Kuna kitu viongozi labda hawaelewi au wanaelewa lakini wakaamua kukomaa, kiukweli ni kwamba baada ya mzunguko wa pesa kuwa mdogo sana mitaani kutokana na Serikali kukosa pesa, na pia kutokana na sera ya Serikali ya kuondoa pesa zake ktk mzunguko wa mabenki yetu .matokeo ni kwamba watu hawana pesa ya kununua chakula.
Lazima serikali ikumbuke kwamba mzunguko wa pesa unapokosekana mitaani athari yake ni kubwa kuliko baa la njaa, ni sawa chakula kipo cha kutosha lakini wananchi hawana uwezo wa Kununua hicho chakula.
Ukiona watu wa Mjini wanakosa pesa ya kununua chakula, basi ujue huko vijijini hali ni mbaya zaidi kwa sababu familia nyingi za waishio vijijini Mara nyingi hutegemea waishio mijini. Kwa hiyo binafsi sioni sababu ya Serikali kuendelea kurumbana na wanasiasa na Maaskofu badala yake serikali kwa haraka itafute namna ya kurudisha mzunguko wa pesa mtaani. Vinginevyo soon inaweza kutokea tatizo kubwa sana. Waziri mkuu lazima ajue, mwenye njaa Hana Aibu.