Hakuna siku CCM Zanzibar ilipata tabu kama tarehe 25 - 28 Oktoba, 2015

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Kama mtakunbuka hali ilikuwa tete Zanzibar kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa 2015 Zanzibar.

CCM ilikuwa na hali Mbaya katika Maeneo yote. Uwe po Wa GNU kilikuwa kikwazo cha kwanza.
Kukataliwa kwa ccm na wazanzibari kilikuwa kikwazo cha pili.
GNU kuliinyima CCM Zanzibar

bar Uhuru waliouzoea kuchezea daftari LA kura na kuamua walivyojisikia walau kwa asilimia Fulani ingawa hawakuacha kamwe Kufanya rafu zao.

Kuanzia tarehe 25 Oktoba, viongozi Wa ccm walikuwa wanahaha na hawakuaminiana. Hawakuwaamini hata makada
wao watiifu.

CCM ilikuwa na hofu ya usaliti miongoni mwao.

Unaambiwa baada ya kupokea taarifa za kushindwa kura za urais katika majimbo mkakati yaliyokuwa yakitarajiwa kuweka hesabu sawa, pale kisiwa ndui zilipo Ofisi za ccm ilikuwa hapakaliki. Lawama zilianza kuelekezwa kwa Dr Shein Kuwa Anataka kusaliti mapinduzi.

Vikao vilikuwa haviishi na baadhi ya makada walianza kukata Tamaa. Kadiri muda ulivyoyoyoma matokeo yaliwaacha mkono.

Wapinzani waliweka mkakati Wa kihistoria ambapo hadi SAA sita usiku matokeo wameyakusanya yote. Usiniulize wali fanya nini tambua wazanzibari wanataka mabadiliko.

Wahafidhina hawakuamini, walianza kurushiana maneno.walilaumiana na kushutumiana uzembe.

Mkakati Wa upinzani na mtandao wao ulikuwa smart sana. Ushauri Wa kitaalamu ulishauri makamo Wa Rais Wa kwanza Wa Zanzibar na mgombea Wa Ukawa kupitia CUF wakati Huo Maalim Seif ajiripuwe kwa kutangaza matokeo kutoka vituoni kote Unguja na Pemba. Yale matokeo yalikuwa rasmi kutoka kwenye fomu rasmi za tume.

Mawakala Wa CCM kwenye tume wakiongozwa na Jecha walitaharuki

Ghafla Jecha akaingia mitini na kituo cha kikuu cha kukusanya matokeo kikwekwa undesiege ya Jeshi LA JMT.

Kwa mara nyengine tena maamuzi ya wazanzibari yaliporwa.

Huko Ofisi za CCM hali ilikuwa Mbaya na hawakuamini. Matokeo yalishajulikana kote na mikakati yao iilishafeli. Kwa kawaida CCM haisubiri Namba ziwaache lkn Mara hii namba ziliwaacha.

Taharuki ilishaingia ikawa wanasubiri hat ma yao.

CCM wamshukuru Kikwete Kama amir Jeshi. Kilichofanyika Zanzibar ni uporaji Wa Jeshi. CCM Kama chama Zanzibar walishaishiwa Mbinu. Ghafla Jecha anasikika anafuta uchaguzi wote

Wakati Huo dunia imeshaarifu uchaguzi ulikuwa safi. Hio ikawa Aibu ya mwaka hadi Leo.

CCM walifura, nakumbuka ghafla akina Kificho, Shamsi Nahodha, Vuai Ali Vuai alikuwa Naibu Katibu Mkuu walipewa airtime live kule ZBC TV, walikuwa wametaharuki na macho kuwatoka wakifoka.

Ilimradi CCM ilipata tabu Zanzibar.

Tunasubiri mazingaombwe mengine kwenye uhai mwaka huu Wa 2020.

Ana kweli kukataliwa kubaya.

Kishada.
 
Hakuna taabu yeyote ila ni maalim seif aliwadanganya wapiga kura wake kuwa ameshinda Uchaguzi ili hali akijua ameshindwa

Alijua amevunja sheria za Uchaguzi
KDa Hiyo uchaguzi wa oktoba 2015 ulijuaje kuwa Maalim Seif alishindwa
 
Mwaka huu rafu ile ile, ila consequences zitaacha hawa wahuni mdomo wazi. Nimemaliza.
Zaidi kwa sasa wanacheza na namba za wapiga kura na mipaka ya Majimbo. Said I ya hapo ni kufuta uchaguzi wote. Jecha's principle
 
Kinachoendelea ni kuwayima watu vitambulisho ili wakose haki ya kupiga kura.
 
Sasa zinarudi zama za zamani... Uko Pemba watu wananyimwa vitambulisho vya mzanzibari sasa.
 
Wenyewe husema mzowea Vya kunyongaa Vya kuchinja haviwezi. Bila hivyo ccm ni ngumu kushinda. Lkn hawakosi majibu. Wanajitengenezea maswali na majibu yake kabisa. Wakikosa majibu kabisa watakwambia nenda mahakamani.
 
Kama mtakunbuka hali ilikuwa tete Zanzibar kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa 2015 Zanzibar.

CCM ilikuwa na hali Mbaya katika Maeneo yote. Uwe po Wa GNU kilikuwa kikwazo cha kwanza.
Kukataliwa kwa ccm na wazanzibari kilikuwa kikwazo cha pili.
GNU kuliinyima CCM Zanzibar

bar Uhuru waliouzoea kuchezea daftari LA kura na kuamua walivyojisikia walau kwa asilimia Fulani ingawa hawakuacha kamwe Kufanya rafu zao.

Kuanzia tarehe 25 Oktoba, viongozi Wa ccm walikuwa wanahaha na hawakuaminiana. Hawakuwaamini hata makada
wao watiifu.

CCM ilikuwa na hofu ya usaliti miongoni mwao.

Unaambiwa baada ya kupokea taarifa za kushindwa kura za urais katika majimbo mkakati yaliyokuwa yakitarajiwa kuweka hesabu sawa, pale kisiwa ndui zilipo Ofisi za ccm ilikuwa hapakaliki. Lawama zilianza kuelekezwa kwa Dr Shein Kuwa Anataka kusaliti mapinduzi.

Vikao vilikuwa haviishi na baadhi ya makada walianza kukata Tamaa. Kadiri muda ulivyoyoyoma matokeo yaliwaacha mkono.

Wapinzani waliweka mkakati Wa kihistoria ambapo hadi SAA sita usiku matokeo wameyakusanya yote. Usiniulize wali fanya nini tambua wazanzibari wanataka mabadiliko.

Wahafidhina hawakuamini, walianza kurushiana maneno.walilaumiana na kushutumiana uzembe.

Mkakati Wa upinzani na mtandao wao ulikuwa smart sana. Ushauri Wa kitaalamu ulishauri makamo Wa Rais Wa kwanza Wa Zanzibar na mgombea Wa Ukawa kupitia CUF wakati Huo Maalim Seif ajiripuwe kwa kutangaza matokeo kutoka vituoni kote Unguja na Pemba. Yale matokeo yalikuwa rasmi kutoka kwenye fomu rasmi za tume.

Mawakala Wa CCM kwenye tume wakiongozwa na Jecha walitaharuki

Ghafla Jecha akaingia mitini na kituo cha kikuu cha kukusanya matokeo kikwekwa undesiege ya Jeshi LA JMT.

Kwa mara nyengine tena maamuzi ya wazanzibari yaliporwa.

Huko Ofisi za CCM hali ilikuwa Mbaya na hawakuamini. Matokeo yalishajulikana kote na mikakati yao iilishafeli. Kwa kawaida CCM haisubiri Namba ziwaache lkn Mara hii namba ziliwaacha.

Taharuki ilishaingia ikawa wanasubiri hat ma yao.

CCM wamshukuru Kikwete Kama amir Jeshi. Kilichofanyika Zanzibar ni uporaji Wa Jeshi. CCM Kama chama Zanzibar walishaishiwa Mbinu. Ghafla Jecha anasikika anafuta uchaguzi wote

Wakati Huo dunia imeshaarifu uchaguzi ulikuwa safi. Hio ikawa Aibu ya mwaka hadi Leo.

CCM walifura, nakumbuka ghafla akina Kificho, Shamsi Nahodha, Vuai Ali Vuai alikuwa Naibu Katibu Mkuu walipewa airtime live kule ZBC TV, walikuwa wametaharuki na macho kuwatoka wakifoka.

Ilimradi CCM ilipata tabu Zanzibar.

