Hakuna wakati mbaya kwa CCM kugawanyika kama sasa, wazee wa chama wamekosa maono ya kukinusuru chama?

Kuna mambo makuu matatu ambayo CCM wakiyapuuza hakika watatawanyika kama ndege wa angani uwarushiapo jiwe.
1. Kesi ya Sabaya na Makonda.
katika kesi hizi wengi wanaona ni kesi za kawaida lakini kiuhalisia ni kesi za kimfumo. Ni kesi ambazo top layer ya awamu ya tano, maafisa wandamizi wa jeshi la polisi pamoja pamoja na maofisa wa juu wa idara ya ujasusi hawatasalimika. Hivyo uwepo wa kesi hizi ni sawa na kutaka kujisambaratisha wanaccm wenyewe ambao kwao haki siyo kipaumbele.

2.Kesi ya Mbowe.
kesi hii imeleta mvurugano mkubwa na taswira mbaya sana kwa taifa letu. Katika hali isiyo ya kawaida makosa waliyoamua kumuwekea na kumtuhumu nayo Mbowe ni makosa makubwa mno kiasi cha wao kukosa namna ya kuyatetea. Kuendelea kuwepo kwa kesi hii kutawagawa sana ccm na kuwatawanya kama hayawani.
3. mfumuko wa bei, suala la bwawa la umeme Rufiji na matatizo ya kukatika kwa umeme.
kila mmoja atakubali matatizo haya yamepigwa chapuo na awamu ya sita hivyo ni kansa kwao..
4. Ongezeko la wahuni tangu kuja na kutoweka kwa Magufuli
 
Wazee wenu wa chama ndiyo hao kina mzee mwinyi waliokua wanasema hadharani kuwa katiba ibadilishwe Pombe awe rais kwa miaka 100??
 
Back
Top Bottom