Hali bado tete Dar, Watu watishiwa kuwa mabomu mengine yatalipuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali bado tete Dar, Watu watishiwa kuwa mabomu mengine yatalipuka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 3, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,628
  Trophy Points: 280
  Hali bado tete Dar, Watu watishiwa kuwa mabomu mengine yatalipuka.Na Pdidy Wetu

  HALI bado si shwari katika maeneo ilipotokea milipuko ya mabomu, huku miili ya waliopoteza maisha kutokana na tukio hilo ikiendelea kuokotwa sehemu mbalimbali za wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya watu wanaojifanya kuwa ni maafisa usalama na jeshi wanadaiwa kupitika katika nyumba kwa nyumba katika baadhi ya maeneo kuwela za watu kuwa wakati wakati wowote mambomu mengine yaanza kulipuka wakati wowote.

  Taarifa hizo zimeafanya baadhi ya wakazi katika maeneo ya Mbagala, kuishi kwa wasisi na idadi kubwa ya wanawake na watoto wamekwenda kujihifadhi kwa ndugu zao.

  Imeelezwa kuwa hali si shwari katika eneo hilo kwa kuwa mabomu bado hayajatolewa katika kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) 671 KJ kilicho Mbagala, Kizuiani jijini Dar es Salaam ilipotokea milipuko hiyo.

  Taarifa kutoka watu wa wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu zinasema mpaka sasa zaidi ya watu 600 na zaidi ya askari sita wa JWTZ hawajulikani walipo.

  Pia nyumba 700 zikiripotiwa kuharibiwa na milipuko hiyo pamoja na mali zilizo ndani.

  Mpaka kufikia jana miili watu 13 iliripotiwa kuwepo katika hospitali ya manispaa ya Temeke, tisa kati ya hiyo ikiwa ni ya watoto.

  Jana miili ya watu sita ilipokelewa katika hospitali ya manisipaa ya Temeke, minne kati yake ikiibuliwa na wananchi kutoka mto Kizinga.

  Akitoa taarifa za hali ya majeruhi wa tukio hilo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Asha Maita alisema kufikia jana kulikuwa na majeruhi 18 waliokuwa wamebaki hospitalini hapo na mmoja kati yao alipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

  Alifahamisha kuwa kati ya wagonjwa hao, Mtoto Asha Hamisi mwenye umri wa miaka 13, hakuwa na ndugu aliyefika kumwona tangu alipofikishwa hospitalini hapo Jumatano.

  Alitoa wito kwa mtu yeyote anayemfahamu mtoto huyo afike katika hosipitali hiyo.

  Baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na mto Kizinga wameilalamikia serikali kwa kutoweka mkazo katika kutafuta miili ya waathirika wa tukio hilo ambayo ambayo wanadai ipo katika mito hiyo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema, wameopoa miili ya waatoto wawili katika mazingira magumu kutokana na kutokuwa na vifaa vya uokoaji, hivyo kuitaka serikali kupeleka vikosi vya uokoaji katika mto huo kwa ajili kutafuta miili zaidi.

  "Kwenye huu mto bado kuna watu wengi kwa sababu siku ya tukio mto huu ulikuwa na maji mengi kutoka na mvua zilizo kuwa zinaendelea kunyesha, watu wengi na hasa watoto walizama wakati wanakimbia ili kuokoa maisha yao," alisema mmoja wa wananchi aliyekuwa katika Mto Kizinga baada ya kuopoa miili ya watoto wawili.

  Hatia hivyo, hali tete bado inaendela katika maene kadhaa huku baadhi ya yake yakiwa bado yamezungushiwa utepe unaoashiria hali si shwari hivyo watu hawatakiwa kufika huko.

  Mpaka kufikia jana miili ya watu wanne kati ya 13 iliyopokelewa katika hosipitali ya Temeke, imeishachukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alisema serikali itagharamia mazishi ya watu wote waliokufa katika tukio hilo pamoja na kutoa chakula kwa waathirika. Slifahamisha kuwa Jumatatu serikali itatoa Sh1.5 milioni kwa kila mfiwa kama ubani.

  Katika hatua nyingine Mkuu wa Operesheni ya Kuhudumia Wafiwa wa Jeshi la Polisi, Triphoni Rutaihwa, aliwataka wananchi wanaoishi na waathiriwa wa tukio hilo, wapeleke katika kituo chochote cha polisi ili iwe raisi kutambuliwa na ndugu zao.