Tunasubiri mazingaombwe mengine kwenye uhai mwaka huu Wa 2020.

Ana kweli kukataliwa kubaya.

Kishada.
Shein anaswali ilikuwa ni wakati mgumu Sana kuisaliti Imani yake kutoshiriki uporaji dhuluma.Wa bara ndio walimforce kushiriki dhambi.
 
Wenyewe husema mzowea Vya kunyongaa Vya kuchinja haviwezi. Bila hivyo ccm ni ngumu kushinda. Lkn hawakosi majibu. Wanajitengenezea maswali na majibu yake kabisa. Wakikosa majibu kabisa watakwambia nenda mahakamani.
Huwezi ukaishinda ccm mahakamani
 
Ushauri Wa kitaalamu ulishauri makamo Wa Rais Wa kwanza Wa Zanzibar na mgombea Wa Ukawa kupitia CUF wakati Huo Maalim Seif ajiripuwe kwa kutangaza matokeo kutoka vituoni kote Unguja na Pemba. Yale matokeo yalikuwa rasmi kutoka kwenye fomu rasmi za tume.

Mawakala Wa CCM kwenye tume wakiongozwa na Jecha walitaharuki
Ile timu unayoita ya wataalamu ilikuwa ni timu ya wana CCM waliowekwa ndani ya CUF NDIO WALIMSHAURI Seif atangaze matokeo kinyume na katiba na sheria za uchaguzi za zanzibar ili mkurugenzi wa tume apate uhalali wa kufuta matokeo.Sababu kisheria ni tume tu ndio inayotakiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi zanzibar sio mgombea !!!

Maalimu Seif Akaenda kichwa kichwa kujitangaza kuwa yeye ndie mshindi wa uraisi alivyo mjinga.Baada ya kujitangaza JECHA akapata sababu akafuta matokeo yote.

Alipofuta Seif akawarudia hao wataalamu wa CCM waliokuwa CUF AMBAO YEYE hakuwajua undani wakamshauri asusie uchaguzi aende mahakama ya kimataifa ya ICJ wao watalisimamia!!! akazira kumbe wenzie wanapiga chini kuhakisha Zanzibar CUF haipati mbunge,wala mjumbe wa baraza la wawakilishi!! CUF IKAPIGWA CHINI YOTE KAMA ILIVYO
Zanzibar nzima!!! Mission acomplished

Baada ya hapo Seif hakuna cha kwenda mahakama ya kimataifa wala nini akawa anahangaika na migogoro iliyopikwa na wana CCM ndani ya CUF KUTWA MAHAKAMANI AKAPIGWA mateke out CUF sasa Hivi anapumulia mashine ACT WAZALENDO na HUKO ATAKUTANA NA WANA CCM NDANI YA ACT WAZALENDO karuka mkojo kakanyaga mavi

Mleta mada hadi hapo nani alipata taabu tarehe hizo kati ya CCM na CUF YA MAALIMU SEIF?
 
Akaenda kichwa kichwa kujitangaza kuwa yeye ndie mshindi wa uraisi alivyo mjinga.Baada ya kujitangaza JECHA akapata sababu akafuta matokeo yote.

Alipofuta Seif akawarudia hao wataalamu wa CCM waliokuwa CUF AMBAO YEYE hakuwajua undani wakamshauri asusie uchaguzi aende mahakama ya ulaya wao watalisimamia!!! akazira kumbe wenzie wanapiga chini kuhakisha Zanzibar CUF haipati mbunge,wala mjumbe wa baraza la wawakilishi!! CUF IKAPIGWA CHINI YOTE KAMA ILIVYO
Zanzibar nzima nzima!!! Mission acomplished katoka hapo Seif hakuna cha mahakama ya kitaifa wala nini akawa anahangaika na migogoro iliyopikwa na wana CCM ndani ya CUF KUTWA MAHAKAMANI AKAPIGWA mateke out CUF sasa Hivi anapumulia mashine ACT WAZALENDO na HUKO ATAKUTANA NA WANA CCM NDANI YA ACT WAZALENDO karuka mkojo kakanyaga mavi

Mleta mada hadi hapo nani alipata taabu tarehe hizo kati ya CCM na CUF YA MAALIMU SEIF?
Haki ipo itachelewa tu,ngoja kikishaputika hiki kizazi cha wezi kura kwanza
 
Ile timu unayoita ya wataalamu ilikuwa ni timu ya wana CCM waliowekwa ndani ya CUF NDIO WALIMSHAURI Seif atangaze matokeo kinyume na katiba na sheria za uchaguzi za zanzibar ili mkurugenzi wa tume apate uhalali wa kufuta matokeo.Sababu kisheria ni tume tu ndio inayotakiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi zanzibar sio mgombea !!!

