Hakutawahi kutokea Tanzania Rais kama Mzee Kikwete

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,691
2,000
Yeereeeeeh!

Kamwe katika historia ya Tanzania hakutawahi kutokea Rais kama JK. Alikuwa mtu wa watu mpole wakati wote. Vijana wa TISS na UVCCM walikuwa wanamrukia hadi mabegani. Ndie rais wa kwanza Tanzania kuvaa jeans na Tshet hadharani. Hatutawahi kumpata kama JK.

pix.jpg
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,249
2,000
Yeereeeeeh!

Kamwe katika historia ya Tanzania hakutawahi kutokea Rais kama JK. Alikuwa mtu wa watu mpole wakati wote. Vijana wa TISS na UVCCM walikuwa wanamrukia hadi mabegani. Ndie rais wa kwanza Tanzania kuvaa jeans na Tshet hadharani. Hatutawahi kumpata kama JK. View attachment 1758622

JK - Julius Kambarage
JK - Jakaya Kikwette

Wote hao walikuwa maridadi kabisa. Hawa ndiyo wazee wa legacy.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

Ngosha Mashine

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
430
1,000
Mimi nasema kila siku kama Jakaya nae angeamua kuishi kama JPM angekuwa raisi ambae tusingetamani atoke madarakani

Namaanisha angebana uhuru wa habari, kuwaminya wapinzani kuzuia bunge kuruka mbashara, hapa tungeona mazuri tu hakuna kujua mabaya

Leo hakuna mtu angejua ufisadi wa Escrow, Richimond, IPTL nk maana uwazi pia usingekuwepo, kupindi cha Jakaya watu walipiga sawa ila kulikuwa na uwazi wakipiga leo kesho raia tunajua

Ila kwa huyu alietangulia mbele za haki watu wamepiga kweli kweli ila hakuna uwazi unadhani wananchi hawa masikini wa kila kitu (wanyonge) na hii elimu bure kabisa kichwani mwao wangejuaje zaidi ya kuimba mapambio

Kwa Jakaya miaka kumi yake hela walizopiga hazifikiiii hizi za JPM kwenye hii miaka yake mitano

Kuna watu wapo kubeza vya JK ila kutwa kutetea kitu kinaitwa REGACY ya hayati isipotezwe, ndg zangu REGACY inajitetea

Mwendazake mwenyewe mda wake madarakani alikuwa kutwa kubeza vya watangulizi wake "ndg zangu tumeliwa mno, tumelaliwa mno" ila misukule yake haitaki yeye aongelewe against

Inajitoa fahamu eti elimu bure wakati robo tatu ya hao walimu wachache muajili ni Jakaya, 🤔 tumejenga mahospital kila kona ya Tanzania haya sasa hao wahudumu kwenye hizo hospital robo tatu yao wameajiliwa kwa Jakaya JPM hakuwa ameweka hata dawa za kutosha kutwa porojo tu misukule inashangilia "tumeongeza bajeti" ila ukienda hospitali unapimwa tu then dawa ukanunue mwenyewe duka binafsi

Ilaaa hiiiiiiiiiiiiiii kazi ipo haki ya Mungu
 

road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
1,036
2,000
Huyu jamaa amekulia Royal family nafikiri baba yake alikua DC those days hivyo hakuwa na ushamba wala ulimbukeni.
Tizama hata Uhuru Kenyatta alikulia Royal Family angalia alivyo na tabia za kigentlemen hana ushamba wala ulimbukeni.
Angalia JKN babake alikua chief hivyo pia ni Royal family by then Mwangalie alivyokua Jentomeni
The same to Mkapa !!!!
 

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
11,576
2,000
Huyu jamaa amekulia Royal family nafikiri baba yake alikua DC those days hivyo hakuwa na ushamba wala ulimbukeni.
Tizama hata Uhuru Kenyatta alikulia Royal Family angalia alivyo na tabia za kigentlemen hana ushamba wala ulimbukeni.
Angalia JKN babake alikua chief hivyo pia ni Royal family by then Mwangalie alivyokua Jentomeni
The same to Mkapa !!!!
kuna li mtu limekulia mashambani huko GAMBOSHI lichunga ng'ombe ngoja nitarudi.
 

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
1,664
2,000
Yupo na ameshapatikana. Ila aliyepatikana anatatizwa na legacy tu. Ashike kamba yake, anaweza. Ni muda tu utasema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom