Hakuna nia ya kuondoa umasikini tanzania- a. Mkulanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna nia ya kuondoa umasikini tanzania- a. Mkulanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpekuz2009, May 11, 2012.

 1. m

  mpekuz2009 New Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ili jambo lolote lifanikiwe duniani linahitaji mambo matatu: nia, sababu na uwezo.

  Katika utelezaji likupungua moja kati ya mambo haya huwa hakuna mafanikio. Lakini jambo kubwa zaidi katika haya ni NIA.

  Katika misahafu ya Mwenyezi Mungu na mafunzo ya manabii tunausiwa kwamba kila amali ya mja huanza na nia. Hata wahenga wetu wanasema, “Penye nia pana njia.” Katika nia ndipo zilipo fikra na ubunifu, uwajibikaji na uadilifu, kujitolea na kuthamini utu.

  Kwa mnasaba na Tanzania na tatizo kubwa la kuongezeka zaidi kwa umaskini - sababu za kuondoa umaskini zipo; uwezo wa kuondoa umaskini upo; lakini nia ya kisiasa na kiuongozi ya kuondoa umaskini haipo. Kila mmoja wetu anafahamu fika kwamba kiini cha umaskini wetu si uvivu wa wananchi kwamba hawataki kufanya kazi kama wengi wa “wataalamu” wenye dhamana wanavyosema.

  FULL STORY>>>>>>

   
Loading...