Hakuna Tanganyika wala Raisi wa Zanzibar kuwa makamu Muungano, nipe uhalali wa Muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna Tanganyika wala Raisi wa Zanzibar kuwa makamu Muungano, nipe uhalali wa Muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Apr 30, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0  Written by mkulima // 30/04/2011 // Habari // No comments

  Kilicho unganicha Muungano hakiko tena kiungo,ikiwa Raisi wa Z’bar ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri na ni waziri asio na wizara sasa Wz’bar tunasubiri nini?.
  Hivi sasa hakuna tena Muungano kuna utapeli tu wenzetu wa Tanganyika wanawafanyia viongozi wa Smz na wao wakaridhika kutokana na njaa zao,sasa tuseme viongozi wetu wana ridhika na kuuza utaifa wao na utu wao na nchi yao?,Hili ndio jibu lakujiuliza Wazanzibar.
  Asari za kupotea kwa utaifa wa Mzanzibar hazito malizia kwa wazanzibar wakawaida tu,zitawakuta hata Wajukuu wa Kificho na Samia.
  Hivi juzi kulikuwa na sherehe za kutimiza miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulio asisiwa na wasisi wawili Mwalimu Julias Nyerere na Mh Abedi Amani karume? Wote hawa walikuwa ni maraisi na nchi zao na watu wao? Wakakubali kunganicha nchi zao.
  Sasa mazingaombwe yalio fanywa kwa vile upande moja haukuwa na nia ya Muungano nia ni kujifanya mkoloni mpya wa Kuwatawala Wazanzibar ni kuwa Raisi wa Tanganyika yupo yani Jakaya Mrisho kikwete lakini Rasi wa Zanzibar hayupo kimtazamo wa Muungano kuna Mjumbe wa baraza la Mawaziri na Waziri asiekuwa na hawizara malumu.
  Wenyewao Smz hujifurahisha husema nchi inayo Raisi wa Zanzibar lakini mimi nasema tuna mjumbe wa kamati kuu ya ccm, maana mara zote Rais ni yule aliochaguliwa na wananchi wake na kuwaskiliza wananchi wake sio kuskiliza sera na ilani za chama.
  Huyu wasasa ndio kazidi maana hata kura ya diwani hakupiga Zanzibar kapiga Tanganyika kaletwa tu Zanzibar kama Mwari kuja kusimikwa uraisi na washenga wake Mzee Kondom na Dume la Nyani.
  Na ili tujuwe kuwa hatuna Dume Zanzibar nikuwa kila kinacho husu Mustakbali wa Zanzibar husema ngoja kwanza niulize Tanganyika.
  Jee Wao Watanganyika (Kikwete)mambo yenye maslahi na nchi yao wana tuliza sisi? Mfano mdogo tu kuhusu mswada wa Katiba haukumshirikisha Raisi wa Zanzibar kukaa pamoja na rais wa Tanganyika Kikwete bali ni wao Tanganyika kukaa pamoja na kutuamulia sisi lipi watakalo liwe?.
  Hii ndio zarau ya mwicho na viongozi wetu wa Smz kimya na hii haikuanza leo Nyerere aliitisha Bunge la Tanganyika na kuvunja mikataba yote ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kufanya ajuwavyo kwa kushirikiana na ndugu zake wa Tanganyika bila kuwashirikisha Wazanzibar.
  Nipale alipo itisha Bunge na kusema kuanzia sasa hakuna tena Tanganyika wala katiba ya Tanganyika ? kila palipo andikwa Tanganyika andika Tanzania, ndio ukaona hapo ndio walipoanzia utapeli wa kutaka kuitawala Zanzibar kiujanja na kujifanya Wakoloni weusi.
  Hivi sasa husema Muungano wetu ni wapekee nikweli Muungano wetu niwapekee? Kwa sababu ukiuhoji Muungano Pinda na ndugu zake wanakuja juu? Wanajuwa kuwa kuna masuala katika Muungano hayana majibu ni kuwa-comfuse Wazanzibar ili watutawale kimbinu.
  Hii ile ukitaka kuliza Muungano ni lipi na lipi lisio la Muungano hupati jawabu utababaishwax2 na mwicho kuambiwa unataka kuvunja Muungano?. Wakati kuna mambo ya pande mbili yasio ya Muungano kwanza ni mawaziri na wizara zisizo za Muungano ? upande wa Zanzibar utasikia huyu waziri sio wa Muungano ni waziri wa SMZ mfano Wziri wa Kilimo,Afya,Utali etc hawa wote sio ktk Muungano lakini Bara utata ulopo ni kuwa Mawaziri wote niwa-Muungano na wao hujifanya ni ma-Big Boss mbele ya Mawaziri wa SMz?.
