Halbadiri itashusha bei za nyumba Tz?

k_u_l_i

Senior Member
Jan 26, 2010
122
2
Miaka kumi iliyopita nyumba zimepanda bei bila ya kiasi hasa kwenye miji mikubwa kama vile Dar. Ni kweli sababu kubwa ya tatizo la uchumi ninaloendea duniani limeanzia kwenye mijengo kupanda bei mno katika miji mbali mbali duniani . Afadhali kwa sasa miji mingi bei zimepoa kidogo na zinaendea kupungua lakini Bongo imegoma. Kwa kawaida waTz hununua nyumba kwa cash hivyo kuifanya hadithi yetu kuwa tofauti. Hata hivyo kila kinachokwenda juu inabidi kirudi chini. Kwa vyovyote vile bei ya mijengo inabidi ishuke au itulie hapo hapo kwa miaka kadhaa ijayo. Je hii ni ndoto yangu ya mchana au yuko anayefahamu mwelekeo wa hili soko la nyumba bongo?
¬K
 
Nadhani unasahau kuwa nyumba ni mlolongo wa mambo mengi: kiwanja (bei na dalali), ukiritimba wa wizara ya ardhi kusajili, manispaa, ufisadi wa serikali za mitaa, kama ni mkopo riba kubwa. Vifaa vya ujenzi bei juu, mafundi nao bei juu. Muuzaji nae anafidia vyooote hapo na faida kidooogo. Unategemea itashuka?
 
Miaka kumi iliyopita nyumba zimepanda bei bila ya kiasi hasa kwenye miji mikubwa kama vile Dar. Ni kweli sababu kubwa ya tatizo la uchumi ninaloendea duniani limeanzia kwenye mijengo kupanda bei mno katika miji mbali mbali duniani . Afadhali kwa sasa miji mingi bei zimepoa kidogo na zinaendea kupungua lakini Bongo imegoma. Kwa kawaida waTz hununua nyumba kwa cash hivyo kuifanya hadithi yetu kuwa tofauti. Hata hivyo kila kinachokwenda juu inabidi kirudi chini. Kwa vyovyote vile bei ya mijengo inabidi ishuke au itulie hapo hapo kwa miaka kadhaa ijayo. Je hii ni ndoto yangu ya mchana au yuko anayefahamu mwelekeo wa hili soko la nyumba bongo?
¬K
Jenga yako halafu ukaiuze kwa bei rahisi uone joto ya jiwe............. SIWEZI KUGHARIMIA UJENZI KWA 100 MILIONI HALAFU NIKUUZIE CHINI YA HAPO NOOOOOOOOOOO.....................
 
Hili si jibu ya mjadala hapo juu. Hoja imekaa kitaalam zaidi kwa hiyo haihitaji majibu ya ovyo. Kimsingi bei za nyumba zinaendelea kuwa kubwa kutokana na ufinyu wa miundo mbinu. Kila mtu anapenda aishi sehem ambazo huduma za msingi zinapatikana kwa urahisi, km ni biashara basi kuna potential customers ila kubwa zaidi ni serikali yenyewe kuwa na ukiritimba katika ugawaji ardhi na usimamizi wa mpangilio wa mji.
 
Nakubaliana kuwa vifaa na gharama za ujenzi kila leo zinapanda nilichoshidwa kufahamu ni uhusiano wa ongezeko hilo na ungezeko la bei za nyumba hasa katika baadhi ya maeneo. Kwa mfano nyumba Kariakoo ambayo iliuzwa kwa milioni 60 miaka 7 iliyopita hivi sasa ni milioni 600. Kitendawili hapa ni kugundua huu MWELEKEO wa bei za nyumba ndani ya baadhi ya maeneo. Nikiusukuma huo mfano miaka 7 ijayo nyumba hiyo hiyo itauzwa milioni 6,000? Jee hii inaingia akilini?
¬K
 
Mkuu hizo ni dua za kishetani

:) Najua mkuu! I was just pulling the guy's leg...it's just one of those days

Kaandika halbadiri, ni neno la kiarabu, kwa maandishi haya ya kirumi linaandikwa "al-badir"

Halafu kichwa chake cha habari hakiendani na hoja aliyoandika. Ingawa kaandika jambo la maana tu.
 
