Hakuna tena Mahubiri ya habari njema, kuacha dhambi, msisitizo ni matoleo

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,330
4,771
Imani imezidi kumkamata MTU MWEUSI na watumishi wameendelea kusisitiza Kutoa ZAKA na FUNGU LA 10, UJENZI NA MAENDELEO YA JIMBO nk.

Hakuna tena Mahubiri ya HABARI NJEMA, KUACHA DHAMBI nk MsisitIzo ni MATOLEO na ili kulipa uzito basi kanisa LITATOA Mualiko kwa Mchungaji/Mtumishi anayejua kushawishi vizuri.

Imefika wakati Muumini anabeba sadaka yake ya Elfu 2 na njiani anapopita anakuta kuna kipofu kanyoosha mkono kuomba hela na pengine ana mtoto anayehitaji hata kikombe tu cha chai, lakini Muumini huyu atapita na kujiwazia kuwa hela aliyonayo ni ya SADAKA KANISANI.

HAKIKA INGEKUWA KIPINDI KILE CHA YESU ANGESEMA HIVI " ENYI WATUMISHI ACHENI KUWADANGANYA WAUMINI WENU", " ENYI WAUMINI TUMIENI AKILI NA UJINGA UWATOKE"/

Pili Muumini Masikini atahimizwa kutoa matoleo lakini akiugua hana hata hela ya panadol lakini uongozi wa Kanisa ukipata taarifa za kuugua wao watasema " TUMUWEKE KWENYE MAOMBI". Badala ya kutoa fedha kidogo za Sadaka.

KANA KWAMBA SADAKA NI KWA AJILI TU YA HUDUMA KWA WATUMISHI , UTAWALA NA UJENZI lakini siyo kusaidia waumini wasiojiweza.

KIDOGO NAWASIFU RC angalau
 
Ni sahihi.
Sadaka zetu zimekua ni kama matairi ya baiskeli kwamba yanatakiwa kujazwa upepo periodically ili kuendelea kuwa useful. Bila Mchungaji kanidani kuongea vifungu vya kutosha na kufoka unaona sadaka yako haitakua useful mbele za Mungu.
 
Leo nimepata mafundisho kutoka kwa Padri na si tapeli. Amesema uhusiano wa kwanza wa binadamu uwe kati yako wewe na Mungu kwa sala. Sala humuweka shetani mbali.

Uhusiano wa pili ni kujitoa kwaajili ya wenye uhitaji. Huwezi kujiita Mkristu wakati kuna mjane unaemfahamu ana shida ya pango. Hata ikibidi ukose chakula msaidie.

Tatu funga hata siku moja kwa wiki. Yesu mwenyewe aliteswa sasa wewe ni nani uishi duniani bila mateso!
Tatizo kuna Mkrito na Mkristu.Hawa pia ni watu wawili tofauti.Hata imani zao ni tofauti
 
Thread fikirishi mno.Nakubaliana wewe Sikh hizi hakuna mahubiri ya kukemea dhambi tena.

Msisitizo upo kwny ishara zaidi kwa back up ya shuhuda chache.
Shuhuda hizo lazima ziwe
Kupona, baraka za kazi, kuolewa,nk

Wanasema ni injili ya utajilisho.sijui hv kwngneko duniani nao wana mwelekeo huu
 
Leo nimepata mafundisho kutoka kwa Padri na si tapeli. Amesema uhusiano wa kwanza wa binadamu uwe kati yako wewe na Mungu kwa sala. Sala humuweka shetani mbali.

Uhusiano wa pili ni kujitoa kwaajili ya wenye uhitaji. Huwezi kujiita Mkristu wakati kuna mjane unaemfahamu ana shida ya pango. Hata ikibidi ukose chakula msaidie.

Tatu funga hata siku moja kwa wiki. Yesu mwenyewe aliteswa sasa wewe ni nani uishi duniani bila mateso!

Yak 1:27​

Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

Yak 1​

Salamu
1 Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu.
Imani na Hekima

2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. 6Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 7Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 8Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

Umaskini na Utajiri

9 Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa; 10bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka. 11Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

Majaribu na Mateso

12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. 13Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. 14Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. 15Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. 16Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. 17Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. 18Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.

Kusikia na Kutenda Neno

19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika; 20kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu. 21Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. 22Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake. 26Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. 27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
 
Back
Top Bottom