  Sasa kulikuwa na Sababu gani kuiuwa Tanganyika na Katiba yake yenye kusimamia mambo yasio ya Muungano? Lakini wenzetu husema hawawezi kufanya kitu kisicho na faida na wao, faida kubwa hapa ni kuturudisha tena katika ukoloni na utumwa wakututawala.
  Ndio ukaona hawataki kabisa wabara kuitaja au kuitamka Tanganyika ambai nimshirika mkuu wa Muungano na kuvunjika kwake ndio utata huu tulionao. Wamefanya hivi ili watule akili Wazanzibar na wamefanikiwa pakubwa kwa hili kutokana na viongozi wetu wa Smz kuwa zaifu na walafi wa kukumbatia Dunia na kuasha mambo ya umuhimu.
  Hii leo ngoma Watanganyika wameibadilisha hakuna hata kikao kimoja cha Muungano kinacho jadiliwa ki-Muungano baina ya watu wa pande mbili zilizo ungano vikao vyote hujadiliwa kichama na watu hao hao wa chama kimoja wakiwa na wakubwa wao wasio weza kuwatowa makosa.
  Ndio ukaona hata huyo Raisi wetu tuambiwae ni wa watu wa Zanzibar basi kukiwa na suala la Muungano halitetei kuwa ni Raisi wa Zanzibar hulitetea kichama na mpaka arudi Dodoma ktk halmachauri ya chama na vikao vya chama ndio alipatie jibu.
  Kwa nini tujiulize Wazanzibar iwe hivyo? Kwa sababu wameshanyoyoa mbawa kawa Butugali hana mbawa na kakubali kuwa Waziri asio kuwa na wizara ndio ukaona ktk mswada wa katiba ya Muungano hakushirikiswa yeye wala mkaguzi wa misidu ya Serengeti Mh Bilali.
  Hata Pinda alipo ulizwa masuala kuhusu mswada wa katiba ya Muungano itafanyika lini? Jibu alilojibu nikuwa nitanzungumza na Raisi Kikwete na hakusema nitazungumza na Rais wa Tanzania na Raisi wa Zanzibar.
  Mimi hujiuliza kuna sababu gani za viongozi wetu wa SMz kutuwakilisha ktk sherehe za Muungano wakati Muungano wenyewe fake usio kuwa na jibu mazonge matupu na haupo? Ikiwa Muungano upo eti list ingekuwa Raisi wa Zanzibar nikama vile Mh Abedi Amani kuwa ni makamo wakwanza wa Raisi ktk Muungano na kinacho sherehekewa kiwepo.
  Yani Serekali ya watu wa Tanganyika na Serekali ya watu wa Zanzibar? Lakini leo tunaambiwa Tanganyika haipo na makamo wakwanza wa Raisi wa Zanzibar hayupo sasa niwapumbavu kiasi gani viongozi wetu wa SMz kwenda kujizalilisha na kutuzalilicha sisi Wazanzibar?.
  Bora wangekwenda ktk Sherehe za chama chao ccm kuliko kusherehekea Mwiku,kitu kilichokuwa hakipo. Hizo nisherehe au matanga? Maana Tanganyika haipo na wala watanganyika hawaitaki kuwepo sasa vipi viongozi wetu wakubali kulishwa matapishi?.
  Mimi nasema kama Wazanzibar hatukushikamana kuuvunja Muungano fake basi tutakuja kujuta mbeleni na tutatafuta viongozi hawa walafi wa SMz kuwalaumu na wao watatulaumu sisi itakuwa Wazanzibar twalaumiana wenyewe wakati ni too late.
  Hawa viongozi wetu SMz ndio chanzo kikubwa cha matatizo ya Zanzibar na niwanafiki no 1,utaona ktk vikao vya Baraza la Uwakilishi husema Muungano unatunyoyo hauupi haki ya kiuchumi na kimaendeleo Zanziba ndio nyiyi ni viongozi silaha munayo kwa nini tusiitumie?
  lLakini ni unafiki tu wao hususani Ccm/Smz hawa nimakatili wakubwa wa Zanzibar na nimoto wakuuotea mbali munaweza kupanga hivi wakifika Dodoma wakichovaa nguo zao za unyama hubadilika na kuwa mafisadi.
  Wanasubiri Zanzibar ipewe asilimia % 5.4 bila ya kuvunja Muungano wallah Zanzibar haitoweza kunyanyuka kiuchumi wala kupiga hatuwa za kimaendeleo, hawa wabara sio ilikuwa wao kama kweli nindugu sisi tulio ungano waisaidie Zanzibar kwa vile Zanzibar ni ndogo na inawatu kidogo?.
  Lakini niwachoyo wao kila siku huzidi kuikandamiza Zanzibar nitafauti na nchi za kiarabu U.A.E Dubai ni nchi ndogo lakini walikubaliana jumuia ya kiarabu kuwa Dubai kwa vile haina ushumi waweke Freeport ili inyanyuwe ushumi wa nchi yake.
  Sisi Zanzibar wenzetu kutokana na choyo chao na roho mbaya yao waliiuwa Bandari ya Zanzibar na badae wakatuletea jini la TRA kuja kufonza mifupa, wakati huku zanzibar tuna ZRO na makoto mengine yalio tukabili na huku kiwango cha Mishahara Zanzibar nikidogo.
  Hii yote ni mbinu yakutula akili wa-Tanganyika ukiangalia mishahara ya Dubai nimikubwa kuliko nchi nyingine za UAE kwa vile ni ndogo na wananchi wake nikidogo ili wasiweze kuikimbia nchi yao Dubai,leo sisi hufanya hivyo kusudi kuwa Tanganyika mishahara mikubwa ili Wazanzibar wahame wahamie huko na kuiminya Zanzibar hata misada ya Muungano kwa njina la Tanzania basi hupewa %5.uwa Bandari ya Zanzibar na badae wakatuletea jini la TRA kuja kufonza mifupa, wakati huku zanzibar tuna ZRO na makoto mengine yalio tukabili na huku kiwango cha Mishahara Zanzibar nikidogo.
  Hii yote ni mbinu yakutula akili wa-Tanganyika ukiangalia mishahara ya Dubai nimikubwa kuliko nchi nyingine za UAE kwa vile ni ndogo na wananchi wake nikidogo ili wasiweze kuikimbia nchi yao Dubai,leo sisi hufanya hivyo kusudi kuwa Tanganyika mishahara mikubwa ili Wazanzibar wahame wahamie huko na kuiminya Zanzibar hata misada ya Muungano kwa njina la Tanzania basi hupewa %5.4 asilimia?.
  Wzanzibar tuvunje biashara na hawa matapeli na Majambazi wakubwa nchi wataiangamiza sio hawa, kujenga kwa Hamadi rashi Msasani na Shein Mbezi kusiwe ndio sababu ya kukubali kuua utaifa wetu.
  Hawa wana lao , na lao kubwa nikuimeza Zanzibar chini ya ilani za ccm na mawakala wao smz, kama sio chadema kukataa msada wa katiba basi hawajali Zanzibar kuwa Raisi kashirikis au hakushirikishwa wachabaini Raisi Z’bar na Spika na wajumbe wa Baraza wengi ni wao ccm/smz kwa hio hawawezi kwenda kinyume na wao, lakini tushukuru chadema mswada haukupita, mama Wazanzibar hatukupiga kura ya maoni kumuonyesha Pinda kuwa Muungano basi ,basi kwa Tamaa ya wawakilishi wetu bado ni mtehani .
  Mfano zaifu tu spika wa BLW Kificho kulikuwa na sababu gani za kuificha mswada wa Mh Jussa? Bila hata wakutolewa hoja Ktk baraza za wajumbe? Hawa ndio makatili wa Zanzibar na wenye kuwafuata hawa ni Firauna na watu wake.
  Hawa ndio waliotia chokochoko hata Serekali ya SUK isiwe wakenda kwao Makundushi kujaza kasumba, tusitafute wachawi wa Zanzibar ni Wazanzibar wenyewe, lakini Ishaallah M/mungu atawauwa vifo vibaya vyakuteseka kufa huku wanajiona, hakuna kiongozi hata moja Zanzibar asio na Presha ana Sukari hata bado dunia nitamu lakini tutaiasha hapa hapa na Mungu akiwatia makuchani ndipo hapo watakapo kumbuka katiba na ilani na sera za chama?.
  Kila mwenye wazifa M/mungu atamuhukumu kwa jinsi alivyo utumia, wanafiki hukumu zao jee?
  Mungu ibariki Zanzibar.
   
 2. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hiki ulichoandika hapa ndo kizanzibari, kipemba au kiunguja??? Ila usikonde, binafsi nimekuelewa baada ya kutumia kamusi ya kiloliondo! Nitarudi baadaye!!!
   
 3. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ,,,,,,Mwisho wa siku hata wewe na MAHASIRA yako haya UTAKUFA tu,kifo ni kifo tu hata kama utakufa kwa namna ya JABU au kimya kimya kitandani kwako,,,,,,pole kaka inaonesha haya mambo ya TANZANIA hakika yanakunyima usingizi kweli kweli.:help::help:
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi wazanzibar hawana kazi za kutosha kila siku kelele.
   
 5. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  HAWA WAZANZIBAR WATAIIBIA TANGANYIKA MPAKA DHAMBI SASA INAFUNUA NA ETI WAO NDIO WANALALAMIKA...
