Hakuna rafiki wa kweli katika dunia hii, wengi wako kimaslai

Nyinyi nyote mpo sahihi embu jipigieni makofi !!.
  • Fikiria marafiki wako wale wa udogoni mpaka sasa hivi, wako wapi sasa? je bado uko nao?
  • Fikiria marafiki uliosoma nao, wengine wana vyeo, wengine matajiri, wengine bado wanataabika ....je bado mna ule ukaribu wa zamani?
  • Fikiria marafiki uliowapata kazini, au katika miangaiko yako...je wanathamini utu wako?
  • Fikiria ule urafiki wa wazazi wenu mpaka wengine mkaanzisha family friend...baada ya wazazi kufariki, je urafiki ule wa karibu bado upo?
  • Fikiria umepata marafiki kutokana na nafasi ulionayo, labda we ni bosi na kwa sasa umefukuzwa kazi, je ule ukaribu na marafiki zako bado upo?
  • Fikiria mpenzi uliyenaye kwa sasa mnakula bata na anakuita honey, baada ya muda ukapata janga la kupofuka macho na ukawa unajisaidia haja kubwa ndani ya mavazi yako.....Je atakupa heshima kama mwanzo?
  • Leo uko hoi kitandani mahututi, Je wale marafiki zako mliokuwa mnakula nyama choma na mvinyo.... bado wako karibu na wewe?
  • Rafiki wa kweli ni watoto wako....wekeza kwa damu yako, kama unauwezo fyatua wa kutosha na uwape misingi mizuri; ndio watakuwa mkombozi wako pale sisi wapembeni tutakapokutenga.
Rafiki wa kweli Yesu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom