Halahala Chadema, huenda maziwa yenu mkayatia ndimu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
NILIPOKUWA namsikiliza na kumwangalia Rais Jakaya Kikwete akilihutubia bunge mara baada ya kushika wadhifa huo, Novemba 18, mwaka huu sikutegemea lolote la ajabu lakini ghafla utulivu wangu uliondoshwa na kitendo cha wabunge wa Chadema kutoka ndani ya ukumbi huo wakati hotuba inaanza kusomwa.
Sikuwa na shaka sana na hili la kususia hotuba ya rais kwani inawezekana ni njia mbadala waliyoiteua ili kuwakilisha hisia zao hata kama walikwishaapa kiapo lakini siku zilivyozidi kwenda ndivyo nilivyozidi kujionea mengi ndani ya chama hicho.

Chadema ni chama ambacho kimekuwa na wanachama wanaofanya vizuri bungeni tena bila shaka utendaji wa hao ndiyo uliokifanya chama hicho kikapata nguvu kipindi cha uchaguzi wa mwaka huu.
Nguvu iliyonayo Chadema katika kilinge cha siasa miaka ya hivi karibuni si ndogo na pengine imesaidia kuleta mapinduzi ya aina fulani katika siasa za Tanzania yumkini imefanya mapinduzi hata katika vichwa vya Watanzania wengi.

Nafikiri nitumie methali hii, Mgema Akisifiwa Tembo Hulitia Maji, pengine ni kukosa maamuzi ya busara au kutokupanga mipango yao vyema, Chadema imejikuta ikifuata mkondo usio sawa siku hadi siku.
Tangu wakati huo mpaka sasa yametokea mambo kadha wa kadha ambayo kama si yamewapotezea imani wananchi walioipigia kura Chadema ambao wamekuwa na mitazamo mbalimbali mingi ikiwa ni hasi.

Baada ya Zitto na wenzake kutoingia bungeni siku ya hotuba ya Rais Kikwete, Katibu mkuu wa Chadema (Slaa) alisema waliosusia uamuzi huo wangechukuliwa hatua na kamati ya wabunge ya Chadema, punde si punde zikasikika habari za Zitto kuvuliwa Unaibu Katibu Mkuu .

Hii karibuni mnadhimu wa upinzani bungeni (Chadema)Tundu Lisu alisema wabunge wa chama hicho ambao hawakuonekana katika kikao cha bunge tarehe 18 November watatakiwa kuandika barua ya kujieleza kwa kukiuka mwenendo na utaratibu wa chama hicho walioupanga kwa siku hiyo.
Wabunge ambao hawakuwepo kabisa bungeni wanaadhibiwa kwa kipi, je wangeingia halafu wakagoma kutoka si ndiyo ingeonekana wamewatukanisha kabisa wenzao?

Zitto na wabunge wengine waliosusia kikao nao waliamua kuwsilisha hisia zao kwa namna ile, nauliza tena Chadema ingefanya nini endapo wangekuja halafu wasitoke ukumbini wakati wengine wenzao wanatoka, nadhani huo ungekuwa si utovu wa nidhamu bali yangekuwa matusi ya nguoni.

Ni mara ngapi wabunge wa CCM, CUF, NCCR au Chadema wenyewe wanakosa kuhudhuria vikao vya bunge lakini hawachukuliwi hatua lakini leo wanalazimishwa waandike barua?
Inaonekana mnataka kuvaa viatu walivyovivaa NCCR mwaka 1995pale makundi yalipoendekezwa ndani ya chama hicho na matokeo yake sasa hivi wana wabunge si zaidi ya watano bungeni.

Tafadhali Chadema zingatieni dhambi ya makundi ipo njiani inawangojea, imeacha mdomo wazi na mkizidi kuiendekeza itawameza mkapotea tukawasahau kama wengine waliyosahaulika.
Nalitegemea nguvu mliyoipata ndani ya bunge safari hii itakuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko na vitendo vikuu katika majimbo yenu lakini badala yake nyinyi kwa nyinyi mnaanza kutofautiana na kuleta mpasuko ndani ya chama mapema.

Maajabu mengine yaliyojitokeza hivi juzi tu ni kamati inayoundwa na jopo la wazee wa Chadema kutangaza rasmi kumtambua Rais kikwete, sasa najiuliza kipi kilichowafanya wamkubali mtu waliyemkataa awali? Inaonekana dhahiri wamekosa misimamo.
Chama ni sawa na serikali kwa upande wake, pindi chama kinapokosa muelekeo na kuaza kuvurugana ni dalili tosha kuwa uongozi wake hauko makini.

