mistari4G
JF-Expert Member
- Feb 10, 2019
- 553
- 649
Mnajitahidi sana kumsafisha jamaa. Lakini ukweli ni kuwa hotuba anazoziona ni hisia zinamharibia sana. Mara nyingi hujikuta katamka maneno yasiofaa kutamkwa na amiri jeshi. Ukizingatia kauli ya amiri jeshi ni sawa na amri.Kuna upotoshaji mwingi sana anaoufanya Tundu.Hasa la Rais kuruhusu Askari wapandishwe vyeo kwa kuua Raia.
Kilichosemwa na Mhe Rais ni Askari asikamatwe kwa kosa la yeye kupambana na kuhatarisha usalama wake na jambazi!Alienda mbele zaidi katika mapambano ya aina hiyo na wahalifu ni vyema Askari wakapewa kongole na ikibidi wapandishwe vyeo kwa kutimiza wajibu wao vyema.
Sasa sijui huyo Tundu anapata wapi nguvu na ujasiri wa kutuhumu uongo kwa kiwango kile!
Anyway,malipo ya uongo wake soon yatajibu.
Aseme hakumaanisha kwani yeye ndiye anayetafsiri maneno ya rais. Rais alisema na alikosea kunatakiwa kuwepo utawala wa sheria na sio watu wachache kuamua nini kifanyike. Kama kuua.Sasa kwa nini Tundu asiseme kweli kwamba Mhe Rais hakumaanisha vile na anabaki kusema uongo kwamba Magufuli karuhusu Askari waue Raia wema?
Hoja je ni kweli mhe Rais alitamka bayana km kile Tundu anavyotaka kuaminisha watu?