Hakuna uhuru wa pa kusemea ila kuna uhuru wa vyombo vya habari!!!!

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,658
3,646
Wakuu leo tuongelee hili jambo la kusema eti Tanzania kuna uhuru wa kutoa maoni. Mimi nasema si kweli!!! Ukweli ni kwamba kuna uhuru wa vyombo vya habari yaani vimeruhusiwa kuanzishwa na kufanya shughuli za kupasha habari. Lakini habari zenyewe ni zile ambazo zimechujwa na vyombo hivyo vya habari kukidhi matakwa ya waliovianzisha. Mfano, mahala sisi wananchi tunapotakiwa kutoa maoni basi hayarushwi moja kwa moja mpaka kwanza yachujwe.
Ama utakuta chombo cha habari kinapenda kutoa fursa ya kukosoa mtu au taasisi nyingine lakini chenyewe hakitaki kusemwa!!! Na ukitoa maoni kupitia chombo hicho yanayogusa maslahi ya chombo hicho, basi maoni yako hayatarushwa. Maelezo ni mengi lakini kwa kifupi ni kwamba hakuna uhuru wa kutoa maoni maana hata vyombo vyenyewe vya habari vinatubana sana. Na angekuwa ni kiongozi na si chombo cha habari ndio anayetubana sisi watoa maoni vyombo vya habari vingemwita "dikteta". Namalizia kwa kusema tusidanganyane.....hakuna uhuru usio na vikwazo au mipaka.
 
Back
Top Bottom