Likaja kubwa hili hapa, Pale Zitto alipohojiwa na TBC na kusema mengi mazito yaliyo ndani ya chama chake ambayo kwa mtazamo wa wengi ilikuwa ni sawa na kukivua nguo chama chake, kwani wapo watakayoyapuuzia aliyoyasema na wapo watakaoyachukua kama yalivyo.
Zitto alikiri kuwepo kwa udini ndani ya chama, na kitendo chake cha kuiunga mkono ama kuiendeleza hoja hii ambayo ilikuwa ni silaha ya CCM ya kuiua Chadema yaani udini inaonekana kabisa ana ‘mouth diarrhea’ au mropokaji ugonjwa hatari sana kwa mwanasiasa.

Kitendo cha kutoa siri za chama chako katika vyombo vya habari ni usaliti ambao hakika ni sumu kwako na kwa chama chako pia, ingekuwa vyema kama Zitto angekaa kimya kuliko kutamka aliyoyatamka hata kama yana ukweli.
Maneno madogo huweza kumshusha mtu katika kiti cha enzi hadi katika milango ya gereza, kwa mfano vijisenti, mabinti wana viherehere ni baadhi tu ya maneno yaliyowagharimu waliyoyatamka.

Chadema imeanza vizuri na ninaamini ina watendaji wazuri ndani ya bunge na ndani ya chama lakini msipokuwa makini matayatia ndimu maziwa yenu ambayo yalikwishaanza kuwarutubisha ninyi na wananchi waliowachagua.
Zingatieni kuwa mpasuko ni kuwa na fikra tofauti na si vinginevyo hakikisheni kuwa mnaenenda kwa hekima, kwani hekima ni mwisho wa matatizo.

Plato aliwahi kusema kuwa, “wananchi hawawezi kuona mwisho wa matatizo mpaka… wapenda hekima watakaposhika madaraka ya kisiasa au pale wenye madaraka watakapoipenda hekima.”
 
NILIPOKUWA namsikiliza na kumwangalia Rais Jakaya Kikwete akilihutubia bunge mara baada ya kushika wadhifa huo, Novemba 18, mwaka huu sikutegemea lolote la ajabu lakini ghafla utulivu wangu uliondoshwa na kitendo cha wabunge wa Chadema kutoka ndani ya ukumbi huo wakati hotuba inaanza kusomwa.
Sikuwa na shaka sana na hili la kususia hotuba ya rais kwani inawezekana ni njia mbadala waliyoiteua ili kuwakilisha hisia zao hata kama walikwishaapa kiapo lakini siku zilivyozidi kwenda ndivyo nilivyozidi kujionea mengi ndani ya chama hicho.

Chadema ni chama ambacho kimekuwa na wanachama wanaofanya vizuri bungeni tena bila shaka utendaji wa hao ndiyo uliokifanya chama hicho kikapata nguvu kipindi cha uchaguzi wa mwaka huu.
Nguvu iliyonayo Chadema katika kilinge cha siasa miaka ya hivi karibuni si ndogo na pengine imesaidia kuleta mapinduzi ya aina fulani katika siasa za Tanzania yumkini imefanya mapinduzi hata katika vichwa vya Watanzania wengi.

Nafikiri nitumie methali hii, Mgema Akisifiwa Tembo Hulitia Maji, pengine ni kukosa maamuzi ya busara au kutokupanga mipango yao vyema, Chadema imejikuta ikifuata mkondo usio sawa siku hadi siku.
Tangu wakati huo mpaka sasa yametokea mambo kadha wa kadha ambayo kama si yamewapotezea imani wananchi walioipigia kura Chadema ambao wamekuwa na mitazamo mbalimbali mingi ikiwa ni hasi.

Baada ya Zitto na wenzake kutoingia bungeni siku ya hotuba ya Rais Kikwete, Katibu mkuu wa Chadema (Slaa) alisema waliosusia uamuzi huo wangechukuliwa hatua na kamati ya wabunge ya Chadema, punde si punde zikasikika habari za Zitto kuvuliwa Unaibu Katibu Mkuu .

