Hakuna uhusiano wowote kati ya demokrasia na maendeleo

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,003
2,000
Tabia ya demokrasia ni kuweka mlolongo wa mambo ambapo hata maamuzi mazuri na yenye tija bado yanahitaji maamuzi ya wengi ili yatekelezwe tofauti na mahali ambako hakuna demokrasia mnyororo wa maamuzi ni mfupi hivyo mambo yote yenye tija huamuliwa kirahisi na kutekelezwa.

Kwa maoni yangu maendeleo ni matokeo ya kuongozwa na kiongozi/ viongozi mwenye upeo wa kuona mbali na mwenye usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa hayo maoni.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,901
2,000
"...Mambo yote yenye tija", na wala hukujisumbua kueleza ni nani hasa au mambo hayo yanaletwa na nani na ni nani huamua kwamba haya ndiyo "mambo yanayoleta tija"!

Huyo "kiongozi mwenye upeo", na yeye sijui anatokana na nini?

Kama kiongozi ni mwenye upeo hawezi kamwe kuwaogopa wananchi wake na kuacha kuwashirikisha katika mambo yanayowahusu wananchi hao.

Hizi mada nyingine tunajianzishia tu bila kuwa na fikra nzito juu yake.
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,540
2,000
Tabia ya demokrasia ni kuweka mlolongo wa mambo ambapo hata maamuzi mazuri na yenye tija bado yanahitaji maamuzi ya wengi ili yatekelezwe!

Tofauti na mahali ambako hakuna demokrasia mnyororo wa maamuzi ni mfupi hivyo mambo yote yenye tija huamuliwa kirahisi na kutekelezwa.

Kwa maoni yangu maendeleo ni matokeo ya kuongozwa na kiongozi/viongozi mwenye upeo wa kuona mbali na mwenye usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa hayo maoni.
Kwa kuwa uumunimi wa udikteta, ni sawa.
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
15,291
2,000
Tabia ya demokrasia ni kuweka mlolongo wa mambo ambapo hata maamuzi mazuri na yenye tija bado yanahitaji maamuzi ya wengi ili yatekelezwe!

Tofauti na mahali ambako hakuna demokrasia mnyororo wa maamuzi ni mfupi hivyo mambo yote yenye tija huamuliwa kirahisi na kutekelezwa.

Kwa maoni yangu maendeleo ni matokeo ya kuongozwa na kiongozi/viongozi mwenye upeo wa kuona mbali na mwenye usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa hayo maoni.
Nchi hizi 3 ziliwahi kutawaliwa na Madikteta kamili, hebu tupe aina ya maendeeo waliyonayo;
1.Afrika ya kati.
2.DRC
3.Uganda.
 
mazojms

JF-Expert Member
Sep 22, 2017
1,528
2,000
Demokrasia inafanya kazi pale tu ambapo kila mmoja atashirikishwa, atawajibika na atashiriki.

Shida ni ufahamu hafifu wa tafsiri ya maneno "kuwajibika, kushirikishwa na kushiriki" , watu wanapenda kushirikishwa lakini hawapendi kuwajibika na kushiriki.

Jamii yenye watu wasiopenda kuwajibika na kushiriki, demokrasia haiwezi kufanya maendeleo yeyote.
 
Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,479
2,000
Tabia ya demokrasia ni kuweka mlolongo wa mambo ambapo hata maamuzi mazuri na yenye tija bado yanahitaji maamuzi ya wengi ili yatekelezwe!

Tofauti na mahali ambako hakuna demokrasia mnyororo wa maamuzi ni mfupi hivyo mambo yote yenye tija huamuliwa kirahisi na kutekelezwa.

Kwa maoni yangu maendeleo ni matokeo ya kuongozwa na kiongozi/viongozi mwenye upeo wa kuona mbali na mwenye usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa hayo maoni.
Lete case study.
Mimi naleta ya Europe
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,405
2,000
Tatizo sio dictator shida ni ubinafsi mbona libya waliongozwa na dictator ila walikua na hali nzuri Hadi kufikia hatua ya kufadhili umoja wa africa!?

Kwahiyo Gadaffi hakuwa mbinafsi? Naona umekuja na utetezi ule ule wa kutetea watu waovu ili waendelee kutawala, kisha ukiona limejengwa daraja useme ni kwakuwa kiongozi aliyepo ana maono hata kama hajali demokrasia, kana kwamba kukiwa na demokrasia bado daraja halitajengwa.
 
Malcom Sr

JF-Expert Member
Apr 17, 2021
991
1,000
Nimewaza huu ujinga wetu miafrika ..

Yaan Rais anatoa bilion34 kujenga kariakoo only...wakati fedha hizo zingetosha kutuwekea maji Safi mikoa ya Lindi na Mtwara na Ruvuma ambapo 75%tunakunywaji maji ya tope..

Na bei ya dumu la maji Ni 500 Sasa...Toka naanza awali miaka ya 1990 mpk leo tunamkamua chura ...

Ni aibu Sana ....Kuna mdau aliandika humu Viongozi wa Afrika hawana Future Plans na hata hiyo mipango Plans ya Taifa haifuatwi...

Pumbavu kabsaaaa...Demokrasia Afrika Ni Pasua Kichwa...kwa viongozi..
 
The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,003
2,000
Kwahiyo Gadaffi hakuwa mbinafsi? Naona umekuja na utetezi ule ule wa kutetea watu waovu ili waendelee kutawala, kisha ukiona limejengwa daraja useme ni kwakuwa kiongozi aliyepo ana maono hata kama hajali demokrasia, kana kwamba kukiwa na demokrasia bado daraja halitajengwa.
Swali la muhimu ni kwamba chini ya dictator au chini ya demokrasia iliyopo sasa libya ni wakati gani walishuhudia ustawi wa wananchi!?
 
FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,529
2,000
Hao viongozi wenye upeo wanashuka kutoka sayari gani?

Dikteta ndiye kiongozi mwenye upeo? Hoja dhaifu!

Maendeleo ni pamoja na raia kunufaika na haki zao kama raia, ikiwemo haki ya kuwa huru na kuwachagua viongozi wanaowataka.
 
MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,862
2,000
Mleta, Kwa hiyo Tanzania kuna udikteta na ni Faida?

Au unataka kusema hizi juhudi za kuuwa Demokrasia Tanzania unazibariki?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom