Hakuna tena Mahubiri ya habari njema, kuacha dhambi, msisitizo ni matoleo

Yapo kwa wingi sema tu unaingia makanisa ya wazinzi.
Ukija kwa pastor Joshua Mwembeyanga ndipo utayakuta hayo mahubiri.
Unaweza kuabudu huku mwaka mzima usisikie mahubiri ya sadaka.
Hata mahubiri ya kurudi kwa yesu kwa mara ya pili hakuna siku hizi, wanahubiri maendeleo,mali,utajiri na mengineyo ya dunia pekee .
 
Ndugu yangu ndio maana Suleiman aliomba Hekima. Binadamu unapokuwa Masikini wa Akili basi utadanganywa sana. Ndio maana baadhi ya watumishi wameteka Akili za waumini wengi. Inahitaji hekima kubwa kubaini hili neno ni Halisi au Tango Pori.

Unakuta Mchungaji anakuja anasema eti Jana ameongea na Mungu na Mungu kamuagiza aje atuambie moja, mbili, tatu. Kwakweli Mimi huwa sikubali kama kweli kapewa hayo maagizo. Kwanza akutane naye wapi.
Umenifanya nicheke kwa sauti kubwa,
 
Leo nimepata mafundisho kutoka kwa Padri na si tapeli. Amesema uhusiano wa kwanza wa binadamu uwe kati yako wewe na Mungu kwa sala. Sala humuweka shetani mbali.

Uhusiano wa pili ni kujitoa kwaajili ya wenye uhitaji. Huwezi kujiita Mkristu wakati kuna mjane unaemfahamu ana shida ya pango. Hata ikibidi ukose chakula msaidie.

Tatu funga hata siku moja kwa wiki. Yesu mwenyewe aliteswa sasa wewe ni nani uishi duniani bila mateso!
Unapaswa kutunza watu wa nyumbani kwako kabla ya kujali wajane.
Asiyetunza wa kwao ni mbaya kuliko asiyeamini.
 
Asante kwa andiko zuri, siku hizi wachungaji /manabii/mitume, nk. wengi wao ni pesa kwanza MUNGU baadaye, wanasahau 1Timotheo 6:5 wameufanya ukristo ni njia ya kujipatia faida.
 
Kuna miji isiyo na kuta kuna miji isiyo na vitabu kuna miji haina wafalme isiyo na nyumba wala hazina na tena kuna miji haina hata mahali pa kuchezea michezo lkn mji usiyo na hekalu , msikiti , au mahali pa kuabudia kwa ibada za kipagani hakuna mtu aliyewahi kuuona mji wa namna hiyo kumcha MUNGU ni sehemu ya asili ya mwanadam. lkn KUKANA UWEPO WAKE MUNGU ni ugonjwa ustaarabu na dalili ya uharibifu wa tabia ambayo ni sawa na kujiua kimakusudi na vile vile n dalili ya uharibifu wa ulimwengu.
Mkuu,

Kuna kipindi watu karibubdunia nzima waliamini dunia ni ya ubapa (flat).

Lakini watu kuamininhivyo, hakukufanya dunia iwe flat.

Kama.Mungu hayupo, hata kila mtu akiamini Mungu yupo, hilo halifanyi Mungu awepo.

Thibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.
 
Ujenzi hauishi harambee haziishi ni kuomba pesa tu waamini hawaambiwi ukweli kwamba dhambi ni mbaya amri za Mungu na sheria za Musa wametupilia hukooo.

Ndo maana hawaoni hata maono wapo wapo tu. Haiwezekani rais anakufa akiwa madarakani hakuna cha askofu nabii mtume padre aliyeona maono tahazari ikachukuliwa,

Waambieni Mamndenyi ame wa disqualify.
Tatizo la mfumo wa udikteta, hata watu wakiwa na maono, wengi wanaogopa kuyasema.
 
Mkuu,

Kuna kipindi watu karibubdunia nzima waliamini dunia ni ya ubapa (flat).

Lakini watu kuamininhivyo, hakukufanya dunia iwe flat.

Kama.Mungu hayupo, hata kila mtu akiamini Mungu yupo, hilo halifanyi Mungu awepo.

Thibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.
Ni kama kipindi hiki tuu ww (na member wote humu) tunavoamini jamii forum ipo na kwamba ww n member wa humu ndani lkn nataka nikwambia JF haipo na kama unabisha thibitisha uwepo wake😇😇🤕
 
Back
Top Bottom