chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 19,682
- 22,685
Kumetokea wimbi la viongozi hasa wanaowinda vyeo serikalini kujinasibu na kutaka kuwaaminisha Watanzania kwamba wapo tayari kufuata nyayo za mwendazake. Kiukweli bila chembe ya unafiki hizo ni hadaa kama zilivyokuwa hadaa za mwendazake.
Tukubali kila nyakati zina mambo yake, nasema hivyo kwani hata hasara kubwa ya shilingi bilioni 60 iliyoonekana katika shirika letu la ndege wakati wa utawala wa Hayati Magufuli hakuna ambaye angethubutu kuweka wazi.
Ninaamini hata Mh Rais S.S. Hassan hafuati nyayo za mtangulizi wake bali anatengeneza Legacy yake mwenyewe na akimaliza muda wake basi atahukumiwa kwa aliyoyafanya na wala siyo yale ya mtangulizi wake.
Muda ni Jibu.