Halali waziri kuapishwa uwakili wa kujitegemea wakati ni mtumishi wa umma? Chikawe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halali waziri kuapishwa uwakili wa kujitegemea wakati ni mtumishi wa umma? Chikawe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 7, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe akitunukiwa Uwakili na
  Jaji Mkuu Othman Chande katika hafla ya kuwatunuku
  uwakili wanasheria wa serikali iliyofanyika leo jijini Dar es salaam

  Waziri Mathias Chikawe ameapishwa na jaji Mkuu Chande kuwa wakili wa kujitegemea wakati akiwa mtumishi wa umma kama waziri. Je, kama sheria zinaruhusu hivyo, lakini ni jambo jema kiutendaji? Lini atafanya uwakili wakati anakuwa na majukumu ya kutumikia umma?
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hata mwaka Jana Maalim (Naibu Waziri) Mambo Nje aliapishwa kuwa wakili.hilo suala limejadiliwa kwa kina na kuamriwa jinsi itakavyokuwa ili kuepusha mgongano wa maslahi,iko wazi nadhani wadau wa ndani wa sheria walioko hapa watatusaidia huo waraka wa ufafanuzi!
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni nchi ya kula; hata sheria za nchi na taratibu za serikali zimetungwa kikulakula tu. matokeo ya Azimio la Zanzibar: ambayo watu wake hawaipendi serikali hii ya muungano inayojiendesha kigoigoi tu!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Binafsi naona kunaweza kuwepo mgongano kiwajibikana na kiutendaji. Kama hakuna sheria inayozuia jambo hilo lakini ni busara ya kawaida tu. Hata mbunge tu jambo kama hilo lisingefaa.
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,768
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..nadhani wameapishwa kuwa mawakili wa mahakama kuu, na mahakama ya rufaa ya Tanzania.

  ..labda wanajiandaa kuanzisha shughuli zao binafsi mara watakapoachana na siasa.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwani yule Nimrod Mkono si mbunge yule? Halafu si ni wakili pia....halafu tunaambiwagwa kuwa ni bonge la lawyer...yaani super lawyer (ingawa mimi nasemaga super lawyer my azz....hana u-super lawyer wowote). Kwanza bongo kuna super lawyers? I don't think so.
   
 7. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  Ni sawa na leseni ya udereva.
   
 8. Magu

  Magu Senior Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe kama unataka jua kama mkono ni super lawyer au siyo chukuwa kesi ambayo wewe utakuwa upande mmoja yeye mwingine, ndo utathibitisha kauri yako.

  Suala la uwakili ni mitihani wanafanya na kupewa status hiyo, ambayo kama mjumbe mchangiaji mmoja alivyosema mtu anajiandaa na maisha after public service, mbona Magufuri alipopata PHD katika chemistry hamkuhoji? Au hamna interest nayo au kwa vile ni kipenzi cha wengi?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hana lolote huyo Mkono zaidi ya kutuhumiwa kujihusisha na ufisadi.
   
 10. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Tumtendee haki Mh Chikawe.
  Kujindeleza kitaaluma ni utashi wa mtu, kupata uwakili inabidi usomee tena sheria za uwakili.
  Na hapo unakuwa a proffessional advocate.
  Hilo halimaanishi umekwisha anza kazi ya uadvocate- ina maana UPEO wako wa kuja masuala ya sheria umekuwa mpana.
  Mimi nilukwepo hapo jana wakiapishwa mawakili.
  Na ubunge ukiisha je? Ndio mtu unaanza kutafuta uwakili ili kupractice?
  Hiyo ni kukumbuka shuka tayari kumekucha.
  Nampongeza adv Chikawe na wengine walio pata veti vyao kana.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  mawaziri wanaapishwa, ila watumishi wa serikali wanaambiwa wachague uwakili au Utumishi!
  This kantri kwa double standards!
   
 12. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We jamaa hebu wacha kuturusha hapa; mie bro wangu ni mtumishi wa serikari na ni mwaka jana tu kaapishwa kama Wakili.
  Sasa sijui wamaanisha ni watumishi wa serikali gani au wa ngazi zipi ambazo wanatakiwa kuchagua!!
   
 13. mka

  mka JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Wapo watumishi wa umma kama maofisa wa PCCB, wanasheria wa serikali na wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliopishwa pia.
   
 14. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  chikawe ni mwanasheria tena sio wa jana wala juzi,amesomea sheria miaka mingi iliyopita ,anazijua sheria za nchi.sasa unategemea angekubali kuvunja sheria kirahisirahisi tu kama ingekuwa hairuhusiwi?!uwaziri unapita,ila uwakili haupiti!je akistaafu uwaziri?
   
 15. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  haina tofauti na mganga wa kienyeji? prof maji marefu=ubunge
   
 16. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Mkuu si watu wengi humu JF wanaoweza ku-think critically!
  Michango mingine katika thread hii haina hata iota ya proffessional orientation.
   
 17. m

  mhondo JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wengine wanaapishwa lakini hawapewi practsing certificate inategemea na chombo au Taasisi anayofanyia kazi.
   
Loading...