Hakuna utamaduni wa nchi, kuna utamaduni wa makundi /jamii za watu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,346
45,698
Jana waziri Nape alizungumzia suala la TEHEMA na utamaduni wetu. Bila shaka alikuwa anazungumzia utamaduni wa nchi. Haya ni maneno ambayo huwa yanasikika sana kutoka kwa viongozi wa siasa na dini na hata watu wa kawaida mara kwa mara.

Sidhani ni sahihi kuzungumzia suala la utamaduni katika muktadha wa nchi kwa sababu huwezi kupata utamaduni wa nchi popote duniani. Utamaduni unapatikana zaidi katika kabila au dini, sio katika ngazi ya taifa.

Baadhi ya makabila ni lazima mwanaume kutahiriwa ila makabila mengine hawatahiriwi, baadhi ni mwiko mwanamke kuongoza ila makabila mengine anaweza kuongoza, baadhi kama Wamasai wana mavazi yao rasmi, dini zinatofautiana katika mambo mengi kama idadi ya wanawake kuoa n.k haya na mengine mengi ndio utamaduni.

Mataifa mengi kama sio yote hasa ya Africa ukiyatazama yanakusanya jamii nyingi za watu wenye tamaduni tofauti sana pamoja.

Katika uhalisia kama huu, Je tunaweza kuwa na utamaduni mmoja wa Taifa? Sioni uwezakano huo.
 
Back
Top Bottom