Hakuna Timu inaitwa"AC VITA",ni "AS VITA".

CAGvsSPEAKER

JF-Expert Member
May 16, 2019
1,340
5,048
Nasikiliza kipindi cha michezo muda huu Clouds FM,namsikia mtangazaji anasema timu ya AC VITA imefuzu.....hili ni kosa na limekuwa likirudiwa mara nyingi na watangazaji na wachambuzi wengi wa mpira wa miguu. Ile si AC VITA,ni AS VITA.
 
Na pia huwa hakuna kitu kinachoitwa 'best losers', ila waandishi wa kibongo dizaini ya Kitenge sijui wameleta tafsiri ya moja kwa moja ya kiswahili ndio likawa linatamkwa kimakosa. Kimataifa, nafasi hiyo huitwa runners-up
 
Ni AS VITAL na si AS VITA.
Na wewe umebugi!
Halafu hilo ni jambo la kuanzishia uzi kweli?
 
Sawa nimekusikia nipo na mkazuzu na cotinyo hapa ila edgar kibwana fala Sana aniita simba pisi Kali wote hapa studio tumeshtuka
 
Na pia huwa hakuna kitu kinachoitwa 'best losers', ila waandishi wa kibongo dizaini ya Kitenge sijui wameleta tafsiri ya moja kwa moja ya kiswahili ndio likawa linatamkwa kimakosa. Kimataifa, nafasi hiyo huitwa runners-up
Hivyo ni vitu viwili tofauti,km kama kuna makundi 3 yenye timu 4 kila kundi na zinatakiwa zifuzu timu 8 tutachukuwa washindi 3 kila kundi runners up 3 kila kundi na over all best losers 2 kati ya hayo makundi 3 tunapata jumla ya timu 8
 
wala hakuna walichokosea hapo mkuu kwenye kiingereza hasa matamshi S haitamkwi "esi" bali inatamkwa "sss" kwahiyo AS vital ni sawa.....
 
Nafikir ni mazoea ya kimatamshi
Tusiwashushe vyeo kwa hilo
Unaifahamu tofauti ya C na S?
Hivi panapotakiwa S wewe ukaweka C mathalani ni kwenye interview kazi utaipata?
Hakuna kitu kinakera kama mtu akosee neno hala akuambie"nafikiri umeeleewa". Ni ujinga.
 
  • Thanks
Reactions: Gef
Na pia huwa hakuna kitu kinachoitwa 'best losers', ila waandishi wa kibongo dizaini ya Kitenge sijui wameleta tafsiri ya moja kwa moja ya kiswahili ndio likawa linatamkwa kimakosa. Kimataifa, nafasi hiyo huitwa runners-up
Hapana, best loser ipo.

Hii inaapply pale ambapo mathalani kuna makundi 5 ya timu nne kila kundi lakini mnahitaji timu 12 kufuzu next round. What happens ni kwamba zitachukuliwa timu 2 zilizofanya vizuri kila kundi kupata jumla ya timu 10 and then kukamilisha timu 12, hapo zitachaguliwa timu 2 bora kati ya walioshindwa wale waliopata nafasi ya tatu kila kundi. So, ni best losers among washindi wote watano walioshika namba 3.

Kuhusu runner-up, hilo ni neno linalowakilisha mshindi namba mbili katika aina yoyote ile ya mashindano.

Nadhani nimekusaidia kwa kiasi flani kukuelewesha.
 
Jane nimekuelewa mamaa!!

Uzuri wako na akili yako vimefanana....kwanza ni mzuri halafu mweupe...........NASEMA UONGO NDUGU ZANGUUU??
 
Back
Top Bottom