Elections 2015 Hakuna upinzani wa kweli bila tume huru Tanzania

Kupiga kura ni haki ya kila mwananchi ya kikatiba na ni muhimu kupiga kura.

Kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi ama mazingira halisi tuliyonayo Tanzania, wa kulaumiwa si mwananchi anayepiga kura.

Ni ujinga wa wazi kabisa wa viongozi wa upinzani kuendelea kuendesha kampeni za marudio ya uchaguzi wakati wakijua kula ya mwananchi anaye hamasishwa kupiga kura haina impact ama wewe kiongozi huna uwezo wa kuitetea na kuilinda haki yake hiyo ya kumchagua kiongozi anaye mtaka isi dhurumiwe.

Mi nitaendelea kuwashangaa viongozi wa upinzani wanao lialia badala ya kutafuta namna bora ya kulinda haki ya mwananchi anaye hamasishwa kupiga kura.

Labda niseme hili kwa viongozi wetu hawa; Tunataka katiba mpya, tunataka tume huru ya uchaguzi acheni kulialia.!
 
Back
Top Bottom