Hakuna namna, Wazazi wa watoto shule za binafsi lazima walipe ada yote

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Kufundisha mtoto ni sawa na kujenga nyumba. Anayejenga nyumba huanza kujenga mstari wa Kwanza, halafu mstari wa pili hujengwa juu ya mstari wa Kwanza.

Hali kadhalika mstari wa tatu hujengwa juu ya mstari wa pili. Ikitokea siku ya kujengwa mstari wa pili kukatokea dharula na ujenzi usifanyike, bado dharula ikiisha mstari wa pili LAZIMA ujengwe kabla ya kujenga mstari wa tatu. Hakuna namna ya kujenga mstari wa tatu KABLA ya kujenga mstari wa pili.

Kwa hiyo mjenzi ni lazima aijenge nyumba ikamilike na LAZIMA alipwe malipo YOTE Kama walivyopatana awali.

Hali kadhalika, masomo na vipindi ambavyo watoto wangefundishwa mwezi wa nne na wa tano LAZIMA wafundishwe kabla ya kufundisha masomo na vipindi vilivyoko kwenye ratiba ya mwezi wa Saba. Ndiyo maana ni LAZIMA kutafuta nyongeza ya muda ili kufidia vipindi vilivyopotea wakati wa likizo ya dharula iliyotokana na mlipuko wa ugonjwa wa covid 19.

Kwa hiyo LAZIMA wazazi walipe ada ambayo hawakuilipa maana watoto wao LAZIMA wafundishwe na waalimu LAZIMA walipwe mishahara yao ambayo haikulipwa maana kazi wataifanya kikamilifu katika kuwafundisha watoto. Huo ndio utaratibu.

Sidhani Kama Kuna mzazi anategemea waalimu wataruka sehemu ya mada bila kuzifundisha kwa kuwa ilikuwa zifundishwe mwezi wa nne na wa tano.

Kwa mantiki hiyo haitegemewi mzazi kudhani kuwa hatadaiwa kulipa ada Yote.
 
Kulipa lazima,tulipe maana huduma itatolewa,hata kama imechelewa,
Ila lazima tuelewe kwamba,sio waalimu tu walioathirika na covid19,hata sie wazazi kuanzia march mpaka June,mapato yamepungua,kwahiyo ile ada ambayo,tulitakiwa kulipa April,ilitumika kuendeshea maisha,sasa ni busara tukiweka utaratibu ,while/walimu wapate mapato,na sie tuwe na ahueni ya kulipa,tutalipa ada yote,lakini ingekuwa vzr tulipe kidogokidogo
 
Kwani kuna watu walitaka walipe ada nusu? Mimi nililipa ada Januari ya miezi 6 nusu mwaka..mwezi wa tatu Covid 19 ikaingia sasa hivi nasubiria nilipe ya nusu mwaka uliobaki maisha yaendelee...
 
Kama nililipa ada yote ya muhula wa kwanza, hili unalizungumziaje?
 
Kwani kuna watu walitaka walipe ada nusu? Mimi nililipa ada Januari ya miezi 6 nusu mwaka..mwezi wa tatu Covid 19 ikaingia sasa hivi nasubiria nilipe ya nusu mwaka uliobaki maisha yaendelee...
Same applies. Na hiyo ya muhula wa pili na hadi wamalize mitihani ya muhula wa kwanza.
 
Kama unarisiti unawapelekea tuu kuwaonesha kuwa ushalipa.
Hadi sasa hakuna walichodai. Nilimuuliza mleta mada maana amegeneralise hajui kwamba kwa shule zenye mihula miwili ada huwa inalipwa mwanzoni mwa mwaka. Na COVD-19 imetokea ikiwa wanafunzi wanaendelea na masomo ya muhula kwa kwanza ambayo bado hawajafanya mitihani.
 
Hili ni somo kwamba kama hela zako ni za kuunga unga somesha watoto shule yenye mihula miwili, hizi shule zinazofanya za mihula mitatu sijui minne wataki mtaala wenyewe ni wa necta ni upuuzi mtupu...mara mia useme mtoto anasoma IGCSE..inaleta tija
 
Ukiona mzazi analialia kuhusu kulipa ada jua kuwa huko aliko mpeleka mwanae sio level yake anatakiwa ampeleke shule za serikali huko hakuna ada.
 
Kulipa lazima,tulipe maana huduma itatolewa,hata kama imechelewa,
Ila lazima tuelewe kwamba,sio waalimu tu walioathirika na covid19,hata sie wazazi kuanzia march mpaka June,mapato yamepungua,kwahiyo ile ada ambayo,tulitakiwa kulipa April,ilitumika kuendeshea maisha,sasa ni busara tukiweka utaratibu ,while/walimu wapate mapato,na sie tuwe na ahueni ya kulipa,tutalipa ada yote,lakini ingekuwa vzr tulipe kidogokidogo
Hiyo ndiyo hekima inayopaswa kutumika. Si lazima azilipe zote kwa Mara moja Bali utaratibu wa kulipa kidogo kidogo kwa makubaliano. Cha msingi ni kwamba makubaliano yakulipa yaeleweke.
 
Kama nililipa ada yote ya muhula wa kwanza, hili unalizungumziaje?
Hapo itakuwa huna deni. Utalipa tu mhula wa pili. Tatizo ni kwa wake ambao hulipa kwa awamu mbili kwa kila mihula. Alilipa awamu ya Kwanza Jan hadi March. Awamu ya pili April hadi June hakulipa na shule zikafungwa! Hao ndio wanataka wasilipe kwa kuwa watoto hawakufundishwa! Lakini like ambacho hawakufundishwa lazima kitafidiwa! Utata uko hapo!
 
Back
Top Bottom