  MZANZIBARI ni bingwa wa KUBONYEZA, ukitulia anazamisha kidogo kidogo, na ndivyo inavyo fanywa Tanganyika na watu wake.
  Wazanzibari ni asilimia 2 ya watu wa Tanzania, unalalamika wakipewa mgao wa asilimia 5.4? hapo wewe mwenyewe hutendi haki.
  Watanganyika tumedanganywa na kuifuta serikali yetu na kuikumbatia serikali ya UMOJA WA KITAIFA yaani ya MUUNGANO, hawa wajanja wa ZNZ wakaendelea na kuitunza kuiboresha serikali yao na Taasisi zake kibao na Bora kuliko za Bara manake wanasaidiwa sana na Wazungu, na wamesonga mbele kuliko Bara kwa mambo mengi mfano mmoja Vitambulisho vya Mzanzibari miaka 4 iliyopita, na ni bora, zimetengenezwa Zanzibar, kwa technology ya msaada wa Israel, huku yule yule Waziri Nahodha iliyekuwa Kiongozi wa Serikali ya ZNZ anaiongoza Wizara inayotea ID za wabara na eti tenda anawapa Maustaadh wa Malaysia, yao Israel, nchi hizi wapi na wapi? kwa nini?
  Licha za Zanzibar kuwa na serikali nyepesi na shapu kushugulikia mambo ya Zanzibar, pia wamo Bara kwenye hiyo inayoitwa Serikali ya UMOJA yaani MUUNGANO, lakini mbona wamejaa wazanzibar wanaotutawala kwa kutunyonya wakipuliza? hata Muungano isivunjike, lakini Zanzibar ishatuacha, na ndio maana sasa wanatukoromea, katika watalii wazungu wanafurika zanzibar, kati yao wamejaa wataalamu wa kila aina, kwa kiasi fulani serikali ya UMOJA yaani MUUNGANO imekuwa mzigo kwa Zanzibar, mfano kutoa mzigo bandarini zanzibar ni kati ya siku 1 na 3, bara ni aibu ya kimataifa na dunia yote inajua, hii ni kwa sababu ya ukubwa wa serikali na wamejaa watu wa kuteuliwa kwa sababu eneo wanalotoka mfano wazanzibari.
  Wawekezaji Zanzibar wanaambiwa wasiende bara ni hatari, bara wanaambiwa tuna kisiwa kuzuri cha Znz, na hata kwenye matangazo ya Zanzibar ni marufuku neno Tanzania, wao wanasema kisiwa cha bahari ya Hindi kilichopo mashariki mwa bara la afrika, huu kama si unyama ni nini? kwa nini watuongoze mara mbili? Tanganyika ni Coloni la Zanzibar? Tabazamu zetu za bara zimetuponza huku hatusikii kidole cha Mzenji kimezama? ni lipi lifanyike? au na wao waifute serikali ya ZNZ yaani SMZ na kuingia ndani ya serikali moja ya UMOJA yaani MUUNGANO, na waingize katika mamlaka ya Rais baraza la MAPINDUZI lile lenye mamlaka zote za KUTANGAZA VITA, pia vikosi imara vya MAJESHI YA ZANZIBAR iingie kwenye mamlaka ya Rais wa Muungano sio kama sasa ni watiifu wa Rais wa Zanzibar na waziri wake wa VIKOSI yaani Majeshi au kwa usafi zaidi ni WAZIRI WA ULINZI WA ZANZIBAR, au basi tupewe na sisi kijiserikali cha Tanganyika, na wapewe wachapakazi wenye mawazo ya kileo waikimbize haraka kama japo tutakuwa kama Zanzibar.
  Wizara zote zinazosemekana za Muungano hamna, kwani Zanzibar inazo nyengine hizo hizo, WAZARA YA FEDHA ETI NI YA MUUNGANO? aliyekuwa naibu waziri wa fedha wa muungano amepewa wizara katika ofisi ya rais inayoshugulikia fedha na uchumi, sasa hiyo ni wizara gani? ulinzi nimeshaelezea, na mengine mengi tu.
  au TANGANYIKA MMEPENDA KUBONYEZWA NA MUJAHIDINA MZANZIBAR? BASI INAMENI WAMALIZE HAJA.... pole wabara
   
 6. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ,,,,,Duuh juzi katika zile sherehe za muungano jopo zima la viongozi lilijazwa na akina AMIII,,,yaani kuanzia makamu wa raisi MUUNGANO ni mgunya,rais wa zenji mpemba,makamu wa kwanza wa rais mgunya,makamu wa pili wa rais zenji mpemba,nikamuona mstaafu Salmin na mzee Mwinyi wote hawa walikuepo,nia yangu nikuonesha kua huko juu kwenye uongozi,kichwa toka Tanganyika ni kikwete tu,lakini bado wazee hawaridhiki.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...