Hakuna wa kumtetea Assad, si serikalini si upinzani...

Watanzania walio wengi ni VICHWA VYA WENDAWAZIMU hawa ni wale wa Lumumba wakata mauno huku wakiimba ccm nambari one huku nchi ikiendelea kukosa maendeleo kwa miaka 57 sasa.

Magufuli anachota Fedha za umma na kuzitapanya bila utaratibu wala kufuata kanuni na bajeti ya serikali na bunge wala halihoji CAG akisema bunge dhaifu watu wanatokwa na mapovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe na mimi hata tupayuke vipi hapa JF nani wa kutusikiliza?

Nategemea kuna wabunge wachache wajitokeze na kuwa wa kweli wa nafsi zao na kupaza sauti ya wananchi.

Bunge ni dhaifu.
Dada Faiza, In Shaa Allah uu bukheir uu Afya. Tupo wengi tunaounga mkono kuwa kiti cha CAG kisiingiliwe. Uhuru wake uachwe kama katiba inavyosema.

Wengi wetuhapa JF bado hatujatambua ni nani wanasiasa waupinzani walio true Nationalist na ni akina nani ni populist Opposition leaders.

Mpaka dakika hii tunamuona ni Zitto pekee, anayezindua hoja muhimu, hiki la CAG tumemsikia Halima na Bi Karume ambaye naye anatumia nafasi yake pasivyo.

In Tanzania it is easy the public to be united against injustice, but the Opposition political leaders will never be honest to each other or on any issues.

Sister thank you for your great contributions

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halima Mdee naye kaitwa kwenye kamati maana naye alimuunga mkono CAG mara tu baada ya tamko lake..hivyo ni moja kwa moja wapinzani inaonekana wanamuunga mkono CAG..

CAG lakini sio wa kwanza hata LISSU aliwahi kutamka hili na kwenda mbali kufikia kuliita bunge ni rubber stamp ya ikulu, ZZK alishaitwa kamatini juu suala hili hili, PASCAL MAYALA mwana JF mwenzetu alishawahi kuitwa bungeni juu ya suala hili hili..

Nafikiri inatakiwa hukumu kutoka kwa wananchi dhidi ya bunge hili lenye wabunge wengi wa CCM..
Wako wapi, akina Lema, Mnyika, Sugu, Msigwa, Lowasa, Sumaye na wale wababe waliokuwa na PHD za kumtukana Mkwere

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo hii ilitakiwa upinzani wote uwe umeshatoa kauli za kumuunga mkono Assad na kusema wazi wazi kuwa bunge ni dhaifu, hususan wabunge wa upinzani kama kweli wapo pale kusimamia maslahi ya Tanzania.

Hali kadhalika wabunge wa chama tawala, kama kweli wapo pale kutetea wananchi waliowachagua, wawe wa kweli kuwa fedha zetu hazisimamiwi na bunge ipasavyo na kuna udhaifu mkubwa bungeni kwenye hilo. Na hilo linatokana uendeshaji bunge dhaifu wa Ndugai.

Bunge ni dhaifu.
Si kwamba hawajui au hawataki, wanaogopa ya mwenzao Lissu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Assad ni mtu pekee Tanzania hii ambae yupo serikalini lakini anaweza kuikosoa mihimili yote mitatu ya mfumo wa uongozi wa Tanzania.

Anaweza kuukosoa mhimili wa taasisi ya Urais kwa maana ya wizara na idara zote zilizo chini ya taasisi ya Urais. Anaweza kuukosoa mhimili wa bunge ikiwemo ofisi ya spika. Anaweza kuukosoa mhimili wa mahakama. Anaweza kuikosoa mihili yote hiyo kwa kutokusimamia matumizi mazuri, ubadhirifu, uvunjaji wa sheria na kanuni za matumizi na ndiye pekee anaweza kutoa maoni yake ya udhaifu uko wap na akasikika.

Assad majukumu yake hayaishii serikalini tu, ni mtu pekee anaeweza kuyafanya yote hayo juu kwa upinzani pia.

Kwa kutazama hayo kwa uoana wake, Assad ni mtu pekee anaeweza kuikosoa (kwenye usimamizi wa fedha) Jamhuru nzima ya Muungano wa Tanzania.

Hilo ni jukumu kubwa sana na lazima awe na maadui kutoka kila pembe.

Hakuna asiyeelewa kuwa Tanzania matumizi mabovu ni kila pahala.

Ni dhahiri hakuna mhimili usio mchekea usoni tu lakini akigeuka anasonywa.

Kwa hiyo tusitarajie mhimili wowote kumtetea Assad zaidi ya wachache wanaotaka kuona matumizi ya fedha zao yanasimamiwa vizuri.

Hili sakata la Assad ndiyo litatuonesha ukweli wa mambo ulivyo Tanzania.

Hakuna ataepinga kuwa kuna madudu mengi ya kifedha yapo serikalini na inawezekana kabisa kuwa madudu hayo yapo hata ofisi ya spika. Spika ameshindwa kabisa kuliendesha bunge kuwa wasimamizi wa serikali na kwa maana hiyo basi bunge limekuwa dhaifu.

Tutegemee nani wa kuwa upande wa Assad?

Bunge ni dhaifu.
Islam ndugu yake Islam Mama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la faizafoxy ni mdini ameguswa wa imani yake ndo anajifanya kusimama kidete, ingekuwa huyu CAG ni wa dini nyingine wala hata asingehaika, kinachomsumbua ni udini hakuna lingine. Maana hizi kauli zimeongelewa sana ndani na nje ya bunge na baadhi ya viongozi wa upinzani pamoja na mwandishi wa habari wa kujitegemea na akaitwa kuhojiwa mbele ya kamati ya maadili ya bunge lakini mleta mada alikuwa kimya.
 
Hakuna uchonganishi nje.

Assad siyo mwanasiasa. Assad ni professional anaejisemea ukweli wake.

Kwa sakata hili, hakuna "next time".

Asikubali kabisa kupelekeshwa na asimamie profession yake. Hana cha kukikosa.
Mkuu Assad amekosea sana tu yeye kama CAG alikuwa na uwezo wakuonana na Spika na kumweleza concern zake siyo kutoka TZ na kwenda huko kwa Mabeberu na kuliponda Bunge la nchi yako huo ni utoto wa hali ya juu lazima tuwe waungwana. Hata nyumbani kwako kama kuna tatizo la ndani huwezi kwenda kwa jirani na kuanika uozo wenu nje! Kwa waliolelewa huwezi fanya hivyo. Hata makazini huwezi toka ofisini kwako na kwenda nje ya ofisi yenu nakumwambia mpinzani wenu matatizo ya management ya ofisini kwenye
Management ikijua lazima ikushughulikie kinidhamu. Hivyo CAG amefanya kosa kwa mujibu wa Katiba ibara ya 144(2) kwa kuonyesha tabia mbaya na hiyo inamkositi. Mtapiga kelele weee lakini hilo analo na yeye analijua!
 
Kwani Assad haonani na speaker? Reports zake anamkabidhi nani bungeni?

Unajuwa Assad alikuwa anafanya nini UN?

Awenalo asiwe nalo, ni sababu anatafutuwa. Huo ndiyo mwiba uliobakia. Nani wa kumtetea? Wewe? Hahahahahaha.
 
Huyu ndiye mtaalam kweli kweli sio wale ambao wanafanya ujinga wakiulizwa wanasingizia wanasiasa wanawaingilia, haingiliwi mtu if assad is our CAG, long live our son of Africa.

Back
Top Bottom