Hakuna watu wavumilivu kama waajiriwa walio chini ya TAMISEMI

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,684
36,045
Habari ndugu zangu!

Kila nikitazama television nagundua jambo jipya.

Wafanyakazi walio chini ya TAMISEMI wana mabosi wengi sana, na kila boss anataka kuonyesha nguvu yake.

Punching bag la ma RC, RAS, DC, DED, DAS, na kadhalika na kadhalika ni watumishi walioko huko serikali za mitaa.

Wanadhalilishwa kila siku, no extra duty allowance, no lunch allowance, no fare allowance, no house allowance but wanavumilia dhihaka wanazofanyiwa.

Duuuhh aiseee mna kiwango kikubwa cha uvumilivu.

Samahani Kama nimemkwaza mtu.

Tujenge taifa kwa moyo na uvumilivu.
 
Sio watumishi wote wanaokubali upuuzi huo wa kudhalilishwa, hao wanasiasa hukutana na vichwa sema media huwa zinawasitiri.

Mzee Agrey Mwandri akiwa RC kuna siku alikanya waya akiwa ziara zake za kikazi, aliambiwa; "Usinitishe, Usinitishe, Usinitishe". Akawa mpole tu siku hiyo.
 
Sio watumishi wote wanaokubali upuuzi huo wa kudhalilishwa, hao wanasiasa hukutana na vichwa sema media huwa zinawasitiri.

Mzee Agrey Mwandri akiwa RC kuna siku alikanya waya akiwa ziara zake za kikazi, aliambiwa; "Usinitishe, Usinitishe, Usinitishe". Akawa mpole tu siku hiyo.
Hajatumia yale masaa 48 aliyopewa na ikulu?
 
Acha tu..hii nchi hii imekua ya mambo ya ajabu sana..huko local govt ni stress tupu kila siku hasa ukiwa mkuu wa kitengo au idara huwezi lala ukatulia...kila kibosi kinakuja na maelekezo yake na kinataka utekerezaji wa haraka..ila ukiangalia hakuna hata fedha au vitu vya kutekereza hiyo projecka kwa uharaka..urasimu mingi sana.

#MaendeleoHayanaChama.
 
Kwakweli ni balaaa kwenye huo Msuruu hujawataja Viongozi wa Ngazi ya VYAMA VYA SIASA WILAYA NA MKOA, Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi Mkoa na Wilaya, Wakuuu wa Taaasisi za Umma Mkoa na Wilaya, Bado Wakuu wa Seksheni na Idara kwakweli ni msururuuuuu wa hatari.
Mtu mmoja anakuwa na mabosi hata kumi
 
Wanasiasa watu wa hovyo sana washazoea kuropoka majukwaani ,sasa wamehamishia msongo wao wa mawazo kwa watendaji wetu huko maofisini.

Msifanye makosa Oktoba tumieni kura yenu vizuri msije lia lia tena humu.
 
Back
Top Bottom