Hakuna urafiki wa mke na mwanaume nasitataka kuaminishwa na yeyote

markbusega

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
826
847
Zamani niliamini jambo hili linawezekana. Lakini kupitia uzoefu wangu nimeona jambo hili haiwezekani. Nitashare nanyi uzoefu wangu.

Nimewahi kufahamiana na wadada kadhaa katika pilikapilika zangu za maisha aidha kupitia huduma anayotoa au kama mteja kwangu lakini mwisho wa siku wenzangu wamekuwa na idea ya kuishia kuwa wapenzi kinyume na malengo yetu

Nianze na huyu dada ni mwite d, baada ya yeye kunihudumia mara kwa mara basi tukawa tunawasiliana kawaida tu kibiashara mfano kutaka ufafanuzi wa jambo fulani kama nimekwama.

Nakumbuka ilikuwa siku ya mwaka mpya 2013 nikaamua kuandika meseji ya kawaida ya kuwatakia heri ya mwaka mpya watu wote waliokwenye simu yangu, huyu d alipoipokea alifurahi naye alijibu vizuri tu tena kwa furaha. Iipopita siku 1, majirani yule dada alianza kuhoji kwa nini niliamua kumtumia ile sms, nilijitetea kwamba ilikuwa sikukuu kwa hiyo nikaona si vibaya watu wanaofahamiana kutakiana heri ya mwaka mpya lilikuwa ni hilo nilimalizia. Kilichofuata nilitukanwa mpaka basi sikujibu mpaka basi mpaka sasa sijui nilikosea wapi?

Wapili alikuwa ni mteja wangu alinipenda tu. Na mpaka sasa sijui huyu dada alinipendea nn ghafla hivyo, huyu alikuwa mteja wangu wa viatu mara nyingi alipenda kununua viatu kwangu tukawa tumezoeana. Akanikaribisha kwake kumbe alikuwa mwalimu na hajaolewa alikuwa anamalizia masters yake, nilivutiwa na mazungumzo yake siku hiyo tukajikuta tumefika saa 9 usiku tangu saa 2, yule dada ana akili balaa za darasani na za maisha

Siku hiyo aliniaga anaondoka kwenda kuanza kazi kama mhadhili msaidizi, katika moja ya vyuo hapa Tz. Nilihuzunika sana Maana alikuwa ameshakuwa rafiki yangu.

Mungu si matoborwa baada ya wiki matokeo ya usaili yalitoka nimefaulu na kupangiwa kazi karibu na wilaya alipo. Hunisisitiza sana nimtembelee kwake, Kutokana na uzoefu nilioupitia nimekuwa mzito juu ya hili ukizingatia ameanza kuonesha element za mapenzi wazi na mimi siko tayari ukizingatia nina mchumba wangu

Mimi huwa si rahisi kumzoea dada maana huwa si mtu wa maneno mengi. Tutaongea kiofisiofisi basi ukiongezea na uzoefu wa kutukanwa na yule dada ndo kabisaa ofisini wadada wameanza kuniita mgumu,

nipeni mbinu wadau mmewezaje kumaintain urafiki wa jinsia tofauti? Bila kuishia kufikia mapenzi. Ili tusifike huko na mwalimu anamadini hatar Sitaki tugombane hadi mwenyewe atakapoona inatosha for good. Nawasilisha
 
ni kweli kaka hakuna urafiki wowote kati ya jinsia hizi mbili ambao hauwezi kuishia kwenye ngono,ni ujinga kuamin simba na swala waweza kukaa kirafiki,siku njaa ikimshika atamla tu
 
Unachokiamini wewe sio kila mtu anakiamini, na ulichokishindwa wewe wengine wanakiweza ni kujifunza tu hakuna linaloshindikana.
kama mtu wako ana mtu wa jinsia tofauti pembeni kisha anakuambia eti ni rafiki tu stuka mama utaibiwa,labda kama mwanaume huyo si riziki,ila kama ni mwanaume wa kweli tusidanganyane
 
Zamani niliamini jambo hili linawezekana. Lakini kupitia uzoefu wangu nimeona jambo hili haiwezekani. Nitashare nanyi uzoefu wangu.

Nimewahi kufahamiana na wadada kadhaa katika pilikapilika zangu za maisha aidha kupitia huduma anayotoa au kama mteja kwangu lakini mwisho wa siku wenzangu wamekuwa na idea ya kuishia kuwa wapenzi kinyume na malengo yetu

Nianze na huyu dada ni mwite d, baada ya yeye kunihudumia mara kwa mara basi tukawa tunawasiliana kawaida tu kibiashara mfano kutaka ufafanuzi wa jambo fulani kama nimekwama.

Nakumbuka ilikuwa siku ya mwaka mpya 2013 nikaamua kuandika meseji ya kawaida ya kuwatakia heri ya mwaka mpya watu wote waliokwenye simu yangu, huyu d alipoipokea alifurahi naye alijibu vizuri tu tena kwa furaha. Iipopita siku 1, majirani yule dada alianza kuhoji kwa nini niliamua kumtumia ile sms, nilijitetea kwamba ilikuwa sikukuu kwa hiyo nikaona si vibaya watu wanaofahamiana kutakiana heri ya mwaka mpya lilikuwa ni hilo nilimalizia. Kilichofuata nilitukanwa mpaka basi sikujibu mpaka basi mpaka sasa sijui nilikosea wapi?

