Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Niliwahi kumsikia Goodluck Ole Medeye akiomba kura bungeni, miaka michache iliyopita. Yupo vizuri kwa maana ya elimu na upeo, huwa hapendi kuongea pumba.
Kitendo cha kuamua kuhamia UDP huku akieleza sababu ni kutopendezewa na jinsi wabunge wa upinzani wanavyokuwa na uhusiano mbaya kikazi na Naibu Spika, kinajenga uhalali wa uamuzi wa serikali kutoonyesha live shughuli za bunge.
Ikiwa wanaopigia debe kwa uwezo wao wote ili bunge lioneshwe live, ndio hawa hawa ambao mbunge wa zamani Ole Medeye anawaona kama wanapotea njia, nadhani ni sahihi kabisa kwa marudio ya bunge kuonyeshwa usiku.
Treatment mbovu anayopewa Dr Tulia ingeweza kumkumba Ole Medeye pia. Ukorofi wa baadhi ya wabunge kiasi cha kusahau wapo katika jengo lenye hadhi kubwa kiasi gani kwa taifa hili, usingeshindwa kumkwaza Ole Medeye.
CDM na upinzani wanahitaji sana kufanya mabadiliko ya mienendo yao ili waweze kuipata tena ile huruma ya jamii.
Walililia bunge lionyeshwe live, lakini cha ajabu ni kwamba mtu yule yule waliyempigia makofi wakati akiomba kura ili awe spika, ndiye anayekerwa na mienendo yao.
Bunge ni chombo chenye hadhi kubwa sana, na sio eti kwa sababu kwenye mabunge kama lile la Ukraine kuna wabunge wendawazimu basi eti na sisi tuige upuuzi.
Maadili ya wanasiasa wetu ni jambo ambalo linapaswa kuwa kielelezo cha ustaarabu wetu. Na sio wanasiasa wa leo tu hata wale wenye nia ya kuja kuwa wawakilishi wa wananchi, wajifunze kuishi kwa kuheshimu maadili.