Hakutawahi kutokea Tanzania Rais kama Mzee Kikwete

Mjanja mjanja tu. Asingekuwa raisi bila figisu, raisi angekuwa salimu au mwandosya.
Kanacheka huku kanakufyeka. Aliharibu mchakato wa katiba na kura za maoni za uraisi za ccm 2015.
Wezi alikuwa anahamisha badala ya kufukuza. Alifuga mafisadi haijawahi tokea TZ .
RIP magu ulimfunika Jk kwa miaka mitano tu na kuonyesha ombwe la kiutala.
Sikuwahi sikia ma ajali ya hovyo kipindi cha Jiwe wala albino
kuuwawa.

JPM alifukuza wezi wangapi?
 
Alitupiga kwenye dowans
ALITUPIGA SANA ALIPOWAKABIDHI BANDARI YETU WASHIHIRI WA HOME SHOPPING CENTRE!! WALIKUWA WANAINGIZA MAKONTENA BILA KULIPA KODI NA MKWERE ALIKUWA ANACHUKUA MSHIKO WAKE KWAO!!!
 
Mimi nasema kila siku kama Jakaya nae angeamua kuishi kama JPM angekuwa raisi ambae tusingetamani atoke madarakani

Namaanisha angebana uhuru wa habari, kuwaminya wapinzani kuzuia bunge kuruka mbashara

Leo hakuna mtu angejua ufisadi wa Escrow, Richimond, IPTL nk maana uwazi pia usingekuwepo, kupindi cha Jakaya watu walipiga sawa ila kulikuwa na uwazi wakipiga leo kesho raia tunajua

Ila kwa huyu alietangulia mbele za haki watu wamepiga kweli kweli ila hakuna uwazi unadhani wananchi hawa masikini wa kila kitu (wanyonge) na hii elimu bure kabisa kichwani mwao wangejuaje zaidi ya kuimba mapambio

Kwa Jakaya miaka kumi yake hela walizopiga hazifikiiii hizi za JPM kwenye hii miaka yake mitano
Kwa hiyo kujua ufisadi wa escrow na richmond kumetusaidia nini? Yaani rais mwizi kama wizi wa escrow ni rais bora kuliko aliyethubutu kujenga Nyerere HP, kupanua viwanja vya ndege, kujenga hospital kwa wingi nk.

Sijaielewa akili yangu.
 
Mr.President ......naunga mkono hoja hata kimuonekano unasema yes huyu ni president na sio
... ....Mjanja ni Mjanja tu miaka mia.....!!
 
Kwa hiyo kujua ufisadi wa escrow na richmond kumetusaidia nini? Yaani rais mwizi kama wizi wa escrow ni rais bora kuliko aliyethubutu kujenga Nyerere HP, kupanua viwanja vya ndege, kujenga hospital kwa wingi nk.

Sijaielewa akili yangu.
Hiyo JKHP imekamilika, hivyo viwanja wa denge wewe maskini (mnyonge) vinakuhusu na hizo hospitali zina wahudumu na madawa? kiukweli hata mimi nashindwa kuielewa akili yako

Kwamba Jakaya hakufanya vya maana barabara za rami kuunganisha mikoa yote alijenga baba ako?, watoto wako hao wakimasikini bila Jakaya kujenga shule za kata leo wangesomaje hiyo elimu bure kabisa ya JPM?
 
62170fd5-63a5-4293-a4b5-91eacaa78acb.jpg
 
JK - Julius Kambarage
JK - Jakaya Kikwette

Wote hao walikuwa maridadi kabisa. Hawa ndiyo wazee wa legacy.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Mkuu katika utawala wa Nyerere ulikuwa na umri gani? Au unaongea kisiasa?
 
Maana yake nini?! Kwamba kutawahi kutokea kama Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Magufuli lakini siyo kikwete?!
Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli wote ni walewale!
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom