Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,844
- 43,313
Wasalaam Wanajf.
Baada ya kusikia kelele nyingi kutoka bungeni kuwa Makonda amedharau/kashifu bunge hivyo kutakiwa kufika kwenye kamati kujieleza nimeshangazwa sana na ilinibidi nirudi kwenye video hasa ya jana pale Makonda akiongea na waandishi wa habari lakini nimeshindwa kupata sehemu ambapo Makonda amedharau/kutukana/kukashifu bunge.
Labda wengine mnisaidie kusema ni wapi na ni vipi Makonda kadharau bunge au kulikashifu?
Kumbukumbu zinaonesha kuwa baadhi ya wabunge ndio wamekuwa wakilitumia bunge kukashifu,kutukana, kudharau wengine kwa kisingizio kuna kinga...na hawa wanao kashifu huwa hawapewi nafasi ya kujitetea bado najiuliza kuwa wao ndio wameona wameguswa? kwanini na wao wasiondolewe hiyo kinga?
Hizi hasira za wabunge hazitokani na kile wanachosema kuwa bunge limedharauliwa bali wana ajenda nyuma dhidi ya Makonda lakini ukweli ni kwamba watagonga mwamba safari hii....
Wabunge wanacho hitaji sio bunge kuheshiwa bali wanahitaji Makonda avuliwe ukuu wa Mkoa.
Makonda hajaanza kuandamwa leo wala jana ni siku nyingi sana hivyo kwa sasa wanachotaka kujaribu ni kumshinikiza Rais kutengua ukuu wa mkoa wa Makonda.
Hawa wabunge wanaotaka waheshimiwe na wakuu wa wilaya na mikoa wao wamekuwa wakivunja sheria makusudi huko uraini wakidhani kinga hiyo inaendelea wakati wao wanatakiwa kuhakikisha hawavunji sheria za nchi lasivyo lazima watakutana na mikono ya dola.
Kama mlisikia wabunge hawa wakichangia kuhusu wanacho kiita kudharauliwa kwa bunge basi mtakubaliana nami kuwa wanae muhitaji sana ni Makonda na kwenye hili wengi wameungana.
Wasalaam...