyesha viwango vya ukuaji vya zaidi ya 10% katika mwaka 2010 ni mawasiliano,(22.1%), ikifuatiwa na Ujenzi, Umeme na Gesi (10.2%) na Taasisi za Fedha(10.1%).

Mwaka 2010, Sekta zilizokuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa GDP ni Biashara na Matengenezo, Kilimo, Utengenezaji Bidhaa na Milki/Majengo na Huduma za Biashara.

Zaidi ya hayo, uchumi unategemea zaidi kilimo, ambacho ni zaidi ya robo ya GDP, kinatoa 85% ya mauzo ya nje, na kuajiri kiasi cha 75% ya wafanyakazi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom