Hakuna nchi iliyowahi kusonga mbele kwa kukandamiza Demokrasia

Hawana hata hiyo katiba na haiwasumbui! Lakini kuhusu Demokrasi Prof. PLO Lumumba alisema nchi zenye neno demokrasi ndani ya jina lao ni zile ambazo hazina demokrasia hata chembe - Democratic Republic of Congo na Peoples Democratic of Korea! Je! vyama vyenye neno hilo mfano CHADEMA?
CHADEMA kirefu chake CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO,je DEMOKKRASIA ipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni jambo ambalo kila mwenye akili timamu alijue .

Haijawahi kutokea mahali popote duniani , na kama kuna mwenye matumaini kwamba kwa haya yanayofanyika Tanzania ya kukamata kila mwenye kufikiri tofauti na watawala kutakuja kuwa na maendeleo katika nchi , basi ni vema akatafuta kazi ya kufanya .

Hizi neema zote mnazoziona katika dunia hii hutolewa na Mungu kwa kuzingatia namna haki inavyotendwa kwenye nchi husika . HAKI HUINUA TAIFA .

Zimbabwe iwe mfano wa karibu .
Mkuu labda kama husomi historia nchi nyingi tajiri zimeendelea kwa ukandamizaji US na utumwa, China ya Mao mpaka sasa hakuna demokrasia, South Africa na ubaguzi, Uarabuni hakuna demokrasia mpaka Leo urusi ya Sterling.
Duniani ni mataifa machache sana yalipata maendeleo kwa misingi ya demokrasia.
 
Usibadilishe mada, umesema demokrasia inafanya nchi ipige hatua. Hizo ni hisia zako tu hazina ukweli. Kama unaweza kuthibitisha unachokisema taja nchi moja tu, nchi moja tu usilete porojo. Ulifikiri unajua kumbe ni tofauti kabisa, kama kweli unajua na kukifahamu unachokisema taja nchi moja tu, moja tu wala sio mbili, taja nchi moja iliyotoka kwenye umasikini ikafuata misingi ya demokrasia, moja tu.
Uyu mtoa mada kichwani hamna kitu na aeleweki anaulizwa badala ya kujibu na yeye anauliza swali na pia anapindikiza mada tofauti na aliyoandika kwa mfano mada yake ni ya demokrasia sasa ivi kabadilisha karukia kwenye katiba.

Mkuu ukijadiliana na uyu atakuumiza kichwa bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa uzi asamehewe na pia aelimishwe kwani hajui vema historia. Demokrasia ipi anayoizungumzia yeye?
Demokrasia inaweza kuwa na tafsiri tofauti kulingana na mazingira,maeneo,tamaduni,historia n.k
Kihistoria hakuna nchi iliyopata maendeleo kwa kutumia mfumo huu wa kidemokrasia wa nchi za magharibi(kibepari).Marekani,Uingereza,Ufaransa,Ujerumani,Uholanzi,Ubelgiji nk.zote hizo zilipata maendeleo bila kutumia mfumo huo wa sasa wa demokrasia.
Hata nchi za Urusi,China,Cuba, Kuwaiti,Libya ya Gaddafi,UAE,Indonesia,Malaysia, Qatar, Venezula ya Hugo Chaves,walipata maendeleo makubwa bila kufuata mfumo huo wa demokrasia.
Hata Africa Kusini ya Makaburu hakukuwa na Demokrasia bali ubaguzi lakini watu walifanya kazi kwa nguvu na kwa malengo ndio maana nchi yao ikapiga maendeleo makubwa sana kiuchumi. Mfano mwingine ni Japan nayo siku nyingi ilishapata maendeleo makubwa kiuchumi na kijeshi bila kuwa na mfumo huo wa demokrasia.
Shirikisho la iliyokuwa Yugoslavia walikuwa na nguvu kubwa sana kiuchumi na kijeshi Ulaya na Duniani hadi kutishia nchi nyingine. Ilibidi NATO ijipange vema kuweza kuisambaratisha Yugoslavia kijeshi.

Maendeleo yanaweza kupatikana kukiwa na kiongozi imara,jasiri,mzalendo,mwenye nia ya dhati kuleta maendeleo, asiye muoga,asiye msaliti,mwenye maono,mchapa kazi,mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu bila uoga,mwenye uwezo wa kutoa maagizo na kufuatilia utekelezaji wake. Pia lazima kuwe na idara za usalama zenye nguvu na weledi wa hali ya juu kupambana na wasaliti wanaorudisha nyuma maendeleo.Aidha wananchi wa nchi husika lazima wafundishwe kuwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na utii na uzalendo kwa viongozi wakuu na Serikali kwa ujumla.Maendeleo hayaji kwa watu kukaa na kuchekacheka au kupoteza muda kujadili upuuzi. Maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi.

Mheshimiwa Rais wetu analengo moja tu juu nalo ni kuwaletea maendeleo walio wengi pamoja na kujenga mfumo bora wa utawala wenye uwajibikaji,kuondoa rushwa,uonevu,kutokutii sheria,wizi,ukweoaji kodi,matumizi mabaya ya rasilimali zetu,upendeleo,uvivu. Tutaendelea kumuunga mkono Rais wetu kwa juhudi kubwa anazozifanya na nyie wapinga maendeleo mtazidi kusononeka. Poleni
 
Hili ni jambo ambalo kila mwenye akili timamu alijue .

Haijawahi kutokea mahali popote duniani , na kama kuna mwenye matumaini kwamba kwa haya yanayofanyika Tanzania ya kukamata kila mwenye kufikiri tofauti na watawala kutakuja kuwa na maendeleo katika nchi , basi ni vema akatafuta kazi ya kufanya .

Hizi neema zote mnazoziona katika dunia hii hutolewa na Mungu kwa kuzingatia namna haki inavyotendwa kwenye nchi husika . HAKI HUINUA TAIFA .

Zimbabwe iwe mfano wa karibu .
Pumba tupu.huna hoja wewe, kwa taarifa yako maendeleo hayaji kw kuchekeana chekeana,democrasia ni mtego wa kimagharibi.kutwa kucha mnabishana,!!! Mtafanya kz wakati gn??!! Rwanda.singapole.china.korea.cuba, russia,ilikuwepo pia iraq ya sadaam husein.na libya, na watu wajinga km ninyi ndio mliotumika kuiangamiza libya.na iraq.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKUU INAONEKANA HUKUSOMA KABISA ARTS ADVANCE KAMA ULISOMA HISTORY TWO KWAKO ILIKUA OPTIONS. JARIBU KUSOMA HATA KITABU CHA KATO ABUBAKAR
Hizo hadithi zako ni za mwaka gani ? kukandamiza demokrasia iliyopo na kutokuwepo kabisa kwa demokrasia ni mambo mawili tofauti , nielewe kabla hujaleta uozo wako , Tanzania ilipokuwa haina demokrasia ya vyama vingi ilifanikiwa katika lipi ?

Msiturudishe enzi za mawe , naona wewe na watu wa kiwango chako mnaleta habari za Mussolin na Hitler katika dunia ya leo .
 
Mtoa uzi asamehewe na pia aelimishwe kwani hajui vema historia. Demokrasia ipi anayoizungumzia yeye?
Demokrasia inaweza kuwa na tafsiri tofauti kulingana na mazingira,maeneo,tamaduni,historia n.k
Kihistoria hakuna nchi iliyopata maendeleo kwa kutumia mfumo huu wa kidemokrasia wa nchi za magharibi(kibepari).Marekani,Uingereza,Ufaransa,Ujerumani,Uholanzi,Ubelgiji nk.zote hizo zilipata maendeleo bila kutumia mfumo huo wa sasa wa demokrasia.
Hata nchi za Urusi,China,Cuba, Kuwaiti,Libya ya Gaddafi,UAE,Indonesia,Malaysia, Qatar, Venezula ya Hugo Chaves,walipata maendeleo makubwa bila kufuata mfumo huo wa demokrasia.
Hata Africa Kusini ya Makaburu hakukuwa na Demokrasia bali ubaguzi lakini watu walifanya kazi kwa nguvu na kwa malengo ndio maana nchi yao ikapiga maendeleo makubwa sana kiuchumi. Mfano mwingine ni Japan nayo siku nyingi ilishapata maendeleo makubwa kiuchumi na kijeshi bila kuwa na mfumo huo wa demokrasia.
Shirikisho la iliyokuwa Yugoslavia walikuwa na nguvu kubwa sana kiuchumi na kijeshi Ulaya na Duniani hadi kutishia nchi nyingine. Ilibidi NATO ijipange vema kuweza kuisambaratisha Yugoslavia kijeshi.

Maendeleo yanaweza kupatikana kukiwa na kiongozi imara,jasiri,mzalendo,mwenye nia ya dhati kuleta maendeleo, asiye muoga,asiye msaliti,mwenye maono,mchapa kazi,mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu bila uoga,mwenye uwezo wa kutoa maagizo na kufuatilia utekelezaji wake. Pia lazima kuwe na idara za usalama zenye nguvu na weledi wa hali ya juu kupambana na wasaliti wanaorudisha nyuma maendeleo.Aidha wananchi wa nchi husika lazima wafundishwe kuwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na utii na uzalendo kwa viongozi wakuu na Serikali kwa ujumla.Maendeleo hayaji kwa watu kukaa na kuchekacheka au kupoteza muda kujadili upuuzi. Maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi.

Mheshimiwa Rais wetu analengo moja tu juu nalo ni kuwaletea maendeleo walio wengi pamoja na kujenga mfumo bora wa utawala wenye uwajibikaji,kuondoa rushwa,uonevu,kutokutii sheria,wizi,ukweoaji kodi,matumizi mabaya ya rasilimali zetu,upendeleo,uvivu. Tutaendelea kumuunga mkono Rais wetu kwa juhudi kubwa anazozifanya na nyie wapinga maendeleo mtazidi kusononeka. Poleni
Kuikataa demokrasia katika nchi ambayo Rais alichaguliwa kwa kutumia njia hiyo ni sawa na Kichaa , umeandika mengi sana lakini bila shaka hukuelewa andiko .
 
Hizo hadithi zako ni za mwaka gani ? kukandamiza demokrasia iliyopo na kutokuwepo kabisa kwa demokrasia ni mambo mawili tofauti , nielewe kabla hujaleta uozo wako , Tanzania ilipokuwa haina demokrasia ya vyama vingi ilifanikiwa katika lipi ?

Msiturudishe enzi za mawe , naona wewe na watu wa kiwango chako mnaleta habari za Mussolin na Hitler katika dunia ya leo .
Itizame tanzania toka 1992 imefanya nn??!! Nyerere kila cku mnamtukana.mwinyi kila cku mnamdharirisha.mkapa kila cku mnamtukana.kikwete yeye ss ndie alietukanwa zaidi kuliko rais mwingne yeyote tanzania.democrasia gn unayoitaka wewe?! Ile ya kupiga kura au unaongelea uhuru wa mtu??!! Democrasia ipeleke kwako na familia yako.《japo cna uhakika hata km unayofamilia》toa haki kw kila analotaka kufanya mtu wa familia yako.mruhusu mkeo avae nguo anazotaka.mruhusu arudi nyumbani mda anaotaka.waruhusu watoto wako wafanye kila wanalotaka.KM ITAKUWA FAMILIA.YEYOTE AHUBILIE UPUUZI PUA NI MPUUZI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Erythrocyte hilo ni kweli tupu..
Katika siku ambayo umenifurahisha kwa hii fact ni leo Mkuu..
Salute sana..

Hakuna maendeleo yoyote yale kwenye nyanja yoyote ile kama hakuna Demokrasia..

Ndio maana hata Foreign Investor yeyote yule kabla hajaenda popote kuwekeza one of the Key Factors anazoangalia ni Kiwango cha DEMOKRASIA cha Mahali/Nchi husika...

Na DEMOKRASIA haina mbadala.. Democracy has no alternative.. Ni DEMOKRASIA.. DEMOKRASIA.. DEMOKRASIA..

Watu wa Lumumba hamuwezi kujua hii fact mpaka wote labda mfe wazaliwe watu wapya.[/QUOTi

Inaelekea kila mtu ana mawazo yake ni nini maana ya demokrasia. Je, unaweza kuifafanua hiyo demokrasia unayoimainisha wewe? Na utaje nchi zilizosonga mbele kwa kuitumia hiyo demokrasia unayoimainisha.
 
Hili ni jambo ambalo kila mwenye akili timamu alijue .

Haijawahi kutokea mahali popote duniani , na kama kuna mwenye matumaini kwamba kwa haya yanayofanyika Tanzania ya kukamata kila mwenye kufikiri tofauti na watawala kutakuja kuwa na maendeleo katika nchi , basi ni vema akatafuta kazi ya kufanya .

Hizi neema zote mnazoziona katika dunia hii hutolewa na Mungu kwa kuzingatia namna haki inavyotendwa kwenye nchi husika . HAKI HUINUA TAIFA .

Zimbabwe iwe mfano wa karibu .
Saudi Arabia,Qatar,UAE,Turkey,China
 
Back
Top Bottom