Hii karibuni mnadhimu wa upinzani bungeni (Chadema)Tundu Lisu alisema wabunge wa chama hicho ambao hawakuonekana katika kikao cha bunge tarehe 18 November watatakiwa kuandika barua ya kujieleza kwa kukiuka mwenendo na utaratibu wa chama hicho walioupanga kwa siku hiyo.
Wabunge ambao hawakuwepo kabisa bungeni wanaadhibiwa kwa kipi, je wangeingia halafu wakagoma kutoka si ndiyo ingeonekana wamewatukanisha kabisa wenzao?

Zitto na wabunge wengine waliosusia kikao nao waliamua kuwsilisha hisia zao kwa namna ile, nauliza tena Chadema ingefanya nini endapo wangekuja halafu wasitoke ukumbini wakati wengine wenzao wanatoka, nadhani huo ungekuwa si utovu wa nidhamu bali yangekuwa matusi ya nguoni.

Ni mara ngapi wabunge wa CCM, CUF, NCCR au Chadema wenyewe wanakosa kuhudhuria vikao vya bunge lakini hawachukuliwi hatua lakini leo wanalazimishwa waandike barua?
Inaonekana mnataka kuvaa viatu walivyovivaa NCCR mwaka 1995pale makundi yalipoendekezwa ndani ya chama hicho na matokeo yake sasa hivi wana wabunge si zaidi ya watano bungeni.

Tafadhali Chadema zingatieni dhambi ya makundi ipo njiani inawangojea, imeacha mdomo wazi na mkizidi kuiendekeza itawameza mkapotea tukawasahau kama wengine waliyosahaulika.
Nalitegemea nguvu mliyoipata ndani ya bunge safari hii itakuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko na vitendo vikuu katika majimbo yenu lakini badala yake nyinyi kwa nyinyi mnaanza kutofautiana na kuleta mpasuko ndani ya chama mapema.

Maajabu mengine yaliyojitokeza hivi juzi tu ni kamati inayoundwa na jopo la wazee wa Chadema kutangaza rasmi kumtambua Rais kikwete, sasa najiuliza kipi kilichowafanya wamkubali mtu waliyemkataa awali? Inaonekana dhahiri wamekosa misimamo.
Chama ni sawa na serikali kwa upande wake, pindi chama kinapokosa muelekeo na kuaza kuvurugana ni dalili tosha kuwa uongozi wake hauko makini.

Likaja kubwa hili hapa, Pale Zitto alipohojiwa na TBC na kusema mengi mazito yaliyo ndani ya chama chake ambayo kwa mtazamo wa wengi ilikuwa ni sawa na kukivua nguo chama chake, kwani wapo watakayoyapuuzia aliyoyasema na wapo watakaoyachukua kama yalivyo.
Zitto alikiri kuwepo kwa udini ndani ya chama, na kitendo chake cha kuiunga mkono ama kuiendeleza hoja hii ambayo ilikuwa ni silaha ya CCM ya kuiua Chadema yaani udini inaonekana kabisa ana ‘mouth diarrhea' au mropokaji ugonjwa hatari sana kwa mwanasiasa.

Kitendo cha kutoa siri za chama chako katika vyombo vya habari ni usaliti ambao hakika ni sumu kwako na kwa chama chako pia, ingekuwa vyema kama Zitto angekaa kimya kuliko kutamka aliyoyatamka hata kama yana ukweli.
Maneno madogo huweza kumshusha mtu katika kiti cha enzi hadi katika milango ya gereza, kwa mfano vijisenti, mabinti wana viherehere ni baadhi tu ya maneno yaliyowagharimu waliyoyatamka.

Chadema imeanza vizuri na ninaamini ina watendaji wazuri ndani ya bunge na ndani ya chama lakini msipokuwa makini matayatia ndimu maziwa yenu ambayo yalikwishaanza kuwarutubisha ninyi na wananchi waliowachagua.
Zingatieni kuwa mpasuko ni kuwa na fikra tofauti na si vinginevyo hakikisheni kuwa mnaenenda kwa hekima, kwani hekima ni mwisho wa matatizo.

Plato aliwahi kusema kuwa, "wananchi hawawezi kuona mwisho wa matatizo mpaka… wapenda hekima watakaposhika madaraka ya kisiasa au pale wenye madaraka watakapoipenda hekima."

Pole mkuu huo ndio mchakato wa siasa, hakuna script hapo, ulitakalo haliwi na unalolitarajia sio na utakaloliona ndilo hasa SIASA
 
Marehem Chacha Wangwe alisema chadema kimejaa ukabila, na sasa Zito anadai kimejaa udini. wahenga wanasema lisemwalo lipo.
 
Back
Top Bottom