Maalimu Seif Akaenda kichwa kichwa kujitangaza kuwa yeye ndie mshindi wa uraisi alivyo mjinga.Baada ya kujitangaza JECHA akapata sababu akafuta matokeo yote.

Alipofuta Seif akawarudia hao wataalamu wa CCM waliokuwa CUF AMBAO YEYE hakuwajua undani wakamshauri asusie uchaguzi aende mahakama ya kimataifa ya ICJ wao watalisimamia!!! akazira kumbe wenzie wanapiga chini kuhakisha Zanzibar CUF haipati mbunge,wala mjumbe wa baraza la wawakilishi!! CUF IKAPIGWA CHINI YOTE KAMA ILIVYO
Zanzibar nzima!!! Mission acomplished

Baada ya hapo Seif hakuna cha kwenda mahakama ya kimataifa wala nini akawa anahangaika na migogoro iliyopikwa na wana CCM ndani ya CUF KUTWA MAHAKAMANI AKAPIGWA mateke out CUF sasa Hivi anapumulia mashine ACT WAZALENDO na HUKO ATAKUTANA NA WANA CCM NDANI YA ACT WAZALENDO karuka mkojo kakanyaga mavi

Mleta mada hadi hapo nani alipata taabu tarehe hizo kati ya CCM na CUF YA MAALIMU SEIF?
Muoneni huyu lihidaya.
Nakushauri pitia tena mada utaelewa namna CCM ilivyoapata tabu.

Mambo yalishaharibika ndio maana Jecha alishingizia kushikwa na tumbo LA kuharisha. Matusi kwa viongozi wakubwa Wa ccm yalishaanza kutoka kwa wahafidhina kwamba wanasaliti mapinduzi. Ccm haijui neno kushindwa ndio imedekezwa Hivyo. Ikifika mahala ukatenda haji utaandamwa kwa kutenda haki.

Mbele ya macho ya kadamnasi Jeshi likavamia kituo kikuu cha majumuisho bwawani. Jecha akawekwa kwenye kituturi chini ya mtutu akalazimishwa kufuta uchaguzi wote na sio labda sehemu uliyoharibika Tu.

Wakati huo fomu za matokeo zilishasainiwa zote na hakukuwa na malalamiko yoyote Siku mbili baada ya uchaguzi.

Mara Hii mbinu zilienda mrama na Namba zikawacheza. Wakabaki watupu kuiabisha
 
Wenyewe husema mzowea Vya kunyongaa Vya kuchinja haviwezi. Bila hivyo ccm ni ngumu kushinda. Lkn hawakosi majibu. Wanajitengenezea maswali na majibu yake kabisa. Wakikosa majibu kabisa watakwambia nenda mahakamani.
mimi kinachoniudhi ni pale CCM Zanzibar ikijitesa kwa kuwanyima vitambulisho wapemba ama kujaribu kuyaunganisha majimbo ili kupunguza wabunge/wakilishi wa chama cha upinzani. Mateso yote ya nini haya kujipa wakati wanaweza kupindua matokeo vyovyote vile? wananshangaza kweli. Si washasema kuwa nchi haitoki kwa makaratasi!
 
Zaidi kwa sasa wanacheza na namba za wapiga kura na mipaka ya Majimbo. Said I ya hapo ni kufuta uchaguzi wote. Jecha's principle
Historia ya uchaguzi Zanzibar tangu enzi za wakoloni wazungu ni hiyo hiyo. Je 1995 ilitumika principle ya nani!
 
ama kujaribu kuyaunganisha majimbo ili kupunguza wabunge/wakilishi wa chama cha upinzani.
Historia ya uchaguzi Zanzibar tangu enzi za wakoloni wazungu ni hiyo hiyo. Kuna wakati idadi ya majimbo kwa Unguja na kwa Pemba ilikuwa inalingana. Kwa sasa hali ikoje? Hiyo ndiyo mikakati ya kisiasa tangu zamani,
 
Back
Top Bottom