Ni kweli kichwa cha habari hakiendi sambamba na hoja. Nimefanya hivyo makusudi ku-sensantionalize kuwavutia watu wagonge hiyo link. Inawezekana kimefeli hapo lakini tunajuwa threads gani ni popular ndani ya JF.
¬K
 
Miaka kumi iliyopita nyumba zimepanda bei bila ya kiasi hasa kwenye miji mikubwa kama vile Dar. Ni kweli sababu kubwa ya tatizo la uchumi ninaloendea duniani limeanzia kwenye mijengo kupanda bei mno katika miji mbali mbali duniani . Afadhali kwa sasa miji mingi bei zimepoa kidogo na zinaendea kupungua lakini Bongo imegoma. Kwa kawaida waTz hununua nyumba kwa cash hivyo kuifanya hadithi yetu kuwa tofauti. Hata hivyo kila kinachokwenda juu inabidi kirudi chini. Kwa vyovyote vile bei ya mijengo inabidi ishuke au itulie hapo hapo kwa miaka kadhaa ijayo. Je hii ni ndoto yangu ya mchana au yuko anayefahamu mwelekeo wa hili soko la nyumba bongo?
¬K

Hela za EPA and Co ndio zilipandisha bei za nyumba...iko nyumba iliuzwa kwa $2m Masaki...
 
Hili si jibu ya mjadala hapo juu. Hoja imekaa kitaalam zaidi kwa hiyo haihitaji majibu ya ovyo. Kimsingi bei za nyumba zinaendelea kuwa kubwa kutokana na ufinyu wa miundo mbinu. Kila mtu anapenda aishi sehem ambazo huduma za msingi zinapatikana kwa urahisi, km ni biashara basi kuna potential customers ila kubwa zaidi ni serikali yenyewe kuwa na ukiritimba katika ugawaji ardhi na usimamizi wa mpangilio wa mji.
Hilo nalo neno. Cha msingi hapo ni huduma za kimsingi zinasababisha demand ya nyumba kupanda katika sehem ambazo huduma hizo zinapatikana kuliko sehem ambazo hazipati huduma hizo za msingi kama maji, barabara nzuri, umeme n.k.

HAta hivho kuna sababu za kibiashara- kwa asili Kariakoo ni sehemu kuu ya biashara hivyo bei ya kiwanja inazingatia potentiality ya returns based on the area.
 
Sababu nyingine ni Kwa kuwa hatuna kampuni inayojenga nyumba za kutosha na kuwauzia raia kwa mkopo wa riba nafuu. Tukumbuke kuwa nchi nyingi zilizoendelea watu hawajengi nyumba ila taasisi hujenga kisha kuuza kwa wananchi kwa motgage system ambapo mtu hulipa taratibu hadi anapomaliza deni.

Mfano rahisi ni Botswana ambapo wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa na nyumba zote zimejengwa kwa mipango na hivyo kutokuwa na the so called "uswazi".

Tatizo letu watanzania tunatengenezaga plans nzuri sana ila utekelezaji unakuwa kisiasa zaidi.

Kwa mfano ulisikia mpango wa kujenga 4 ways barabara ya San Nujoma - mwishowe zimejengwa 2 ways tu ... sasa kwa nini hawakusema 2 ways tangu mwanzo.
Tukasikia daraja la kigamboni miaka karibu 10 iliyopita , je hadi leo limeanza kujengwa?

Na sasa wanasema New Dar es salaam kujengwa Kigamboni, sasa subiri uchaguzi upite utaona kimya hadi uchaguzi ukaribie tena ndio watashtua na makatapila ya kuchimba chimba na kupiga nyumba X then uchaguzi ukipita tena inakuwa kimya!

We haya wee , ndio Tanzania yetu zaidi ya uijuavyo!!

Mungu ibariki Afrika , Mungu ibariki Tanzania, asanteni kwa kunisikiliza,,, oooh sorry kwa kunisoma.
 
Back
Top Bottom