Elections 2015 Hakuna upinzani wa kweli bila tume huru Tanzania

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana Jamiiforums,

Nimepitia sehemu kadhaa nikiangalia maoni ya watu wengi, walikuwa wakilaumu wapinzani kuingia kwenye uchaguzi bila kurekebisha sheria za uchaguzi na tume huru, majimbo mengi ilikuwa ubabe ubabe, watu waliachana na mita 200 za tume na sheria za uchaguzi na kukaa mita hamsini, waliokaa mita hamsini walifaulu kulinda kura na matokeo tumeyaona, waliokuwa waoga, mmeona matokeo, nawaasa sana wale wote waliochaguliwa kuweni makini katika utendaji wenu kwa sababu watu tuna hasira ya maendeleo, wakati wa ndio mzee umeisha.

Wakati wa hili ni jimbo langu yamekwisha, wale wazee wasumbufu, wakina, Mrema, Cheyo, wanaokuwa hawana upande wameondoka, lililobaki tuungane kwa pamoja kumshawishi Zitto arudishe moyo kuungana na vijana wenzie kujipanga upya kuleta democrasia ya kweli, pamoja na mbilinge ya CCM kugomea matokeo kuhesabu kwa siku tatu mpaka nne, bado wananchi wameonyesha ushujuaakwamba hawataki mchezo kwa mtu wa kuchaguliwa, kikatio cha kweli kimefanya kazi, aliyekataliwa kakataliwa aliyekubaliwa ajiandae kuhudumia watu wake.
 
Kosa kubwa ni la UKAWA kwenda kwenye uchaguzi mkuu huku wakijua fika Tume ya Uchaguzi NEC siyo huru ni ya CCM walifanya hivyo wakitegemea nini? Watu wote wa NEC wameteuliwa na Kikwete then unategemea kushinda uchaguzi ni miujiza. Turudi kazini tujenge taifa huku tukidai Tume Huru kwa nguvu zote mambo ya kudai umeibiwa kura hayana msingi ni kupoteza muda.
 
kamuulize mbowe na Lissu

mmewafanya hao viongozi wenu kama miungu, hauwezi kuwakosoa wala kuwashauri; mkiangukia pua ndio mnajua tatizo liko wapi??

ndrbbb
 
Kosa kubwa ni la UKAWA kwenda kwenye uchaguzi mkuu huku wakijua fika Tume ya Uchaguzi NEC siyo huru ni ya CCM walifanya hivyo wakitegemea nini? Watu wote wa NEC wameteuliwa na Kikwete then unategemea kushinda uchaguzi ni miujiza. Turudi kazini tujenge taifa huku tukidai Tume Huru kwa nguvu zote mambo ya kudai umeibiwa kura hayana msingi ni kupoteza muda.

sidhani kama kuna mwaka ntapiga kura ikiwa tume huru ya uchaguzi haitakuwepo na katiba inayoeleweka. Hili lilikuwa kosa kubwa sana kwa UKAWA
 
lowasa alijua atashinda kwa kutumia mfumo wake wa ccm ila hakujua ccm sio chama cha mtu bali watu ndio maana kapata kibano sasa akafuge ng'ombe huko monduli
 
itapatikana hadi pale mtakapo ihitaji na mtakapo kuwa tayari kuipata kwa nguvu na akili zenu. kwa sasa wengi hampo tayari
 
hakuna tume huru,na hamtashinda kamwe .
Ukawa mtaishia kuwa wapinzani milele
 
Uko sahihi kabisa.Tusikubali asilani kupiga kura bila kuwa na tume huru.Ni uzumbukoko.
Kosa kubwa ni la UKAWA kwenda kwenye uchaguzi mkuu huku wakijua fika Tume ya Uchaguzi NEC siyo huru ni ya CCM walifanya hivyo wakitegemea nini? Watu wote wa NEC wameteuliwa na Kikwete then unategemea kushinda uchaguzi ni miujiza. Turudi kazini tujenge taifa huku tukidai Tume Huru kwa nguvu zote mambo ya kudai umeibiwa kura hayana msingi ni kupoteza muda.
 
Basi sina shaka kura halisi za mtanzania zitaipa upinzani ushindi mkubwa tatizo ni tume kujaa uccm kuanzia mwenyekiti hadi kule chini ni ccm
Mwisho niseme tu tunaitaji tume huru ya uchaguzi hili sio ombi bali ni lazima
 
Mbona Lubuva kishasema tume yake ni huru na hakuna mwenye ubavu wa kuiingilia ?
 
Basi sina shaka kura halisi za mtanzania zitaipa upinzani ushindi mkubwa tatizo ni tume kujaa uccm kuanzia mwenyekiti hadi kule chini ni ccm
Mwisho niseme tu tunaitaji tume huru ya uchaguzi hili sio ombi bali ni lazima
Unatakaje labda mbona ueleweki
 
Tatizo si kudai tatizo hao wazee wa mipasho ccm watakubali maana wao ndio siwaelewi kabisa
 
Back
Top Bottom