Hakuna ufisadi mkubwa kama ufisadi wa haki ndani ya mahakama. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna ufisadi mkubwa kama ufisadi wa haki ndani ya mahakama.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Jun 3, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Haki imekuwa ikiiuzwa ikinunuliwa. Mahakama zetu zimekuwa sehemu ya hujuma bila woga ukandamizaji na udhalilishaji. haya yanatokea na wanayoyafanya haya ni wasomi na watu wanaoheshimika sana ndani ya jamii yetu.

  Akihojiwa Jaji mstaafu wa mahakama kuu kwa jina moja namkumbuka kama Steven alikiri kuwa huwa ikulu hushinikiza hukumu kwenye kesi zenye maslahi na Ikuku, mtu wa ikulu au kiongozi wa ndani ya Ikulu. Inasikitisha sana.
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkubwa!naunga na wewe,lakini mimi nasema ufisadi mkubwa ni ule wa kwanza. Ushindi wa wizi wa kura kwa rais na kumfanya kushinda kwa kura za wizi hadi kwenda kuapishwa harakaharaka, huu ndio ufisadi wa kwanza na mkubwa.

  Kwanini nasema hivi, dhambi huzaa, hupata watoto na hatimae vijukuu. Fatilia viongozi wasiokua na maadili wote wameteuliwa na yule aliyepata urais kwa njia ya wizi wa kula. Kaa ukijua nyoka hawezi kuzaa bata hata siku moja.
   
Loading...