Hakuna sehemu inayonuka kama Magogoni njia ya kuelekea ferry kwenye kivuko

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,023
40,693
Yaani hata gari liwe na A/C kali vipi, ukishafika pale kwenye geti la ofisi ya waziri mkuu unapoanza kushuka kile ki-slope, una pigwa na harufu kali na mbaya ajabu, yaani hakuna maneno katika kamusi ya kiswahili yanayoweza kuelezea hiyo harufu.

Nilichogundua ni kwamba mita kama 100 mbele ya geti la ofisi ya waziri mkuu kule ilipo bahari kuna malori ya maji ya chooni huwa yana-off load maji taka pale. Na upande wa kulia opposite na fensi ya Ikulu kuna soko chafu chafu la samaki, ni chafu na linanuka mno!

Maswali: hivi hakuna namna yoyote ya kuliweka soko katika hali ya usafi? Hakuna namna ya kuboresha miundo mbinu ya mifereji ya maji inayooza taka za samaki? Hakuna namna ya kuziba mashimo makubwa njia ya kuingia kituo cha mabasi ferry mita chache toka Ikulu? Yale maji ya mavi ni lazima yapelekwe kumwagwa karibu na ikulu? Maswali ni mengi, ila la msingi, watumishi ofisi ya waziri mkuu huwa wanavaa masks za kuziba pua? Au wanaishije?
 
asilimia 80% ya jiji la kizamani la DAR linanuka kama mzoga,ndio maana wenyeji wa huko wakija mikoani,hasa mikoa ya nyanda za juu huwa hawataki kurudi kwao baada na kukutana na hewa fresh kutoka milimani..
 
Back
Top Bottom