Wapili alikuwa ni mteja wangu alinipenda tu. Na mpaka sasa sijui huyu dada alinipendea nn ghafla hivyo, huyu alikuwa mteja wangu wa viatu mara nyingi alipenda kununua viatu kwangu tukawa tumezoeana. Akanikaribisha kwake kumbe alikuwa mwalimu na hajaolewa alikuwa anamalizia masters yake, nilivutiwa na mazungumzo yake siku hiyo tukajikuta tumefika saa 9 usiku tangu saa 2, yule dada ana akili balaa za darasani na za maisha

Siku hiyo aliniaga anaondoka kwenda kuanza kazi kama mhadhili msaidizi, katika moja ya vyuo hapa Tz. Nilihuzunika sana Maana alikuwa ameshakuwa rafiki yangu.

Mungu si matoborwa baada ya wiki matokeo ya usaili yalitoka nimefaulu na kupangiwa kazi karibu na wilaya alipo. Hunisisitiza sana nimtembelee kwake, Kutokana na uzoefu nilioupitia nimekuwa mzito juu ya hili ukizingatia ameanza kuonesha element za mapenzi wazi na mimi siko tayari ukizingatia nina mchumba wangu

Mimi huwa si rahisi kumzoea dada maana huwa si mtu wa maneno mengi. Tutaongea kiofisiofisi basi ukiongezea na uzoefu wa kutukanwa na yule dada ndo kabisaa ofisini wadada wameanza kuniita mgumu,

nipeni mbinu wadau mmewezaje kumaintain urafiki wa jinsia tofauti? Bila kuishia kufikia mapenzi. Ili tusifike huko na mwalimu anamadini hatar Sitaki tugombane hadi mwenyewe atakapoona inatosha for good. Nawasilisha

Uko sawa Kabisa kwa 100%! hakuna urafiki kati ya Mwanamke na Mwanaume, hivyo siku demu wako akikwambia huyu ni rafiki yangu ujue ipo siku, ipo siku tu watalalana na kinyume chake!
 
Last edited:
Hiyo saa tisa unaongea ulikuwa na lako jambo, kwa maana yeye asingekuambia uondoke. Turudi kwenye mada, urafiki wa mwanamke na mwanaume upo endapo kila mmoja wenu ana mtu wake na kila mmoja anampenda mpenzi wake kwa dhati. Mimi nimekuwa na marafiki kadhaa wa kadhaa katika maisha yangu na bado tunaendelea kuwa marafiki. Cha msingi ni kuondoa hisia za mapenzi unapokuwa naye, maana wao wanawake mara nyingi huwa hawawaanzi wanaume hata kama wanawapenda. Hivyo unapokuwa naye usionyeshe dalili zozote za mapenzi na kama yeye pengine kakaa vibaya kwa bahati mbaya au kwa maksudi usiste kumwambia samahani, umekaa vibaya. Mara zote kaa naye na uongee nae kama vile uko na dada yako.

Sasa wewe uko na mwanamke halafu uanaanza kumsifia eti ooh...mara sijui umeumbika...mara namuonea wivu shemeji yangu unategemea nini?

Mbaya zaidi uso wako wote ukiwa naye facial expression ni full sex!

Yeye ni Malaika?

Yangu ni hayo tu jamani
 
Kama hutaki kuaminishwa maana yake hufai kwenye mjadala na wewe si mtu wa maendeleo kwa kuwa hutaki kujifunza. Uzoefu wako si ruler kwa dunia nzima na hasa inawezekana tatizo lako ni hiyo tabia yako ya kukataa kujifunza.

Umeleta hii kitu hapa ili tufanye nini kwanza?
 
Inawezekana tena hasa kwa wale men wenye maneno mengi (waongeaji sana) ila kama Mungu hakukujalia maneno mengi kama mimi lazima at the end uishie kwenye mapenzi tu maana hakuna namna nyingine na kama sio mapenzi basi urafiki huwa hauchukui muda una kufa
 
Mkuu we ushauri wala kujifunza hutaki kulingana na maelezo yako.
Sasa mkuu utakuwa umefanya jambo la mbolea sana ikiwa hiyo namba ya huyo ticha utanitumia mie naweza kama wewe huwezi.
 
kama mtu wako ana mtu wa jinsia tofauti pembeni kisha anakuambia eti ni rafiki tu stuka mama utaibiwa,labda kama mwanaume huyo si riziki,ila kama ni mwanaume wa kweli tusidanganyane
Sikulazimishi hayo ni mawazo yako na ubongo wako umeishia hapo kufikiri.
 
Na mie nilikuwa najiaminisha kuwa kuna huo urafiki lakini mwisho nikajagundua najidanganya mwenyewe
 
Back
Top Bottom