Hakuna neno la kiswahili linaloweza kuwa na maana bila ya kuwa na irabu

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,047
19,696
Hakuna neno la kiswahili linaloweza kuwa na maana bila ya kuwa na irabu (a, e, i, o, u). Katika Lugha ya Kiswahili irabu ni moja ya vitu ambayo vinahitajika katika neno/maneno ya Kiswahili ili kuleta maana, hivyo hakuna neno la Kiswahili lenye maana pasipo kuwa na irabu
Lakini kwenye lugha nyingine neno linaweza kuwa na Maana hata pasipokuwa na irabu. Rejea Lugha ya kingereza ina maneno Kama vile shy, why, try, myth, n.k maneno hayo yanaleta maana sahihi pasipokuwa na irabu katika maneno hayo.

Japo inasemekana herufi Y katika Lugha ya kingereza ndio herufi muhimu na ambayo maneno mengi yasiyo tumia irabu hujumuisha herufi Y ili kuleta maana ya neno.
Ni ngumu neno la kingereza kuleta maana endapo likikosa irabu pamoja na herufi Y.
Hivyo herufi Y katika Lugha ya kingereza ni muhimu kama zilivyo irabu katika Lugha ya Kiswahili Herufi Y hutumika ili kuleta maana endapo zikikosekana irabu katika Lugha ya kingereza
 
iNine9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,568
6,123
Katika lugha ambazo sijawahigi kuzielewa kabisa basi ni Kiswahili, nakumbuka mpaka kidato cha nne nilkua napeperusha pendera hadi 15F niliwahi pata, ndiyo somo pekee nililokua nafeli ikifatiwa na Civics lakini yenyewe nilikua napata D sana mpaka walimu wa masomo wakawa wananishangaa how comes! Kidogo necta ya kidato cha nne ndo nilipata ka C ka kiswahili..

Nilikua naona somo gumu sana kwangu.
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
99,227
105,945
Ni kweli kabisa...

Bila kusahau matumizi ya herufi X kwenye kiswahili ni adimu sana...
 
Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
798
2,030
Katika lugha ambazo sijawahigi kuzielewa kabisa basi ni Kiswahili, nakumbuka mpaka kidato cha nne nilkua napeperusha pendera hadi 15F niliwahi pata, ndiyo somo pekee nililokua nafeli ikifatiwa na Civics lakini yenyewe nilikua napata D sana mpaka walimu wa masomo wakawa wananishangaa how comes! Kidogo necta ya kidato cha nne ndo nilipata ka C ka kiswahili..

Nilikua naona somo gumu sana kwangu.
Kiswahili kama lugha unaielewa vyema, maana ujuzi wa lugha yoyote duniani huzingatiwa kwanza kwenye mambo mawili;
Kuisema lugha hiyo
Kuiandika na kuisoma lugha hiyo

Sasa wewe unaongelewa ugumu wa somo la kiswahili, sio lugha ya kiswahili.

Somo linalohusu lugha ni gumu popote duniani, lugha (somo/taaluma) ni km hesabu, ni ngumu kuijua hasa kwenye
Isimu
Fasihi
 
Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,047
19,696
Nimesoma juzijuzi tu sema ni mambo ambayo yalikuwa hayanihusu sikukariri nilipita juu juu. Kama sio lugha na isimu au fonetiki na fonolojia.
Ndio ipo hivyo yaani irabu ni muhimu Sana katika Lugha ya Kiswahili.
 
Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,047
19,696
Katika lugha ambazo sijawahigi kuzielewa kabisa basi ni Kiswahili, nakumbuka mpaka kidato cha nne nilkua napeperusha pendera hadi 15F niliwahi pata, ndiyo somo pekee nililokua nafeli ikifatiwa na Civics lakini yenyewe nilikua napata D sana mpaka walimu wa masomo wakawa wananishangaa how comes! Kidogo necta ya kidato cha nne ndo nilipata ka C ka kiswahili..

Nilikua naona somo gumu sana kwangu.
Kiswahili ni kigumu na hili nimeliona nilivyo anza anza kufuatilia maneno kutoka BAKITA.
Mfano neno shurubati, kimbaka, kimemeshi n.k
 
iNine9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,568
6,123
Kiswahili ni kigumu na hili nimeliona nilivyo anza anza kufuatilia maneno kutoka BAKITA.
Mfano neno shurubati, kimbaka, kimemeshi n.k
Kuna siku niliwasikia BAKITA wakitolea maana ya neno DANGA ambalo limezoeleka sana miongoni mwetu na tunajua linatumika vipi..

Ila kwa maelezo ya BAKITA walisema maana ya neno "DANGA" au KUDANGA ni kitendo cha kutafuta kitu ambacho unajua kabisa huwezi kukipata/hakipatikani.

Ila ajabu kuna watanzania wanaDANGA na wanamiliki MADANGA

Kiswahili
 
Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,047
19,696
Kuna siku niliwasikia BAKITA wakitolea maana ya neno DANGA ambalo limezoeleka sana miongoni mwetu na tunajua linatumika vipi..

Ila kwa maelezo ya BAKITA walisema maana ya neno "DANGA" au KUDANGA ni kitendo cha kutafuta kitu ambacho unajua kabisa huwezi kukipata/hakipatikani.

Ila ajabu kuna watanzania wanaDANGA na wanamiliki MADANGA

Kiswahili
Kudanga kutafuta kitu ambacho huna uwezo nacho kwa hali na mali yaani kukipigania.
 
Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Top Bottom