Hakuna ombwe la uongozi nchini ~ "Mwalimu mkuu wa watu" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna ombwe la uongozi nchini ~ "Mwalimu mkuu wa watu"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Imany John, Sep 20, 2012.

 1. Imany John

  Imany John Verified User

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  RAIS wangu matukio yanayotokea nchini mwetu hivi sasa yanaihuzunisha roho yangu kiasi cha kufa! Ole wao, watesao na kuua mwili sasa kwa maana majira yaliyoamriwa yanawadia.

  Watakula majivu kama chakula na kukichanganya kinywaji chao na machozi yao! Wakati huu mgumu wananchi wangetegemea kiongozi wao awe ni mtu wa kuwapa faraja, lakini anapotokea waziri na kufyatuka akisema: "Mtapata wapi waziri kama mimi", anayapoteza hata yale matumaini kidogo ya wananchi yaliyokuwa yamebakia kwa serikali yao!

  Huyu ni waziri maskini! Nikaandika kuwa huo ni sawa na mzaha wa kitoto; lakini mwanamwema akanikosoa na kuniambia, "Mwalimu Mkuu, siyo kwamba anafanya mzaha wa kitoto, bali ndipo akili yake ilipoishia katika kufikiri.

  Chanzo: Tz daima la jana
   
Loading...