Siku hiyo hiyo ndiyo aliyopigwa risasi Tundu Lisu Mama sikoseiNadhani ipo na nyingine inasema wale wanajeshi wanajua wanaosaliti huwa wanawafanya nini??? Ilikuwa wakati wa kuzuia makinikia kama nakumbuka vizuri.
Hata wewe unaweza kudhaniwa ni jambazi ukauawa...Kuna neno hapo alitamka ruksa kuua Raia wema?
Je ni nani anayeamua mtu fulani ni jambazi au la??
Je unajua wale mapolisi walio muua mdogo wake Heche akiwa amefungwa pingu nao pia waliachiliwa kwa kauli hiyo??
Utawala wa sheria uko wapi??
Sasa kwa nini Tundu asiseme kweli kwamba Mhe Rais hakumaanisha vile na anabaki kusema uongo kwamba Magufuli karuhusu Askari waue Raia wema?
Ameruhusu polisi kuua na akasema wakuia wapandishwe vyeo, hiyo nyongeza ya maelezo unayotoa ni ya kwako na sivyo alivyosema.Kuna upotoshaji mwingi sana anaoufanya Tundu.Hasa la Rais kuruhusu Askari wapandishwe vyeo kwa kuua Raia.
Kilichosemwa na Mhe Rais ni Askari asikamatwe kwa kosa la yeye kupambana na kuhatarisha usalama wake na jambazi!Alienda mbele zaidi katika mapambano ya aina hiyo na wahalifu ni vyema Askari wakapewa kongole na ikibidi wapandishwe vyeo kwa kutimiza wajibu wao vyema.
Sasa sijui huyo Tundu anapata wapi nguvu na ujasiri wa kutuhumu uongo kwa kiwango kile!
Anyway,malipo ya uongo wake soon yatajibu.
Hoja je ni kweli mhe Rais alitamka bayana km kile Tundu anavyotaka kuaminisha watu?
Na mimi nilitaka nimwambie hivyo ....kwa kauli ya raisi maana yake ni kwamba yeyote atayeshukiwa kwa ujambazi asipelekwe mahakamani apigwe risasiUnaongea utoto gani? Rais ni mahakama kwamba anajua nani ni raia mwema? Utaratibu wa mtu asiye rais mwema ni kuuliwa na polisi? Hivyo ndio sheria zetu zinavyotaka au ni utashi wa rais?
Ujumbe mzuriHata tutetee vipi, kauli ya Rais kuruhusu Polisi kuua watuhumiwa, ilikuwa ni kauli mbaya kabisa kuwahi kutolewa na kiongozi mkuu kama yeye ambaye alistahili kuwa mfano wa kuzingatia sheria.
Polisi wetu hawa ambao huwawekea watuhumiwa hata bangi, huua raia na kusingizia kuwa ni majambazi, huua mahabusu na kusingizia wamekufa vifo vya kawaida, leo kiongozi mkuu anawaruhusu waue watuhumiwa, na wakiua wasishtakiwe bali wapandishwe vyeo, kauli hiyo ilimshtua kila mwenye akili timamu.
Narudia tena, ile kaulinilikuwa mbaya kabisa ambayo sidhani kama kuna kiongozi mkuu yeyote, hata yule mbaya namna gani, aliwahi kuotamka dhidi ya raia wake.
Kuna neno hapo alitamka ruksa kuua Raia wema?