Hakuna neno la kiswahili linaloweza kuwa na maana bila ya kuwa na irabu

Hakuna neno la kiswahili linaloweza kuwa na maana bila ya kuwa na irabu (a, e, i, o, u). Katika Lugha ya Kiswahili irabu ni moja ya vitu ambayo vinahitajika katika neno/maneno ya Kiswahili ili kuleta maana, hivyo hakuna neno la Kiswahili lenye maana pasipo kuwa na irabu
Lakini kwenye lugha nyingine neno linaweza kuwa na Maana hata pasipokuwa na irabu. Rejea Lugha ya kingereza ina maneno Kama vile shy, why, try, myth, n.k maneno hayo yanaleta maana sahihi pasipokuwa na irabu katika maneno hayo.

Japo inasemekana herufi Y katika Lugha ya kingereza ndio herufi muhimu na ambayo maneno mengi yasiyo tumia irabu hujumuisha herufi Y ili kuleta maana ya neno.
Ni ngumu neno la kingereza kuleta maana endapo likikosa irabu pamoja na herufi Y.
Hivyo herufi Y katika Lugha ya kingereza ni muhimu kama zilivyo irabu katika Lugha ya Kiswahili Herufi Y hutumika ili kuleta maana endapo zikikosekana irabu katika Lugha ya kingereza
... irabu ndizo herufi za sauti; bila irabu sauti haitoki katika lugha ya Kiswahili. Wakati irabu inaweza kutamkika yenyewe, herufi nyingine zote lazima ziambatane na irabu ili zitamkike; mf. (Bb) ba, be, bi, bo, bu; n.k. Hivyo, kwa usahihi zaidi mada yako ilitakiwa isomeke, "Hakuna neno la Kiswahili linalotamkika bila kuwa na irabu".
 
... irabu ndizo herufi za sauti; bila irabu sauti haitoki katika lugha ya Kiswahili. Wakati irabu inaweza kutamkika yenyewe, herufi nyingine zote lazima ziambatane na irabu ili zitamkike; mf. (Bb) ba, be, bi, bo, bu; n.k. Hivyo, kwa usahihi zaidi mada yako ilitakiwa isomeke, "Hakuna neno la Kiswahili linalotamkika bila kuwa na irabu".
Asante kwa nyongeza japo title ni kama imejitosheleza na ina maana ikiyo kamilika.
 
Na sku hizi mwenye kiswahili kuna konsonanti "x"
Mf. Xhem, xaxa, xjui
BASAT sjui BAKITA mliangalie na hili pia.
X na Q zingetolewa tu kwenye herufi za kiswahili kama waarabu walivyoiondoa P kutokana na kukosa matumizi kwenye lugha yao.
 
X-ray. ..... x wangu, ... xsirani..... xy krosomu!..... silabi ya x tunaitamka ivivo!! ....x na y grafu! yaani ziko nyoingi sema tu nyie ni vihio wa kutupwa!
X-RAYS ni kiswahili?
X wangu hio "x" inamaana gani kwenye kiswahili?
xsirani😂😂😂😂 hii ndio nini au kisirani?
 
X-RAYS ni kiswahili?
X wangu hio "x" inamaana gani kwenye kiswahili?
xsirani😂😂😂😂 hii ndio nini au kisirani?
Lugha yeyote ina uhai!! kwa kuwa inazaliwa, inaishi, inakua na inakufa!! kiyahudi alichozungumza Yesu kimekufa!! hawa wa leo wanaongea kigiriki!
 
Hizo herufi; (a,e,i,o,u) zinaitwa Vokali na sio irabu, ukiunganisha Konsonanti na vokali ndipo unapata Irabu, mfano Konsonanti " b" ukiunganisha na vokali "a" unapata Irabu "ba".

Konsonanti ----b, t, r, g, h, nk.
Vokali -----a,e, i, o, u
Irabu---- ba, be, te, go, ha, vu nk.
Hapa utakuwa umetumia mtaala wa Urusi.
 
Back
Top Bottom