Hakuna uchaguzi 2020

Mjema Vushanje

Senior Member
Sep 24, 2017
159
353
KAMA UNATEGEMEA KUFANYIKA UCHAGUZI MKUU 2020 ONDOA NDOTO HIYO!
Mimi sio nabii kama Lema au Tb Joshua lakini ninao uwezo wa kuona mbali kidogo, hebu ngoja nikushirikishe.

Ukweli ni kwamba kwa hapa nchi yetu ilipofikia ni wazi kuwa hatuwezi tena kwenda kwa utaratibu uliozoeleka, kwamba uchaguzi kila baada ya miaka mitano...things have changed!

Nasema hakuna uchaguzi mkuu 2020 kwsababu ;

1. Mchakato wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kwasasa ndio itakuwa kilio na agenda ya watanzania ambayo serikali ya ccm haitoikubali kwani kuikubali ni kumaanisha mwisho wa ccm madarakani.

2. Vyama vikuu vya upinzani (UKAWA) Havitokubali kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya na hii itafanya eidha vyama vidogo vishiriki na kuifanya ccm ikose upinzani wa kweli ama ikitokea vyama vyote vya upinzani vikiugomea uchaguzi ccm itaanzisha vyama vidogo vidogo vya kuzugia. Hapa machafuko yataanza na kulazimu hali ya nchi ibadilike kabisa na kufikia kama Congo.

3. Uchaguzi utacheleweshwa kwa kigezo cha kutaka kupitia maudhui ya katiba mpya kwani shurutisho zitakuwa nyingi kutoka kwa vyama vya siasa, taasisi za dini, wana harakati na wananchi kwa ujumla, walioko madarakani watatumia mwanya huu kuendelea kubaki madarakani kwani wanajua itapopita katiba mpya na uchaguzi kufanyika ccm itapata chini ya 30% ya kura zote.

4. Ndani ya CCM ataibuka kigogo mmoja ambaye kwasasa yuko kimya sana na kutangaza kutia jina ili apambane na aliyepo kwa madai ya kukinusuru chama, huyu ataisomba ccm yote ambayo kwasasa haina sauti na watamuona mkombozi wao, mtu huyu atakivuruga chama mno na hali hii itaibua kundi lingine lenye maslahi kwenye utawala huu na kuamua kusogeza uchaguzi mbele ili wazidi kubaki madarakani, pamoja na hilo bado huyo atakayetia jina ndani ya chama hatakubalika kwa wananchi wengine na lazima mshindi wa kiti kikuu atatokea upinzani na ninamjua.

5. Kati ya 2021na 2022 uchaguzi itabidi ufanyike na everything about ccm itakuwa over, tutakuwa na Tanganyika na Zanzibar, tutakuwa na Rais wa Muungano na tutakuwa na magavana, tutakuwa na mihimili yenye nguvu mitatu na isiyoingiliana kiurahisi 1.Bunge 2.Mahakama na 3. Serikali.
Note: Kwa kipindi hiki maandamano hayatakuwa na nguvu sana isipokuwa hapo 2020 ambapo homa ya uchaguzi itakuwa juu sana!

Msiogope, ni lazima tupitie hapa ili nchi ikae vyema, ni ngumu sana kung'oa jino la mtu mzima kwani limeishi mda mrefu kuliko la mtoto ambalo unasukumiza tu kwa kidole.
 
Hivi ccm haijui haya yatakuja,wadia siku za usoni hapo ndio watajua safari bado sana,
 
Back
Top Bottom