  Wafiwa wasaidiwa

  KAMATI ya mazishi iliyoundwa mkoani Dar es Salaam kufuatia ajali ya kulipuka kwa mabomu, imetoa Sh1 milioni moja na vyakula kwa kila mfiwa kwa familia nne zilizoathiriwa na tukio hilo kwa ajili ya taratibu za mazishi.

  Akikabidhi misaada hiyo jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Jerome Bwanausi alisema wametembelea maeneo yote ya Mbagala na Temeke kwa ajili ya kutoa misaada kwa wafiwa na kutoka kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya mazishi.

  "Tumetembelea maeneo yote ya Mbagala na Temeke kwa ujumla tumekubaliana na wafiwa kwamba, serikali itagharamia mazishi na kila mfiwa atapewa Sh1 milioni, kilo 100 ya mchele, mafuta box mbili na maji katoni, kumi na leo ndio tunaanza kukabidhi misaada hiyo," alisema Bwanausi jana.

  Kamati hiyo pia itahakikisha kwamba, kwa kila familia ataenda na kiongozi mmoja wa serikali kushiriki katika mazishi ili kuonyesha kuwa wapo pamoja nao katika wakati mgumu.

  Mmoja wa waliokumbwa na msiba ulisabishwa na tukio hilo, Kaniki Masanja aliishukuru serikali kwa msaada huo.

  Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Anderson Charles ambayo ni miongoni mwa maeneo yenye watu wengi walioathiriwa na tukio hilo alisema japo watu kadhaa wametoa msaada kwa waathirika wa milipuko hiyo.

  Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Lukuvi alisema misaada ya chakula inatakiwa ikabidhiwe kwa Meya wa Manispaa ya Temeke na kwamba, vifaa vya ujenzi na mingine ipelekwe katika ofisi za mkuu wa mkoa.

  "Watakaotoa michango yao ya chakula kwa watu waliohathirika walete kwa meya wa manispaa ya Temeke na pia yeye ndie atakaewajibika katika ugawaji na misaada ya vifaa vya ujenzi na vingine viletwe katika ofisi za mkoa," alisema Lukuvi.

  Watu wahama makazi

  Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Kijichi na Mbagala Kuu, wameliambia Mwananchi jana kuwa walilazimika kuzikimbia tena nyumba zao baada ya kurejea kutokana na matangazo ya tahadhari kuwataka waondoke kwa kuwa mabomu mengine yanaweza kulipuka wakati wotote.

  "Tangu jana (juzi) familia yangu na majirani tumekimbia nyumba zetu, hali bado ya wasiwasi, watu wanaojitambulisha ni wana usalama wamepita kututaka tuhame, kwa sababu mabomu yataanza kulipuka tena wakati wowote," alisema Himid Juma mkazi wa Kijichi.

  "Mimi mke na watoto wangu wote wapo kwa dada yangu Msasani na karibu eneo lote hili hakuna mwanamke wala mtoto aliyebaki wote wamekimbia, tumebaki wanaume kwa ubishi na kulinda nyumba zetu ma mambo mengine tunamwachia Mungu," alisema mkazi mmoja wa Mbagala Kuu.

  Katika hatua nyingine zaidi ya wazazi 30 hawajui watoto wao walipo mpaka hivi sasa.

  Akizungumza na Mwananchi katika kituo kidogo cha polisi Mbagala, Meneja wa Mkoa wa Shirika la Msalaba Mwekundu (TRCS) Grace Mawalla alisema wazazi hao bado wanahangaika kuwatafuta watoto wao.

  "Idadi ya wazazi wanaofika hapa kituoni kuwatafuta watoto wao ni zaidi ya 30 hivyo kutufanya tuwe wasiwasi kuwa pengine watoto hao wamefia porini ama kwenye mito ya Kizinga na Mzinga," alisema Mawalla.

  Hata hivyo, jeshi imesema imepata taarifa kuwa kuna watu wanaoeneza uvumi kuwa mabomu mengine yanaweza kulipuka wakati wowote na kwamba linafanya upelelezi ili kuwapata wazushi hao na kuwachukulia hatua kali za kisheria. “Hata sisi tumesikia taarifa hizo na tumeanza kuweka mitego ya kuwanasa watu wanaosambaza habari hizo kwa nia ya kuwasumbua wananchi,” kilisema chanzo hicho.
   
 2. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante Mkuu kwa taarifa.....This is serious man.......
  Swali moja nililonalo ni....Kwa nini misaada kutoka kwa wasamaria k.m. Chakula n.k.... ipelekwe kwenye ofisi ya meya kwanza....?
  Kwa nini wasipewe wahathirika moja kwa moja...?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...